Diaspora wa India naomba msaada please

Caro Lynah

Member
Jul 18, 2016
71
61
Habari waungwana! Ninae rafiki yangu ambae mama yake ana hali mbaya na mwanae yupo Goa,India kutafuta maisha.

Naomba kujulishwa kuhusu ni JINSI GANI MTANZANIA ALIYEPO INDIA AMBAE AMEOVERSTAY ANAWEZA KUTUMA PARCEL TANZANIA AU HELA.

Msaada wenu wa mawazo ni wa muhimu sana.Please no bashing or rude comments.Natanguliza shukrani.
 
Ongea vizuri, ueleweke, unakata Kata maneno Sana,hakuna kinachomzuia mtu kutuma parcel eti kisa ka overstay, mimi nipo Strasbourg France, nili overstay Siku 5 lakini ya sita nikatuma pesa, kwa wazazi wangu.
immigration system ya huku wanakufuata hadi uliko sijui kuhusu India, Mimi walinifuata ila wakanitoza overstay fees ya $30.
wewe tuma Kama unatuma.
 
Habari waungwana! Ninae rafiki yangu ambae mama yake ana hali mbaya na mwanae yupo Goa,India kutafuta maisha.Naomba kujulishwa kuhusu ni JINSI GANI MTANZANIA ALIYEPO INDIA AMBAE AMEOVERSTAY ANAWEZA KUTUMA PARCEL TANZANIA AU HELA.Msaada wenu wa mawazo ni wa muhimu sana.Please no bashing or rude comments.Natanguliza shukrani.

Sijajua kama Goa kuna wabongo wengi wanaoenda kutibiwa, lakini kwa Delhi Wagonjwa wa Kitanzania wapo wengi sana na wanaingia na kutoka kila siku/Wiki, hivyo ungeweza kumpa mtu anayerudi mizigo yako

Nilikuwa Delhi mwezi wa 10-11 Mwaka jana na nilirudi na mizigo ya jamaa waliooverstay na pia wengine walinitumia fedha niwanunulie Dawa

mwambie ajaribu kuangalia kwenye Mahospital ya huko Goa
 
Habari waungwana! Ninae rafiki yangu ambae mama yake ana hali mbaya na mwanae yupo Goa,India kutafuta maisha.Naomba kujulishwa kuhusu ni JINSI GANI MTANZANIA ALIYEPO INDIA AMBAE AMEOVERSTAY ANAWEZA KUTUMA PARCEL TANZANIA AU HELA.Msaada wenu wa mawazo ni wa muhimu sana.Please no bashing or rude comments.Natanguliza shukrani.
Kwa nini msimshauri kama yeye hawezi atumie mtu anayeweza kumwamini? Atakuwa anaishi sehemu bila kuwa na rafiki hata mmoja anayeweza kumsaidia kwenye issue kama hiyo? NB: Angalieni asije akawa anawapiga changa la macho kuwa anataka kutuma chochote lakini tatizo anaogopa kwa sababu ame-over-stay huku hana namna!
 
kwa mujibu wake,alipo ni mbali sana na Delhi.sasa anataka kujua kama kuna agency sababu alimpa hela mdada anaerudi na simu uyo mdada alipotea mazima hadi leo.ndio maana yake
 
kwa mujibu wake,alipo ni mbali sana na Delhi.sasa anataka kujua kama kuna agency sababu alimpa hela mdada anaerudi na simu uyo mdada alipotea mazima hadi leo.ndio maana yake
Fedha ya siku hizi humpi mtu mkononi! Ni wachache sana wanafikisha! Mwambieni kama ni fedha atumie agents kama Western Union, MoneyGram etc. Kwa India japo sijafika lakini nadhani hawa agents wako kila kona ya nchi kwani wahindi waliosambaa kote duniani ni watumiaji wazuri sana wa haya mashirika. Kama wanauliza kitambulisho kama nilivyokwisha sema njia ni kumtafuta mtu anayemwamini na aende naye mpaka kwenye kituo cha kutumia na ahakikishe ametuma.
 
View attachment 566354

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
Picha na Makame Mshenga.
Wanabodi.

Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
DIASPORA: Home Page
or
4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

Natanguliza Shukrani.

Pascal Mayalla
+255 784 270403
pascomayalla@gmail.com
 
Back
Top Bottom