DIJITALI ni Akadabra

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Ni biashara ya watu tu ili wauze ving'amuzi vyao.Nchi yetu ilikuwa bado kuzima Analojia. Bado hatujajipanga. Wengi wanateseka...wanakosa habari.Kwani ni kweli kuwa Dijitali ni Ving'amuzi? Ndugu zangu,Dijitali ni Akadabra kama ilivyo kwa 'Freemason'.

Kama ni kweli nchi hii imedhamiria kuwa na Dijitali tu,iweje mwaka mzima mikoa nane tu ndio izimiwe Analojia.Hii sio ubaguzi wa kimaendeleo kwamba ndani ya nchi moja wengine Analojia na wengine Dijitali? Siiamini dhamira ya Serikali kuzima Analojia kwa ujumla wake. Ingewaachia wanaoihitaji kutokana na uwezo wao.
 
Pwent....pwent...pwent!
Halafu nasikia ving'amuzi vinavyouzwa sasa hivi ni nyaya, hii ni maalum kufanya biashara hii iwe endelevu hata kama Watanzania wote watakuwa wamenunua ving'amuzi.
Tanzania nchi yangu, wazazi wako wako wapi?!
 
Kweli hii yetu sijui tutafika wapi? Tulihimizwa nunueni ving'amuzi mwisho desemba 31 analojia zinazimwa mwisho tunaambiwa ni Dar tu siku zote walikuwa wapi? Mpaka kwenda mkoa mmoja mmoja? Si wangeacha kwanza waandae nchi nzima ndiyo wazime? au ni biashara za watu kuuza ving'amuzi?
 
Tumetoka kwenye "speed governor", sasa tunaenda kwenye ving'amuzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…