KIIZA KATABANI
New Member
- Jun 27, 2017
- 1
- 0
DHANA YA VITI MAALUM NA NAFASI YA KWELI YA MWANAMKE KWENYE SIASA
Wakati huu ambapo TANZANIA inajivunia kuwa na viongozi wa ngazi ya juu kabisa ambao ni wanawake – Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson – tunapaswa kujiuliza kwa dhati: je, bado kuna ulazima wa kuendeleza mfumo wa viti maalum kwa wanawake kwenye udiwani na ubunge?
Kwangu mimi, huu mfumo unaonekana kufifisha na kudharau uwezo wa kweli wa mwanamke kisiasa. Mwanamke wa leo si dhaifu – anaweza kushindana majimboni na wanaume kwa hoja, sera, na nguvu ya kisiasa. Tuna mifano hai ya wanawake waliopita majimboni bila utegemezi wa viti maalum, na wamefanya kazi kubwa.
Ni kweli kwamba mfumo wa viti maalum ulianzishwa kwa nia njema – kuongeza uwakilishi wa wanawake. Lakini kwa sasa, baadhi ya watetezi wa haki za wanawake wamegeuka kuwa wanufaika wa mfumo huu, badala ya kuutathmini kwa uhalisia na matokeo. Kwa mantiki hiyo, mjadala huu huogopwa, kwa kuwa maslahi binafsi yameingizwa.
Najiuliza: Je, viti maalum bado vinahitajika kama wanawake wana uwezo wa kweli wa kupambana kisiasa?
Au tumevigeuza kuwa sehemu ya "kuwapa nafasi wasiojiamini" badala ya kuwaandaa kwa ushindani wa kweli?
👉🏽 Badala ya kuendelea kuviita "viti maalum vya wanawake", kwanini nafasi hizi zisipewe makundi mengine yasiyowakilishwa vyema, kama vile:
Wawakilishi wa walimu
Wawakilishi wa madaktari
Wawakilishi kutoka jeshini na vyombo vya ulinzi
Vijana waliopitia mfumo wa vyuo vya ufundi au wenye ujuzi wa kazi
Haya yangekuwa ni "majimbo tembe" ya kitaaluma – yenye kuleta utaalam na ushawishi wa kweli kwenye mchakato wa maamuzi.
📉 Tukitathmini kwa uhalisia mchango wa viti maalum kwa maendeleo ya wanawake kisiasa, tunaona bado haujaleta mageuzi makubwa. Wengi wamekuwa “opportunists” – wanatumia nafasi hizo kama njia ya mkato kupata madaraka, si kama jukwaa la kutetea haki za mwanamke au kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii.
Hitimisho
Hatupingi nafasi za wanawake, tunapinga mfumo wa kuwaonea huruma badala ya kuwaamini. Mwanamke wa leo anaweza – na anastahili nafasi kupitia ushindani, si huruma ya mfumo.