Dhana pana ya umasikini katika Jamii yetu

Libya

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
783
1,918
Copy and paste

Kama utakumbuka maneno ya baba wa taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, kuwa miongoni mwa maadui wa kuwapiga vita usiku na mchana na kuhakikisha wametokomea basi UMASIKINI ni nambari one.

Sababu umasikini ukitapakaa kwenye jamii utatengeneza njia kwa mambo mengi sana mbaya kuingia, mfano tamaa, njaa, maradhi, uhasama, chuki, usaliti, rushwa, na kadhalika.

Hili la watoto wa kike kupenda sana pesa lina uhusiano na insecurities zitokanazo na umasikini wa hali na akili huko walipotoka yaani makwao na familia zao.

Binti aliyelelewa kwa maadili ya utu hawezi kuwa na tamaa za mali au pesa ya mwanaume ambaye si mume wake. Mabinti wa sasa wanatoka familia zenye mentality za kimasikini sana yaani baba na mama wanataka kupata maisha kupitia mtoto wao, haijalishi anatoa wapi.

Kuna vitu vingi vinawaponza watoto wa kike, mfano, kutaka kuonekana mrembo kwa mavazi ya kisasa, kumiliki simu za bei, kuhang maeneo ya bata ya gharama ili kuweza kupiga picha za kupost kwenye social networks na social media. Pesa za kumudu haya yote unadhani wanatoa wapi na wanatoka familia za kipato cha chini kabisa.

Lakini mbaya zaidi ni pressure ya familia wanazotoka hawa mabinti kuwaambia kuwa mwanaume ambaye hana pesa hana cha kukupa katika maisha, nyuma ya pazia, ni hii familia ya binti kutafuta mfadhili kupitia binti yao awatatulie matatizo yao ya ndani ya kifamilia.

Tukirejea miaka ya nyuma kidogo, si kwamba watu walikuwa na pesa sana, lahasha, bali utu ulishika nafasi yake na umasikini haukuwa na nafasi katika jamii.

Kukosa pesa sio umasikini bali ni hali ya kiuchumi ya kutokuwa na kipato. Ila umasikini ni tamaa ya kutaka kuwa na miliki isiyo stahiki yako ukilinganisha na jitihada zako wewe binafsi. Na ndio maana hata watu wezi, mafisadi, wadangaji, mbele ya safari huishia kufilisika sababu ndani ya nafsi zao ni masikini.

Uamasikini unaambukiza (contagious), umasikini ni hali ya akili kuamini mafanikio ni muujiza na sio uhalisia wa matokeo ya jitihada.

Umasikini unapigwa vita kwa kutafuta namna tofauti tofauti za kujitafutia kipato bila kudharau ni kiasi gani unaingiza bali muhimu ni malengo ya leo, kesho na kesho kutwa kipato kinakupeleka wapi kukutoa hapo ulipo.

Tunaposema umasikini ni adui wa taifa haya ndo matokeo ya kudharau hiyo kauli. Unakutana na binti anatumia mwili kama qualifications ya kufanya maisha na wewe ila ukikaa nae ndani hana mchango katika swala la kupigana na umasikini cha zaidi atavuta familia yake waje karibu yenu wamsaidie kukuambukiza umasikini.

Ukiona mwanamke hana elements za productivity kwa namna yoyote basi jua unaandaa kizazi au familia ya watu masikini. Mwanamke mwenye maradhi ya umasikini hatokei familia ya watu wa kipato cha chini, anatokea familia ya watu wasio na utu na wenye uchu na tamaa, hao ni masikini pure, aidha wawe na pesa au mafukara umasikini utaugundua kwao kupitia tabia zao za tamaa na uchu na husuda za kukurudisha nyuma wewe ili wao kupata.

Nilishawahi ona familia ya mzee ambae hana uwezo sana, ni mkulima tu wa kipato cha chini, binti yake ameolewa na kijana ana uwezo wa kipato cha kati. Ila yule mzee kila mwezi alikuwa anafunga kiroba cha mahindi, unga, na gallon kubwa ya mafuta ya alizeti kumtumia binti yake na mumewe kutoka kwenye ghala yake. Na akifanya mauzo ya mazao yake ya kilimo anatoa sehemu ya pesa anamtumia kijana na binti yake.

Imagine huyu mzee utamwita ni masikini?! Au huyu binti anatoka familia ya kimasikini?! Umasikini ni akili au fikra ya kuendekeza tabia ya kuelemea wengine ile hali unaweza kupambana kujitafutia na ukasaidia wengine.

Sasa leo, kupitia elimu, tumezalisha kundi kubwa la vijana makabwela na mafukara wa hiyari wasio na mawazo ya maendeleo hata kidogo. Hebu wazia ni kwa namna hii tutafikia malengo ya taifa kweli ya kuwa uchumi wa kisasa na kuwa na idadi ndogo sana ya watu wa kipato cha chini.?!

So ndugu, kumalizia tu niseme, ukiona binti analeta mazoea ya kuomba pesa usipepese macho wala kuona aibu, mwambie ukweli, mwambie aache tamaa na kuendekeza akili za kimasikini, kama anataka kupata mahitaji kwako kwanza ajue wajibu wake kwako katika vita na umasikini miili ya ngono hii isikuponze ukatumia pesa yako uliyoipata kwa shida sana kirahisi rahisi kisa unafuata maneno ya mjini kuwa sijui mwanaume wa kweli sio bahiri kwa mwanamke.

Mtawalaumu hawa mabinti wanaodanga ila ukweli ni kuwa sisi wanaume baadhi yetu ndio tunachangia huu utomvu wa maadili na nidhamu kukua. Imagine kama wanaume wote tukaweka azimio la kutotoa pesa za matumizi katika maswala ya ngono nje ya kusaidia, utaona kama hawa wadangaji watakuwapo.

Kwanza familia zitaimarika, ndoa zitaheshimika, na wanawake watajua umuhimu wa ndoa. Hivi viburi vyao vinakuja sababu wahongaji na mabwege wa kutoa hela mpo wengi, na mimi nasema nikikuta mwanaume ambaye hajaoa mwanamke ila alikuwa ana muhudumia kama mke kisha huyo mwanamke akapata mtu mwingine akapita hivi, mimi nitatetea huyo mwanamke, sababu yupo sahihi hawezi olewa na mwanaume mpuuzi anayetoa pesa nje ya familia au nje ya ndoa.

Huwa tunawaona wanawake ni wakatili kwa kuwakimbia watu waliowahudumia ile hali hawakuwa wanaume wao wa ndoa. Ila ngoja nikwambie wanawake wenye akili huwa wakiona mwanaume ni bahiri wanajua huyu sasa ni mwanaume wa ndoa maana pesa zake hazitachezewa na wadangaji.

Sasa nyie mnaojiita laki si pesa endeleeni kupoteza pesa kwa mshahara wa ngono na maradhi, wenzenu wanajenga siku hizi, akipata maboya yake kama sita akijisikia usiku anayapigia kuwa anafukuzwa kodi yanatoa laki tatu kila boya moja anajipatia 1.8 ya fasta. Wewe unajikuta mwanaume kumbe fala tu, ndio maana siku hizi watoto wa kike maisha kwao ni utelezi tu akiwa na mwili wa kudatisha.... Sasa wewe endelea kusema laki si pesa honga, watoto wako kwenye mipumbu yako unawadhurumu urithi wao sababu ya kutaka kuonekana mwamba fala m'moja wewe.

Hayo ni maneno tu ila ukweli ni kuwa mwanamke ambaye sio mkeo kumpatia fedha ni hisani tu, ila sio jambo la lazima au msingi kutoa pesa kwake hata kama ni buku ya vocha. Wacha wakuite bahiri sijui mkono mfupi, but usiwe under pressure kutoa pesa ambayo haupo tayari kutoa kwasababu unataka kuonekana mwanaume, but kama ni mkeo mnaishi nyumba moja then atajua matumizi na kipato chako so hawezi omba hovyo.
 
Back
Top Bottom