Diamond apewa cheti Cha appreciation Baada ya kujaza ukumbi London

Diamond apewa cheti Cha appreciation Baada ya kujaza ukumbi London

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
22,854
Reaction score
32,657
Nyota wa Bongo Fleva, diamondplatnumz , ametunukiwa Cheti Maalum cha Heshima baada ya kufanikisha kuuza tiketi zote na kujaza ukumbi maarufu wa Royal Albert Hall jijini London, Uingereza.

1749972791748.png
Huu ni utaratibu wa heshima unaotolewa na baadhi ya kumbi kubwa duniani kwa wasanii wanaofanikiwa kufanya onesho lililojaza ukumbi kwa asilimia 100.

Diamond Platnumz ameandika historia kwa kuwa mmoja wa wasanii wachache kutoka Afrika Mashariki waliowahi kutumbuiza katika ukumbi huo mkubwa na wa kihistoria uliojengwa tangu mwaka 1871. Onyesho lake lilihudhuriwa na maelfu ya mashabiki kutoka pembe mbalimbali za dunia.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Walioujaza uwanja ni wazungu wenyewe au ni diamond? Au uwanja ulijazwa na wabongo walioongozana na diamond kutoka tz?
Alafu hiyo show ilikuwa ya Wanaijeria mkuu huyo kadandia tu. Show ilijaa wazigua na wahehe tu hakuna mzungu atakayeenda kumuangalia huyo akiimba nyimbo zake za kigogo na kinyakyusa labda walienda kumdhihaki.
 
Kwa hapa sasa wale wanaosema Diamond anakwenda Ulaya kujqza vibaa vya mtaani atakuwa kawajibu.

Wiki ya jana nilikiwa nawasikiliza wanaharakati wa Tanzania wanapanga kususia concerts za Diamond kwa sababu anam support Samia na CCM.

Naona wameshindwa kazi ya kufanya concert ya Diamond isifane.
 
Nyota wa Bongo Fleva, diamondplatnumz , ametunukiwa Cheti Maalum cha Heshima baada ya kufanikisha kuuza tiketi zote na kujaza ukumbi maarufu wa Royal Albert Hall jijini London, Uingereza.

Huu ni utaratibu wa heshima unaotolewa na baadhi ya kumbi kubwa duniani kwa wasanii wanaofanikiwa kufanya onesho lililojaza ukumbi kwa asilimia 100.

diamondplatnumz Ameandika historia kwa kuwa mmoja wa wasanii wachache kutoka Afrika Mashariki waliowahi kutumbuiza katika ukumbi huo mkubwa na wa kihistoria uliojengwa tangu mwaka 1871. Onyesho lake lilihudhuriwa na maelfu ya mashabiki kutoka pembe mbalimbali za dunia.

| @errymars_

#ManaraTV
#ManaraTVUpdates

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Watanzania acheni ujinga wa kujitakia....ile shoo ya jana pale London ilikuwa ni ya Wanigeria na Diamond alipiga kama msindikizaji tu na ndiyo maana alianza mwanzoni kama trela na wenyewe Wanigeria wakamalizia shoo, wengi waliojaa pale walikuwa wenyewe wanigeria.....mnadanganya wenzenu ili iweje?
 
Welcome to the new era of secret society mr platnums sisi yetu macho tu.
 
Back
Top Bottom