Okay,mimi ni mlengwa ktk topic hii,mchumba wangu kanizidi miezi mi3;Labda nikusaidie kutokana na kiwango kidogo cha uelewa wangu mkuu,wanawake wana CHANCE kubwa ya kuzeeka(au kuzeeshwa) mapema kwasababu wanapitia nyakati ngumu sana hasa ile ya Kujifungua..kama utampachika mimba mkeo kila baada ya mwaka unategemea nini?! alafu unakuta mnawatoto 6 au 7..lazma azeeke mapema! lakini pia ugumu wa maisha huchangia! mwanamke anaweza kuwa na mtoto 1 tu lakini kutokana na ugumu wa maisha,hasa wale wanaolea bila msaada toka kwa mumewe.Afrika,ktk jamii nyingi wanawake(hata wakiwa wadogo) wamekuwa wakichukuliwa kama Chombo cha kazi!!! kuanzia kijijini na hata mjini! in that case,majukumu mengi huwakomalisha na kuwadhohofisha mapema,hatimae kuonekana wame "kula chumvi nyingi"..
Mwanamke anahitaji kupendwa,kulindwa,kuheshimiwa n.k (lakini na yeye ajipende,ajitunze na kujiheshimu zaidi) ukimpa vitu kama hivyo,utanipa results.
mfano mzuri;Angelina jolie,Beyonce,my mother! utadhani hawazeeki...!