Diamond, Vanessa mdee, Shetta, Joh makini, Alikiba, Richi mavoko na AY

Kidingi

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
1,872
1,832
Kiukweli diamond yupo level nyingine kabisaaaaaa....

Leo unakuta diamond unamwita kwenye show mil 40 anakataa labda ujipange kuanzia mil 50/60 wakati hakuna msanii Tanzania anaelipwa hata nusu ya hiyo pesa na thamani inapanda kila anapopiga hatua na show anapata kama kawaida na ukijaribu kuangalia yupo vizuri sana ni haki yake kufanya hivyo kama wenzetu wanalipwa zaidi ya milioni 160 kwanini na sisi tusisogee huko???

Ukijaribu kuangalia upande mwingine tena dogo anapaa sana anga, alafu hata akirudi Tanzania sio wakwenda ma clubs, kufanyeje ukikutananae ni kazi labda mpo studio, au kwenye show hivii (ukitoa marafiki wa karibu wanaoweza kutembeleana) ukijumuisha na special treatments kwenye shows hivii lazimaaa baadhi ya wadau waone gere...

Ila ndio hivo yaniii dogo kashapaa anga na kizuri anachonifuraisha anajituma saana na yupo tayari mda wote...

Wimbo wa Nana kautoa mwaka huu mwezi wa tano mwishoni lakini video ilikuwa ndani tu ameshoot tokea mwaka jana alipoenda channel o music awards, lakini ilikuwepo tu... Na tayari ndani kuna nyimbo na Mafikizolo, psquare, aka na bado ambazo ameshirikishwa ambazo zinazidi kumuongezea CV na fanbase pia... Now ukicheki chart ya muziki kwenye station kubwa unamkuta diamond kwenye nyimbo mbili tofauti, na bado video ya love boat inakuja, na sahivi yupo south anafanya nyimbo aliyoshirikishwa na Daniel daaaaaaaaah

Vanessa anakuja vizuri mnooo, espect joh makini, respect shetta...... hawa watu wa kuwaangalia saana mwaka huu Vanessa amepata connection nyingi sana kimatàifa na jinsi alivyo makini na kazi yake lazima azidi kutoboa.. Shetta naona akiendelea kuimba itakuwa poa saana ana staili fulani hivii tofauti ambayo kwa flavour iliyopo hata kama hujui anaimba nini utataka kusikiliza.. Joh makini daaah saafi naona akazie saana alipoanzia, najuws ikija kutoka kolable yake na aka atakuwa hashikiki..

Richi mavoko na Alikiba wapo vizuri sana ila tu kuna vitu havijakaa sawa endapo vikikaa sawa tutakuwa tunaongelea balaa lingine nadhani Nigeria wataanza kutuheshimu kikamili

Rich mavoko anazingua sijui tatizo ni nin yanii, alikiba nae sio mbaya saana support kubwa na pressure anayopata kwa mashabiki inampigisha hatua.. hawa wawili waongeze tu userious na kuangalia suala la management sababu kipaji hakijipiganii chenyewe sokoni, na kuna msemo wa kibiashara ""bidhaa hainunuliwi sokoni bali inauzwa"" hapo tu yanii

Mwisho kwa Baba lao Ambwene yesaya namuheshimu sana huyu mtu ametuletea makubwa sana na kizuri zaidi ana moyo sana wa kusaidia yeyote anapohitaji msaada kwakwe... Kwa miezi kadhaa naona ametulia kidogo, na kwa upande wangu alitakiwa kutoa video ya zigo kipindi ametoa wimbo, na huu wimbo aliutunga kiukweli alipatia kila kona na napenda aendelee na staili hii ya uimbaji....

Kuna wasanii wengi, lakini mziki waleo si tanzania pekee (ni sawa na msanii wa tz awike dodoma pekee afu aridhike haifai) so nimegusia ninaoamini mimi wanajitahidi kutuwakilisha kimataifa
 
Milioni 60, Tale, Fela, SK, Iyobo, Rommy, madensa nane ukigawanya inakuwa kama sawa na mzigo anaokula mzee Yusuph jumapili pale travertine.
Na ndio maana anazidi kuwa juu kila siku hao ndio wanaomfanya abaki juu peke yake asingeweza.

Hongera zake kwa kufanya kazi ki-timu.
 
Milioni 60, Tale, Fela, SK, Iyobo, Rommy, madensa nane ukigawanya inakuwa kama sawa na mzigo anaokula mzee Yusuph jumapili pale travertine.

Hahahahaaa mkuu kuna watu hawalijui hilo...basi tu ushabiki umewajaa hata kujua hawataki.
 
Milioni 60, Tale, Fela, SK, Iyobo, Rommy, madensa nane ukigawanya inakuwa kama sawa na mzigo anaokula mzee Yusuph jumapili pale travertine.

Mwisho wa malipo anajuwa yeye wanavyogawanya kwa kila aliyemuajili, cha muhimu ni kwamba kupitia mdomo wake ameweza kufanya kitu kikubwa kama hicho...

Na upande wa faida ipo tu kwa gharama ya video anazo shoot kujiendeleza, Maisha yake yalivyosogea si haba
 
Donald collaborate with Our own Diamond nw in SA.. huyu jamaa namkubali sana kuna nyimbo yke 1 inaitwa Over the moon anaimba RnB tamu sana.
 
Attachments

  • 1434560569033.jpg
    1434560569033.jpg
    101.9 KB · Views: 696
donald is the best kwa muzk wa taratbu hope diamond atazdsha iwe bomb hyo ngoma
back kwa mtoa mada nimekuelewa sana ila kuna mtu hafai kuwa hapo 😁😁😁😁
 
Donald collaborate with Our own Diamond nw in SA.. huyu jamaa namkubali sana kuna nyimbo yke 1 inaitwa Over the moon anaimba RnB tamu sana.

Nooma saana... inatakiwa wasanii wetu wajifunze kwake collable ni kitu cha muhimu saana inaongeza saana fan base na ni kiashiria tosha kwamba upo vizuri na utampaisha kwa collable hiyo....

Hapo bado hajakutana na wakina uhuru waingie studio tena...
 
Mzee yusuph yupi? Huyu wa taarab?

Kama ndiye, ivi unajua team yake, au umeamua tu kujamba ili tukuone.!?

Wewe ndio una timu mimi nalipia muziki ninaosikiliza. Hayo mambo yenu mnaolipiwa viingilio kwenye fiesta au mnatafuta tag instagram.
 
Milioni 60, Tale, Fela, SK, Iyobo, Rommy, madensa nane ukigawanya inakuwa kama sawa na mzigo anaokula mzee Yusuph jumapili pale travertine.

Na kama hufahamu madancer wake wawili wana nyumba tayari....

ukitaka kufanikiwa wafanikishe na wenzako...

Yamoto band leo wanaingia tz kutoka south africa ambapo wameshoot video na godfather kwa gharama ya diamond.. yote hayo hayaji hivihivi ni mkwanja huo na usiniambie ni kitu kidogo sababu wasanii wengi wangekuwa wanaubavu huo
 
afadhal umewaeleweshaaa wagumu kuelewaa
 
Vanessa mdee mwenyewe alipotoa video yake ya nobody but me aliulizwa kwa nini alitoa kwa justin campos na si kwa godfather kama wenzake akajibu kwa sababu mbili hakuwa na bajeti inayolingana na godfather na pili kufahamiana nae...

Maharage sio nyama ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom