Diaspora in US 2010 - a lot to like | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diaspora in US 2010 - a lot to like

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwafrika, Jul 7, 2010.

 1. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimehudhuria mikutano/sherehe nyingi sana za watanzania walioko nje ya nchi - UK, Canada, Japan, na US. Mengi sana mazuri hutokea ila pia mabaya huwa hayajifichi (muulize Nyani Ngabu akuambie why). Kitu kimoja naweza kusema kuhusu huu mkutano wa Diaspora US 2010, kulikuwa na mengi mazuri yaliyotokea na ambayo wengi walipenda.

  Nitaendelea kuweka hapa kama muda utaruhusu, ila kwanza, nilipenda mpango wa NSSF kuhusu kuruhusu watanzania walioko nje ya nchi kushiriki kwenye mfumo wa hifadhi -

  Source ni local paper ya minneapolis - Mshale News
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu haya maneno lakini kitu kimoja tu hivi mbona tunashughulikia sana maswala ya KUFA badala ya UZALISHAJI?..Kwa nini sisi Watanzania tuna mila za kutukuza zaidi hariusi na vifo kutoa michango yetu badala ya kufikiria uwezekano wa sisi Watanzania kufungua mabanda ya biahsara ambayo yanauza mali zetu huku nje iwe Nyama, samaki, korosho, Khanga, vitenge, vinyago, ofisi za Utalii na hata matunda yetu kama ndizi, machungwa, embe na kadhalika.

  Majuzi tu nimetembelea duka la Wazaire hapa mjini wanauza hadi Nyama ya nyani waliokaushwa nikapigwa butaa kuyaona haya huku majuu lakini ndio wanafanya wenzetu. Sisi tunabakia majungu na kukutana siku za kifo na harusi tu vipi Wabongo?

  Sawa, sikatai umuhimu wa kurudisha mwili wa marehemu nyumbani lakini sidhani kama hii ni hoja kubwa sana inayotukwaza kama tukiweza kuzalisha fedha ktk Jumuiya zetu nadhani tunaweza kabisa ku afford expenses kama hizi. Na ndio maana ukiwauliza watu nyumbani kuhusiana na duo citizenship wanashindwa kuelewa mchango wa Diasporas ktk kuendeleza nchi yetu... mimi nadhani imefika wakati tujifunze toka kwa Diasporas wenzetu wanao ongeza pato la nchi zao kwa wao wenyewe kutumia Uraia wao kununua mali za nchi zao na kuziuza nje pasipo kusubiri wageni wafikirie wajaribu ili kutafuta soko la mali hizo..

  Mwisho, kulingana na mpango uliopo sasa hivi kwa nini hao NSSF wasifungue online banking wenyewe badala ya kupitia banks nyinginezo hali inawezekana kabisa kuhamisha fedha kwa credit cards (visa or Mastercard) ili kurahisisha kwa Watanzania wote waishio nchi za nje?

  Wakuu zangu I would love to be part ya hii DICOTA lakini kama kawaida yetu hiki ni chombo cha Marekani...Na sijui kama wizara ya mambo ya nje chini ya Mh. Membe wamefikiria kuunda chombo cha kitaifa chini ya wizara yake ambacho kiwe na vichwa kama kina Mkandara hapa! - Haaa! haaa! haaa!
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkandara,

  Samahani sikupata muda kujibu hii on time.

  Ingawa mimi si msemaji wa DICOTA au wa watanzania wote wa diaspora, jibu la swali lako ni kwamba, yaliyoongelewa ni mengi sana - ya biashara na vitu vingine. Nimesema nitaweka mengine kadri muda utakavyoruhusu.

  Kwa taarifa yako, wafanyabiashara wa kitanzania wanaoishi marekani ni wengi hata mimi nilishangazwa sana na idadi yao. Kuna bwana mmoja alipewa tuzo ya kuwa mjasiriamali bora hapa US, ana business ya usafirishaji inayoingiza zaidi ya dola milioni moja kwa mwaka.

  Kuna mengi sana watanzania wanafanya ila huwa hayasikiki.

  Mkandara,

  Ingawa hata mimi sipendi biashara ya kurudisha maiti nyumbani, siwezi pia kukana usumbufu unaopatikana kila mara tunavyohangaika kujaribu kutafuta dola alfu 15 au 20 ili kufanya hivyo. Kama NSSF wanakubali kutusaidia, am all for it

  Magori alisema kila kitu kiko mezani

  Unaweza kujiunga tu na DICOTA ... kwenye america tutaongeza s mwishoni ili isomeke americas
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kutoka kwenye same source hapo juu ...

  Hii ni jinsi issue ya ICT ilivyojadiliwa kwa ufupi

  BTW - ninajaribu kuwasiliana na jamaa wa DICOTA kuona kama nitapata habari zaidi (maana hiyo source hapo juu iliweka mambo machache tu kwenye online version ya gazeti lao.

  Dj luke ameweka picha kwenye blog yake, najaribu kuwasiliana na mwalimu AB anisadie kuziweka hapa
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwa nafsi yangu nimekuwa diaspora kwa miaka mingi sana (kumi na mbili hivi) lakini sidhani kama nimesaidia kunyanyua uchumi wa tanzania moja kwa moja.

  apart from watalii kadhaa waliokwenda tanzania kutokana na kunijua mimi, na kufunza kiswahili kwa watu wachache..........sidhani kama nimesaidia taifa kwa uwepo wangu nje (moja kwa moja)

  uwekezaji niliofanya tanzania ni wa unmovable assets kwa hiyo faida yake kwa taifa ni ndogo

  watu tulio diaspora we need more oppoturnities za kusaidia taifa nafikiri ( or maybe it is just me .........)


  tungefaidika kwa kupata namna ya utumaji pesa mwepesi zaidi kwa kuanzia
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Gaijin,

  Hii ya kutuma pesa, kama sikosei CRDB walisema wanaongea na benki za huku ili kurahisiha hii shughuli ya utumaji pesa. CRDB pia wameanza mpango unaowawezesha diaspora kufungua akaunti CRDB wakiwa nje ya nchi.
   
 7. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii inatoa kwa ufupi yaliyosemwa na Bloom + Luhanjo

   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii inatoa kwa ufupi yaliyosemwa na Bloom + Luhanjo

   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mwafrika unakumbuka tukaambiwa kuhusu tembo card ya crdb?

  hizo pesa utakazo katwa bora hata uipatie city bank na benki nyengine .............

  service za utumaji pesa kwa benki za tanzania bado zina makato makubwa mno kulingana na huduma yenyewe
   
Loading...