Dhana ya polisi kuwa wakusanya mapato

Nairobian

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
873
2,281
Hili swala linazidi kuwa nzito kila siku. Polisi badala ya kufanya kazi za kulinda Amani, unawakuta wamejimwaga kwenye barabara yetu na EFD machine wanakuja wanakusanya mapato na sehemu zingine wanalazimisha makosa pasipokuwa na Kosa.

Hii picha ni ya mida hii, ambapo wanasimamisha magari kupita maelezo. Nadhani hii Itafika sehemu wananchi watch watachoka huu uonevu.
20170402_130502.jpg
 
Hili swala linazidi kuwa nzito kila siku. Polisi badala ya kufanya kazi za kulinda Amani, unawakuta wamejimwaga kwenye Mabaya mabarabara yetu na EFD machine wanakuja wanakusanya mapato na sehemu zingine wanalazimisha makosa pasipokuwa na Kosa. Hii picha ni ya mida hii, ambapo wanasimamisha magari kupita maelezo. Nadhani hii Itafika sehemu wananchi watch watachoka huu uonevu.
View attachment 490234
Hebu mwangalie huyo bodaboda aliposimama je ni sahihi?
Akilipishwa faini je?
Hebu tujifunze kutii sheria jamani badala ya kupotosha mambo
Kama sheria hizi hazitekelezeki basi zifanyiziwe amendment au zifutwe tuishi kwenye nchi isiyokuwa na sheria
 
Hili swala linazidi kuwa nzito kila siku. Polisi badala ya kufanya kazi za kulinda Amani, unawakuta wamejimwaga kwenye Mabaya mabarabara yetu na EFD machine wanakuja wanakusanya mapato na sehemu zingine wanalazimisha makosa pasipokuwa na Kosa. Hii picha ni ya mida hii, ambapo wanasimamisha magari kupita maelezo. Nadhani hii Itafika sehemu wananchi watch watachoka huu uonevu.
View attachment 490234
Kwhio wanasimamisha magari yote yanayopita na kukusanya mapato?!
 
Kwa iyo polisi ni taasis ya kibiashara sio mkuu? Naona na wew n polisi hao hao wabaya wetu.
 
Polisi hawakusanyi mapato wao wanaandika faini sasa wewe kama unageuza faini kuwa mapato Haya ila cha maana ni kutii sheria na takwimu inayoonesha faini imepunguza kiwango kikubwa cha ajali watu au madereva wamepunguza uwaruwaru kwa kuhofia Faini
 
Nchi hii imekuwa kero hasa awamu hii ya 5 ,serikali imeshindwa kubuni na kutumia fursa tulizonazo ili kuinua uchumi wetu matokeo yake ndo haya
 
Polisi hawakusanyi mapato wao wanaandika faini sasa wewe kama unageuza faini kuwa mapato Haya ila cha maana ni kutii sheria na takwimu inayoonesha faini imepunguza kiwango kikubwa cha ajali watu au madereva wamepunguza uwaruwaru kwa kuhofia Faini
Wakati mwingine faini zimesaidia sana. Kupunguza wasiojua sheria, wenye haraka na wenye migari mibovu kujiondoa wenyewe barabarani
Ilikuwa kero sana, unaendesha anatokea mtu ana overtake pasipo ruhusiwa yaani ilikuwa shida tupu barabarani, sasa ivi barabarani bila kuwa na pesa ya ziada, Barabara utaisikia tuuu. Lengo sio kukomoana swala ni kufata sheria tuuu. Maana Enzi zile mtu anaendesha Gari, Mara mafuta yamekwisha analeta foleni, sasa ivi avipo tena ivyo vimbwanga
 
Hili swala linazidi kuwa nzito kila siku. Polisi badala ya kufanya kazi za kulinda Amani, unawakuta wamejimwaga kwenye Mabaya mabarabara yetu na EFD machine wanakuja wanakusanya mapato na sehemu zingine wanalazimisha makosa pasipokuwa na Kosa. Hii picha ni ya mida hii, ambapo wanasimamisha magari kupita maelezo. Nadhani hii Itafika sehemu wananchi watch watachoka huu uonevu.
View attachment 490234
Si kuna mtu alisema fedha hizo zinasaidia kupata kiwi ya kung'arisha viatu?
 
Ni muhimu kuangalia mambo kwa mtazamo mpana na kuyapa uzito unaostahili. Muda unaopotea barabarani kwa sababu za uwepo wa askari wengi wanaosimamisha magari kwa ukaguzi na kukusanya mapato madogo madogo waweza kuwa na athari katika uchumi kwa ujumla.
Kudhibiti mwendo maeneo mengi kwenye barabara kuu kwa kutumia speed radar zisizo na usahihi, matuta na askari wanaofanya kazi kwa kukariri ni tatizo ambalo athari zake hazionekani kwa muda mfupi.
Yapasa kufanya ulinganifu katika kudhibiti jambo kwa kuwa kuna faida na hasara zake.
 
Back
Top Bottom