Diamond Platnumz afunguka kuhusu tuzo za Killi Music Awards

Diamond Platnumz afunguka kuhusu tuzo za Killi Music Awards

Kasoma alama za nyakati hana lolote, kiba anakupiga bao mwaka huu, unaanza kujitetea mapema, mashabiki ndo wamepropose majina, ulitaka kili wachomeke tu? Hahhaha nilisema.mashauzi yake yatamshusha ona sasa, we endelea imba taarab tu, wakuweke kipengele kimoja na mzee yusuph, mwaka huu kili utagawana tuzo na kiba na huko kwenye mataifa usidhan utapata kwa kuimba twaarab. BADILIKA
 
Unapofanya kazi kubali kupokea hasi pia sijaona hilo tatizo la kili kutowapa vipengele vingi ya moto band kwani Tanzania kuna wasanii wangapi hawajawahi kupata mfano Blue, Dully (ukichanganya na muda wa kwenye game waliopo), Belle 9 lakini sijawahi sikia wakilalamika zaidi ya dully kutangaza hataki kushiriki. Hivyo kama diamond anaona hakutendewa haki achukue uamuzi wa kujiengua au kutoshiriki kabisa siyo kutafuta huruma ya watu
 
Wasalaam WanaJamvi,

Nimeyaandika haya baada ya kuona post ya Diamond akikosoa vikali tunzo za Killi hadi amepitiliza na kuandika yasiyotarajiwa. Pengine alikuwa na hasira sana lakini tusisahau kuwa hasira haijengi! Kwangu mimi naona amekosea sana!

Hakuna busara iliyokuu kama kukaa kimya! Hapa ndio naamini wasanii wanahitaji washauri wa karibu kabla ya kuandika au kusema chochote!

Diamond umekosea sana tena sana. Ulikuwa na nafasi ya kukaa kimya kuonesha busara kuu! Kuna mtu alisema ukitaka kutambua mtu mwenye busara subiri akiwa na furaha sana au akiwa na hasira sana!

Naamini Diamond hukufikiri mara mbili kabla ya kupost uliyoyapost! Kila mtu anajua wazi kuwa hizi tunzo hazijakamilika na haziwezi kukamilika kamwe na hata kama kuna mtu atapewa kuziendesha kamwe haziwezi kuwa satisfy watu wote na wakati wote!

Pengine ni kweli anayojaribu kutuambia Diamond lakini ninachojiuliza hii ndio busara yako ya mwisho?

Kila mdau wa muziki anajua fika kuwa hakuna mwaka ambao umekuwa na hit song nyingi kama mwaka jana na mimi nilijua utaleta malalamiko mengi sana lakini niliamini kuwa busara ndio itatumika zaidi kuliko hasira au maneno ya kuwavunja moyo waandaaji waonekane hawajafanya lolote kwa kuwa tuliowategemea hawapo!

Diamond unasahau kuwa wakati unapewa tunzo wewe kuna watu walilalamika kuwa umependelewa na wengine wakajitoa na wengine wakatumia busara na kukaa kimya!

Jamani kama maneno ya namna hii yangekuwa yanaandikwa basi yangetoka kwa Belle 9 ambaye watu walikuwa wanaamini kuwa anastahili tunzo kila leo.. Lakini kijana wa watu amekuwa ni mwenye hekima sana na ninampongeza kwa hilo!

Diamond kusema kuwa hata usipopewa tunzo huwezi kushuka ni kuwakosea heshima Kill na BASATA kwani hizi ni tuhuma zisizo na msingi kutoka kwa msanii mkubwa kama wewe. Ni kweli wana lengo la kukushusha?

Diamond umekosa busara kabisa kabisa ulipaswa kukaa kimya maana ni wachache wataamini unawatetea hao uliowataja!

Diamond jifunze kuvumilia na si kila kitu cha kukifanya public.. Diamond ina maana kusema kwako hukuhangaika kuwambia watu jinsi ya kupiga kura maana hukupendezwa, ina maana umegomea tunzo? Ni kweli Kill na Basata wamekuwa wabaya kiasi hiki hadi unadiriki kuuliza kama wanaua au kukuza muziki?

Diamond umenishangaza sana tena sana lakini nakukumbusha ujifunze kuweka akiba ya maneno na ndio busara iliyo kuu kuliko kuongea!

Diamond umeshindwa kujiuliza kwanini wengine wamenyamaza?

Mimi naamini hizi tunzo ni nzuri na ni msaada kwa wasanii, pia si tunzo zilizokamilika na hakuna tunzo zilizokamilika duniani!

Uzuri wasanii huwa mnapewa semina kwa hiyo mnaweza kusema huko huko malalamiko yenu lakini kuongea kwenye media tena kwa njia uliyotumia itachukuliwa ni kutaka watu wagomee tunzo hizi!

Wasanii ni vyema mkawa mnaweka akiba ya maneno ili msiwakatishe tamaa waliojitoa kuikwamua tasnia hii kwani nao hawajakamilika!

Karibuni wana jamvi!
 
Teña hakua na sababu ya kubwabwaja hayo yote Leo Hi, Kama Nakumbuka Ktma walipata kuita wasanii wote kwaajili ya mazungumzo nini kifanyike kwa tuzo za 2014-2015, waliotokea ni wasanii watatu Wa bongo flavaour Kama sikosei ambae alikua ni gnako, Joh makin na Msichana mmoja sikumbuki alikua nani, wwngine wote wakala kona tena kwa kijifanya wako busy, Leo Hi majina yametoka anajifanyaa kujikwezaa, atuliee anyolewee, halafuu Ile kauli yake ya pale Mwisho Eti haeezii kushuka Labda wamuue

Kashuka gwiji Wa muzik Rkelly sembusee yeyee Atulizee Mshonooo 😂😂😂😂😂😂
 
11252675_637602313040236_1373619220_n.jpg

​
 
Unapofanya kazi kubali kupokea hasi pia sijaona hilo tatizo la kili kutowapa vipengele vingi ya moto band kwani Tanzania kuna wasanii wangapi hawajawahi kupata mfano Blue, Dully (ukichanganya na muda wa kwenye game waliopo), Belle 9 lakini sijawahi sikia wakilalamika zaidi ya dully kutangaza hataki kushiriki. Hivyo kama diamond anaona hakutendewa haki achukue uamuzi wa kujiengua au kutoshiriki kabisa siyo kutafuta huruma ya watu

We jamaa em nioneshe ni wapi mondi alipotangaza kutafuta huruma...em punguza ushabik maandazi
 
He has a varied argument, although kweli Ile post yake inamapungufu, anyway acha niishie apa for now

Mapungufu aliyo yaonesha ndio yamenifanya nimshauri ajifunze kuweka akiba ya maneno! Muda mwingine kukaa kimya ni bora kuliko kuongea! Hakuna mwaka ambapo hizi tunzo hazijawai kulalamikiwa..lakini Diamond kujiuliza kama hizi tunzo zina kuza au kuua muziki ni kupitiliza...isitoshe kusema hawezi kushushwa as if kuna mtu amepanga kumshusha ni kupitiliza kabisa..
 
Halaf wasanii wa bongo bwana, hvi hakuliona hlo yy ule mwaka aliopendelewa akapewa matuzo kibao, na kuwekwa kweny category kibao, hakuona kama kuna upendeleo ila Leo kapendelewa mwengine ndio anaongea, atutolee upuuzi wake huo
 
Nadhani kusema kushushwa ni kutokana na maneno ambayo wengi wamemwandikia na kumtag kwa sana insta kuwa atashuka.

Mie nilipoona Haombi kura nimekuwa nikifiri ni kwa sababu anataka aachie wengine wachukue.

Ila lazima kuna ya nyuma ya pazia yaliyomfanya aandike hayo...hatuyajui sasa ila tutakuja kuyajua baadae.

Amesha anza kujipanga maisha na biashara so yeye kuandika hivyo lazima anajua watu watakasirika....tumwache amwage part 2

Kuna kilichotokea hatukijui sio kawaida yake ni mvumilivu.
 
Ila kuna wakati unafika wakiowika lazima wapewe nafasi kugombania...wengi humu mlisemaga mmeshangaa kuona Yamoto Band imefanyiwa hivyo

Tumwache aseme kuna ya nyuma ya pazia hatuyajui na lazima anajua hamtampigia kura baada ya kuandika haya.
 
Kimekucha hata msio mpenda Diamond leo mnamuongelea ki positive, ki negative lakini bado anachukua kiki kumekuchaaaaaa
 
Bora umemwambia ukweli kwa sababu utamweka huru kuliko kusifia hata pale anapokua wrong. Kiukweli mwenyewe naona either kapitiwa au yuko stressed na hana tumaini na tuzo hizo, lakini last year alipokea tuzo nyingi Mpaka watu waka complain. Mapungufu kwenye kitu chochote huwa yanatokea kitu hakiwezi kuwa perfect hundred percent. Kilichonishangaza zaidi kauli yake eti ya kushushwa kwahyo yeye ndo anajiona best kwa kila kitu na Ku deserve wengine hawafai? Eti kushushwa kiukweli awe makini na kauli zake tata yee anafikiri ni nani Mpaka ashushwe labda?
Hawa wasanii kukosa washauri makini wa kuwaelekeza kwahyo asipowekwa au hata kupata tuzo anaona watu wanataka kumshusha wonders shall never end indeed.
 
afadhari aisee tena ungewaachia kabisa tuzo zao maana ulizochukua zinatosha waachie wasanii local km kina Kiba wanyang'anyane wewe sasa hivi focus kwenye mituzo ya kimataifa km vile BET, MTV nk

Maneno ya kikunguru haya hahha anaogopa nini kila mwaka wasanii huwa wanaachwa mbona huwa anazizoa hahahahahah hatareeeee
 
[h=1]Peter Okoye: My African people, you asked for it and it's coming to you soon..[/h]
attachment.php
 
Back
Top Bottom