Dini na Elimu za watoto wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dini na Elimu za watoto wetu!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ndyoko, Dec 14, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Wiki iliyopita nilienda shule moja mjini Dodoma kuomba fomu za kujiunga na shule. Hiyo ni shule yenye mlengo wa imani ya kikristo na kila kitu pale kinaendeshwa kikristo kristo.

  Moja kati ya vitu vinavyotiliwa mkazo na utawala kwa wanafunzi wote mbali na elimu dunia ni kwa wanafunzi kuishi na kujifunza imani ya kikristo. Ktk hili ni lazima mwanafunzi husika ajifunze imani ya kikristo na kuiishi kwa kipindi chote anapokuwa mwanafunzi wa shule husika-ikumbukwe pia kwamba anafanya mitihani pia inayojumuishwa ktk ufaulu wake na kumwezesha kuendelea darasa la mbele pindi akifaulu (naomba nieleweke hapa kuwa mimi pia ni mkristo).

  Kwa wazazi ambao watoto wao sio wakristo, ningewashauri wafikirie mara mbili kabla, maana binafsi nahisi lazima mtoto ataathirika ktk makuzi ya imani yake ya dini. Hebu fikiria mtoto anapata makuzi ya imani ya dini tofauti kwa muda usiopungua miaka 9-chekechea miaka 2, na msingi miaka 7 tena kwa kupata alama A ktk akili ya utoto hadi umri wa kwenda sekondari!

  • Je ni madhara gani yanayoweza kuja kujitokeza baadae kwa mtu wa aina hii ktk siku za mbeleni ktk kuiishi imani yake ya dini?
  • Hili linaweza kuwa na madhara kwa taifa kwa maana ya kwamba Taifa likaja kupata watu/viongozi wasio na imani ya kueleweka na hivyo kupunguza hofu yao ya Mungu na hivyo kuishia kutowathamini binadamu wenzao kwa kukosa hofu ya Mungu?
  Hebu tujadiliane!
   
Loading...