Diamond na Wasafi Media ni wanyonyaji sana

chipa GM

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
1,769
2,858
Jonijo kaondoka nilijua lazima aondoke siku 1.

Pale Wasafi unachukua mshahara na huruhusiwi kuwa na YouTube channel, Jonijo alikuwa ana YouTube channel, sasa ameingia WASAFI akajua labda ataendeleza harakati zake akakutana don'ts nyingi ambazo hazipo kwenye Mkataba,. Times FM alipokuwepo Jonijo na Lil Ommy unaweza kuanzisha YouTube channel. Pale Mishahara midogo, wanapewa mishahara mikubwa ni wachache sana wengine wote uzushi tu, kajamaa kanajifanya kanasaidia jamii wakati hakalipi watumishi wake. Angalia hata wakina Iyobo ni maskini sana, kwa kazi wanazofanya bado wanalipwa laki 5 wengine 4.

Harmonize aliondoka kwa upuuzi kam huu, Msanii anapiga show analipwa asimilia 40 ya show, kwa kigezo eti tulikutoa. Mapato ya You tube unapewa 40 percent. Harmonize youtube yake tu aliingiza zaidi ya Millioni 900 za kitanzania lakini hata millioni 100 hakulamba kwenye YouTube, ukibsha naweka ushaidi.

Kituko kingine Rayvanny alitangaza anaenda nyumbani kwao mbeya kupiga show kwa kiingilio cha elfu 5..Diamond akatangaza Mbeya kiingilio bure..Unaambiwa gharama zote za Mbeya kuanzia uwanja..wasanii kuwalipia kila kitu amekatwa Rayvanny zaidi ya millioni 150. Yaani nitangaze show ya kiingilio uje useme ni bure then gharama zote akalipa Rayvanny.

Usione wasanii wa Wasafi wapo hivyo, hawana hela. Hivi unajua kwenye views millioni 1 za YouTube unapata km millioni
4.5 had -7.Diamond umelalamika sana Ruge anakuonea mbona wewe hupigi nyimbo za Harmonize. Unasema Harmonize hapeleki nyimbo kwenu, vipi hao wakina Burna Boy wanapeleka nyimbo Wasafi?

Reactions from comments

1. Mashbaiki wengi wa diamond ni mashabiki maandazi yaani hamtaki jamaa yenu akosolewe, ushamba tu mmezidisha
2. naona watu wengi hamjui mapato ya youtube ya you tube yanavyopatikana, harmonize kafifkisha views zaidi ya millionn300..gawanya views kwa 1000 then zidisha na dollar 2 (4400) au 3 (6600) ni zaidi ya billioni 1. Poleni sana.
hivi mnajua Millard anaingiza zaidi ya billioni 3 kwa kwa mwaka kwa youtube tu.
 
MIMI NA BISHA NA SUBIRIA USHAHIDI.

"Msanii anapiga show analipwa asimilia 40 ya show, kwa kigezo eti tulikutoa. Mapato ya YouTube unapewa 40 percent. Harmonize YouTube yake tu aliingiza zaidi ya Millioni 900 za kitanzania lakini hata millioni 100 hakulamba kwenye YouTube, Ukibsha naweka ushaidi."
 
ona views wa harmonize mpaka leo. Sasa gawanya kwa 1000 then zidisha mara elfu 4600 utajua harmonize anaingiza sh ngapi
View attachment 1435027
USHAHIDI AMEPEWA 40% SI UONI NA USUBIRIA HAPA.

USHAHIDI WA GHARAMA ZOTE KULIPA RAYVANNY SI UONI.

USHAHIDI WA RAYVANNY KUKATWA ZAIDI YA MIL 150 SI UONI.

USHAIDI IYOBO ANALIPWA LAKI 4/5 SI UONI.

Alafu kwa mujibu wa AT wakati akihojiwa na Millard Ayo alisema kwa wastani views milion 1 wa YouTube sawa na $600.

Ukipiga mahesabu 371.8 x600=223,080 kwa hela yaki bongo around milion 490-500.
 
Sina ushahidi ila Harmonize angekuwa ananyonywa sidhani kama angeweza kulipa milioni 500 za kuvunja mkataba. Kumbukeni hiyo ni biashara sio huduma yaani hata kama anakutoa lakini pia ni vizuri kuweka mkataba ambao utampendelea anaewekeza ela, hivi unajisikiaje umewekeza ela yako alafu mtu anaondoka kiurahisi rahisi na baada ya mwezi unamkuta yupo chini ya management nyingine ambayo inakuwa haijagharamia kabisa.

Kwa Harmonize nadhani mnatakiwa mtoe pongezi kwa domo kwa kulea kipaji ambacho sasa hivi kinatisha, mambo ya youtube sijui nini achana nayo huo ni mkataba waliingia of course domo aliwekeza (kwanini usitoe hesabu zilizotumika kweye fedha zilizotumika kwenye maandalizi ya nyimbo za Harmo akiwa wasafi badala yake unakuja kulalamika kwenye fedha za mavuno (output) wakati zilizowekezwa (inputs) huzungumzi
 
USHAHIDI AMEPEWA 40% SI UONI NA USUBIRIA HAPA.

USHAHIDI WA GHARAMA ZOTE KULIPA RAYVANNY SI UONI.

USHAHIDI WA RAYVANNY KUKATWA ZAIDI YA MIL 150 SI UONI.

USHAIDI IYOBO ANALIPWA LAKI 4/5 SI UONI.

Alafu kwa mujibu wa AT wakati akihojiwa na Millard Ayo alisema kwa wastani views milion 1 wa YouTube sawa na $600.

Ukipiga mahesabu 371.8 x600=223,080 kwa hela yaki bongo around milion 490-500.
Mahesabu ya pesa apatayo youtuber haibase kwenye viewers tu, inahusisha muda aliotumia mtazamaji kuitizima video yako, watizamaji wako eneo gani/nchi zipi nk. hivyo mnaweza kuwa na viewers 1m ila pesa zikatofautiana pakubwa sana
 
Siku nyingine:-

Unatakiwa useme hivi:-
1. Wasafi wanawapa 40% wasanii wao Alikiba anawapa 100%
2. Wasanii wa Wasafi wana maisha magumu - wasanii wengine wote wana maisha mazuri kwa mifano.
3. Watangazaji wa wasafi wanalipwa 200k - media zingine zote 2m kwa mifano ukiweza na salary slips zao.
4. Utaje na wanamuziki wengine Tanzania walioweza kuajiri dancers na anawalipa in monthly basis na tena ukiweza utuonyeshe kiwango cha cha utajiri wao hao dancers.

Ukishindwa watu watakuona una njaa tu nafikiri uko katika promotion ya kutangaza kachannel kako ka YouTube ndio unataka beef mseleleko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahesabu ya pesa apatayo youtuber haibase kwenye viewers tu, inahusisha muda aliotumia mtazamaji kuitizima video yako, watizamaji wako eneo gani/nchi zipi nk. hivyo mnaweza kuwa na viewers 1m ila pesa zikatofautiana pakubwa sana
Hilo nalijua ila nimerefer kwa AT,ila hata kama kutakuwa na utofauti basi itakuwa ndogo sana.
 
Hiyo mikataba wanapewa na kukubaliana nayo kabla ama? maana kama mtu ulisoma ukaelewa na ukakubaliana na mkataba husika kwa nn ulalamike? Mleta mada nawewe pia unashindwa kuwa na fikra pevu. Maana ww unafikiri mtu kama zuchu angeweza kufikisha viewers kwa single video 1m, ama angeweza kutoa video zenye ubora ule… kampuni inagharamia mambo mengi sana. Msipotoshe watu kwa mambo ya kizushi.. Mtu kama harmonize unafikiri jina lake lingekuwa liko juu hivyo.. Nitajie msanii mmoja tu aliye nje ya wasafi ama chini ya management yoyote nyingine anayefanya vizuri Zaidi ya watu kama akina Mboso, Rayvanny, ama hata lavalava.
 
Mahesabu ya pesa apatayo youtuber haibase kwenye viewers tu, inahusisha muda aliotumia mtazamaji kuitizima video yako, watizamaji wako eneo gani/nchi zipi nk. hivyo mnaweza kuwa na viewers 1m ila pesa zikatofautiana pakubwa sana
So unaamini Harmonize kaingiza kiasi hicho cha Pesa 900 million kwa views tu?

Mbona maisha yasingekuwa magumu kabisa duniani 😛😛
 
USHAHIDI AMEPEWA 40% SI UONI NA USUBIRIA HAPA.

USHAHIDI WA GHARAMA ZOTE KULIPA RAYVANNY SI UONI.

USHAHIDI WA RAYVANNY KUKATWA ZAIDI YA MIL 150 SI UONI.

USHAIDI IYOBO ANALIPWA LAKI 4/5 SI UONI.

Alafu kwa mujibu wa AT wakati akihojiwa na Millard Ayo alisema kwa wastani views milion 1 wa YouTube sawa na $600.

Ukipiga mahesabu 371.8 x600=223,080 kwa hela yaki bongo around milion 490-500.
Hata hiyo dollar 600 huenda hawaipati ikawa chini ya hapo.
Watu wanaongea ongea tu unafikiri kina Maxence hawa hawana shida na pesa huko YouTube kungekuwa kunalipa kiasi hicho tunachodhanishwa wangejikita huko vibaya sana.
 
So unaamini Harmonize kaingiza kiasi hicho cha Pesa 900 million kwa views tu?

Mbona maisha yasingekuwa magumu kabisa duniani 😛😛
Wapi nimeongelea pesa m900!!! Nimegusia namna youtuber yoyote yule mahesabu ya pesa zake zinapigwa main point ilikuwa kuna vigezo zaidi ya no of viewers.. Sizungumzii pesa ya mtu
 
Back
Top Bottom