The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Katika hatua ya uibuaji wa mradi (Project Plan), ni baadhi ya taarifa tu (facts and issues) hujulikana na zingine hazijulikani. Kutojulikana kwa taarifa hizi zingine (Unknown facts &issues/total guesswork) haipaswi kuwa sababu ya kutokuwa na mradi, hivyo ni jukumu la timu ya uibuaji wa mradi kujenga dhana juu ya taarifa hizi ambazo hazijulikani (Assumptions on unknown facts & issues) Dhana lazima zijengwe kwa uangalifu na ufikiriaji mpana (They should be educated guess; a likely conditions, circumstances)
Dhana na vikwazo mradi (Project Assumptions&constraints) ni matukio (events) au hali (circumstances) zinazotarajiwa kujitokeza wakati wa uhai/utekelezaji wa mradi.
Dhana na vikwazo katika mradi vina hali (conditions) zifuatazo;
- Zipo nje ya uwezo wa mradi (Outside project control)
- Lazima zitokee ili mradi uweze kufanikiwa
Dhana (assumptions) huleta uwezekano (possibilities) katika utekelezaji wa mradi wakati vikwazo (constraints) huleta mkwamo (limits) katika utekelezaji wa mradi.
Katika hatua ya kwanza kabisa ya uibuaji wa mradi; dhana na vikwazo (assumptions & constraints) ni vyema vikaanza kuangaliwa katika vipengele vifuatavyo;
- Bajeti; makadirio ya gharama za shughuli na rasilimali zingine zinazotakiwa ili kukamilisha mradi
- Ratiba (schedule); makadirio ya upangaji wa shughuli na matukio mengine katika mradi ili kuendana na ratiba ya mradi.
- Ugavi; makadirio katika utendaji wa watoa huduma ya ugavi ili kuendana na matakwa na viwango vya mradi.
- N.k
- Utambuzi (Identifying); tambua dhana na vikwazo vyote ambavyo unadhani vina nafasi kiathari katika mradi wako.
- Zitathmini (Assess); baada ya kuwa umezitambua dhana na vikwazo; tathmini matokeo na athari zake katika utekelezaji wa mradi.
- Kuzihusisha katika mpango wa mradi (Incorporation)
- Udhibiti (Control); wakati wa utekelezaji wa mradi; dhana zitakuja kuthibitika ni za kweli au si za kweli na kuathiri utekelezaji wa mradi, hivyo ni jukumu lako kukabiliana na mazingira haya.
- Mapitio (review) hii hufanywa baada ya mradi kuisha, hatua zote ambazo zilipitiwa kuanzia utambuzi, mpaka uthibi wa dhana na vikwazo zinapaswa kufanyiwa tathmini.
Pata huduma ya;
- Uandishi wa miradi ya kijamii na kiuchumi (Socioeconomic projects) na kisanii (Artistic projects) kama matamasha n.k
- Utoaji wa semina katika Usimamiaji wa Miradi
The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania