Dhana fikirishi ya "sayansi"

cDNA

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
353
348
Habari zenu wakuu...
Nilipokuwa shule ya msingi niliaminishwa kuwa sayansi ni somo maalumu na ndugu yake sayansi kimu. Masomo kama jiografia na historia hayakuhisabiwa kuwa ni sayansi.
Hali iliendelea hivyo hadi sekondari. Tulipokuwa kidato cha tatu tukatenganishwa kuwa kuna madarasa ya wanasayansi na wana arts.
Chuo napo nikashangaa kuona yale msomo yaliyokuwa yanaitwa ya arts yameingizwa ktk sayansi na yanaitwa "social sciences" ambapo ni pamoja na historia, jiografia, psychology n.k. Wakati masomo ya biolojia, Kemia, Fizikia n.k. yakiitwa "natural sciences".
Kisha kipindi fulani bodi ya mkopo ikawa yatoa kipaumbele mkopo kwa wasomao sayansi...halafu wakati huo huo wasomao social sciences wanabaguliwa!
SWALI: Nini "science"? Mbona ktk mazingira fulani twayabagua masomo fulani kuwa si sayansi halafu kwa upande mwingine twayaita sayansi?
 
Back
Top Bottom