Dhana kubwa ya mafanikio

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Kuna mafanikio aina mbili katika maisha japo dunia huangalia zaidi mafanikio ya nje lakini kuna mafanikio ya ndani ambayo ndio ya muhimu kuliko vyote.

Kumbuka kitu chochote kabla hata hakijatengenezwa kwa uhalisia hutengenezwa ndani ya kichwa chako,kinachotokeza nje ni matokeo ya kile ulichokiwaza na kuamua kukifanyia kazi.

Vivyo hivyo na kwa mafanikio kwenye kila jambo mafanikio yanayoanza ni ya ndani kwanza ndani ya nafsi yako,ukifanikiwa ndani ya nafsi yako ndipo utaweza kuyahamisha mafanikio yako kutoka ndani hadi nje,hauwezi kufanikiwa nje bila kuwa na mafanikio ya ndani,ndio maana washauri wengi wanasema unatakiwa kujiamini kwanza ndio na wewe uaminiwe.

Mfano wa kufanikiwa kwa ndani ni kama vile umefungua biashara na kuipa malengo ya kusimama baada ya miaka 2 ikiwa inamaanisha kipindi hiki unaweza kuuza ama usiuze kwako itakuwa haina tatizo ila hadi miaka 2 ikikamilika iwe imesimama,haya ni malengo ya ndani ambayo umejiwekea,hivyo kipindi hiki unaweza kuwa na vipindi vya kuuza na kutokuuza kabisa kwako haitakuwa shida sababu ya malengo ya ndani,hata akija mtu kuulizia tu na kuondoka kwako ni mafanikio sababu inaonyesha tayari watu wanakutambua kwenye soko,lakini kwa mtu alieko nje mafanikio kwake ni kuona biashara yako inauza kila siku na inapanda kila siku akiona imesimama ama vitu haviendi yy kwake sio mafanikio.

Mafanikio ya ndani ndio yanayotupa hamasa ya kufanya vitu vikubwa,kwenye mahusiano unaelezwa sifa mbaya za mtu wako sababu ya mafanikio ya ndani unayabeba na kuendelea bila kuathiri mahusiano,kwenye kazi ukifanikiwa ndani yako kuimaliza kazi kwa mafanikio basi hata nje utaimaliza kwa mafanikio,changamoto pia zinapokuja ukifanikiwa ndani basi hata nje utafanikiwa uko kwenye changamoto kubwa lakini unatabasamu na furaha hiyo ni kwa sababu ya kufanikiwa ndani.watu wengi tumekuwa na tabia za kudharau mafanikio yetu ya ndani sisi wenyewe na kukimbilia kuridhisha wa nje kuonekana umefanikiwa matokeo ama gharama ya hii huwa ni kubwa hasa pale inapokubidi kufanya kitu nje ya uwezo wako na hali hii imefanya kupungua sana kwa utu,upendo,urafiki,mahusiano yaliyo imara,sababu ya kutafuta mafanikio ya nje kabla ya yale ya ndani.

Badilika leo anza kutengeneza mafanikio ya ndani kwanza yakijaa ya nje huja yenyewe
,hata biashara mafanikio ya ndani ya biashara ni kuondoa tatizo la mteja wako,pesa inakuja kama fanikio la nje hivyo kwenye biashara pia hangaika kuhakikisha unatatatua tatizo na pesa itaongezeka,kwenye mahusiano usipambane kutafuta uaminifu wa mpenzi wako kwa vitendo vyake ama sheria zako kwanza jenga uaminifu wako kwake ndani yako ambao utakuwa na nguvu ya kukupa mafanikio yote.

Elisha Chuma
Mshauri wa biashara,ujasiriamali na Branding

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyuzi kama hizi vijana wengi hawazisomi ,na mafanikio huwa kwenye nyuzi kama hizi ,big up bro
 
View attachment 1006692

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujumbe mzuri sana.

Hongeara na asante sana bwana Elisha Chuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hongera kwa kutupa ujumbe.
huwa najiuliza wewe huwa unafikilia mambo gani unapo kuwa pekee yako maana inaonekana kuna kitu kikubwa ndani yako.
 
Back
Top Bottom