Dhamira yangu sasa ni kuondoka Dodoma wiki ijayo!

Abaki,ingawa sio lazima kupigana saa zote ila kwa hili uwepo katika uwanja wa mapambano ni muhimu!!!!

Baki hapo mkuu ila kila unapoona mambo yanapinda sema kwa sauti bila ya woga historia itagawanya hakika hamtokaa kundi moja!!!!
Mkuu mwanzoni nilikuwa sikuelewi lakini sasa nimeanza kukuelewa
 
Lema bwana, huyu hawezi ku-survive mahala hakuna fujo. Wanaanza kujadili rasimu kuanzia kesho na yeye ni mweupe atakaa kufanya nini? CHADEMA nzima tunamtegemea Tundu Lissu atuongoze cha kusema kwenye rasimu. Shule muhimu jamani. Watu wa Arusha poleni.

Kweli chadema shule muhimu kama shule ya yule mbunge wa korogwe vijijini mganga wa kienyeji,maana yule msomi si anaitwa profesa maji marefu?
 
Waondoke tu coz wao ndo wanatucheleweshea Katiba Mpya.

Watu wa buku7 at work,nakumbuka makamba alivyowapa simu za samsung kibao muwe misukule ya ccm kwa kushambulia hoja za upinzani na wapinzani,hivi mnalipwa kwa kila unavyopost au kwa siku mnayokuwa kazini?
 
Nimezungumza mara nyingi na wengi wengine wamazungumza pia, UKAWA umekuwa umoja ulioshindwa toka kuanza kwa Bunge hili la katiba, Viongozi wake wamekuwa wanajifanya wana busara sana, kwa kweli wameonyesha hawana uzoefu na masuala ya misuguano ya kisiasa wanabadilisha mara kwa mara misimamo yao bila CCM kubadili misimamo yake, wamepoteza kila kitu na CCM wamepata kila kitu, UKAWA wameishia kulalamika tu kwa namna ya kuwapumbaza wananchi, Hakika kubadilisha mara kwa mara misimamo kumepoteza umaarufu wa vyama hivyo vya upinzani na kumesababisha ajali nyingi za kisiasa, unaweza kuona viongozi hawa wa upinzani walivyokua wanajing'atang'ata na kutumia misemo mingi tena in defeated tone wakikubali hoja ya CCM ya kura ya wazi, ni maoni yangu kuwa mfumo wa kura zote mbili yaani ya wazi na ya siri , kama alivyosema prof, A. Sherrif in essence ni mfumo wa kura ya wazi, UKAWA wametuonyesha kuwa ni wachanga mno katika siasa za majadiliano na mibinyo na zaidi ya yote ni usaliti mkubwa wa misimamo yake, usaliti huu wa kimisimamo hauwezi kufichwa katika kichaka cha " sisi hatutaki tuonekane ni sababu ya kukwama mchakato wa katiba mpya " sentensi hii imekuwa sas ndio kauli mbiu ya UKAWA , hakika hii ni kauli ya woga, kujipendekeza na iliyosinyaa sana, Wananchi hawahitaji katiba mpya tu, wanahitaji katika yao [ Katiba ya Wananchi ], sasa ni hakika kuwa kushindwa huku kwa UKAWA katika hatua za mwanzo hakonyeshi matumaini ya kutetea katiba ya wananchi, tunachoweza kufanya ni kujaribu kupenyeza na kushawishi maoni ya wananchi kwa wajumbe wa CCM ambao kimsingi ndio wanaonyesha kusimamia wanachokiamini au kuaminishwa au kutoweka matumaini yoyote ndanin ya katiba mpya, tukifanya yote haya wawili jambo lililo wazi ni kuwasubiri na kuwaadhibu hawa wanaounda ukawa mwaka 2015, wakiendelea hivi hakika wananchi watawaadhibu, na wananchi watakuwa na kazi rahisi ya kuwazika katika kaburi la sahau kwa vile watakuwa wameshajichimbia kaburi lao wenyewe ndani ya Bunge la katiba.
 
mkuu haya Mimi nimeliona hili ukawa wanayumbishwa sana
 
Unaposema dhamira yako ndiyo itakayokuondoa kwenye ushiriki wa bunge la katiba
hii ni sawa na kuwasaliti watu wako.

Wale wote/wajumbe walioko dodoma kama watataka kujiondoa kwenye bunge la
katiba ni bora wakatumia njia ile ile iliyowapeleka bungeni.

Kama kweli wanao nia ya dhati ya kujiondoa ni bora wakawashirikisha waliwachagua/
waliowapendekeza kwa maana ya kukusanya sahihi zile zile zilizohitajika kuwawezasha/
kuwapitisha wao/yeye kuwania ubunge/nafasi hizo/hiyo.

Kujiondoa hivi hivi eti kwa kushauriana na viongozi/wajumbe wenzenu ni usaliti
kwa waliowachagua/kuwapendekeza kwani ikumbukwe kuwa hamkuchaguliwa/kuteuliwa na
viongozi/wajumbe wenzanu.

Na ikifikia hatua ya yao/yeye kujiondoa ni bora tamko/matamko lako/lao likafanyaika/yakafanyika
nje ya bunge (kwenda kuwaambia waliowapendekeza/kuwachagua) ili kutoa mwanya kwa wengine
kuchukua nafasi zao kama itaonekana inafaaa.

Rai kwa wajumbe:

Wajumbe wasifikiri kujitoa ndio itakuwa njia iliyo bora ya kutatua tatizo wanaloliona,bali
inaweza kuwa ndio njia iliyo bora zaidi kwa wenzao kufanya vile wanavyotaka kufanya.

Na ikumbukwe kuwa kujitoa pekee haitoshi kuonesha kwamba wao/yeye ni wazalendo
sana kupita wenzao sana sana inaweza kuonesha ni jinsi gani pesa za walipa kodi zina-
vyotafunwa kwa utashi wa mtu binafsi.

Ili kuonesha uzalendo wa kweli,ni bora kabisa kwa wale wote wanataka kujitoa wakawajibika
kurudisha gharama zote ili isionekane kwamba walikwenda bungeni ajili ya kukwapua pesa za
walipa kodi na kutafuta sababu zisizo msingi kujiondoa pasipo kuwashirikisha waliowachagua/kuwapendekeza.
 
ulemavu wa akili ni tatizo kubwa sna kwa taifa hili kama wewe.

Mkuu unadhani ni ulemavu wa akili,ni njaa ndio inayowasumbua hao vijana hawana njia mmbadala ya kujipatia kipato zaidi ya hiyo.
 
Lema acha kutishia nyau wewe.Mwenzako Mkosamali alitishia hivyohivyo lkn bado yupo.Kuna wabunge wengi hata wewe ukiondoka hakuna tatizo labda pengo kwenye UKAWA.Hauna faida bungeni kazi yako kutukana tu.Bye Bye Lema.
 
Ni jambo jema. Hata maandiko yanaonya watu makini wasipende kukaa barazani pa wenye mizaha. Bunge la katiba limejaa mizaha, wenye busara na waamue sasa.
 
Lema using'ng'ania kila UKAWA mnachoongea wenzenu wakiunge mkono na msipoungwa mkono ndo mnawatukana wenzenu (ccm na wale 201).Kufanya hivyo ni kuonesha uchanga wa kisiasa na si umaarufu kama wenyewe mnavyodhani ili muonekane na wananchi, kumbe watu tunawaona ni watu msiopenda kushindwa na mna lazimisha.Jifunzeni kujenga hoja na si kuwatukana wenzenu.
 
Nilikuwa na mawazo haya muda mrefu kweli, kwa nini wajumbe wanaoamini "mchakato haupo sawa" pale Dodoma hawajitoi!!
Wewe Lema umefanya nilichokuwa nawaza, ingawa mimi niliwafikiria sana wale wa kundi lile la 2..!!
Bravo Lema, hakuna la maana kule Dodoma
 
Ondoka tu. Mnanikera na tabia yenu ya kulazimisha kila mnachokitaka. Hamtoi hoja za maana zaidi ya kuituhumu tu CCM. Wenzenu CCM wanajibu kwa hoja nyie mnabaki kulalamika tu. Ondoka nenda kwa wahuni wenzako.
 
Ndo mana upo mle ndani, wewe ni sehemu ya mabadiliko. Unless huamini kama unaweza kuleta hayo mabadiliko ambayo watu wa Arusha wanayatarijia toka kwako na watanzania wanaokupenda.Kujitoa katika mchakato ni ishara ya uwoga na kutojiamini kitu ambacho kiongozi mkubwa kama wewe hatukutarajia kukiona toka kwako.UNAKIMBIA...? Huwezi kuwa Jasiri wewe, watu wa Arusha watasikitishwa sana na kitendo chako.
Kama sikosei Jana ni wewe peke yako ndiye hukupiga kura ilihali ulikuwa upo ndani ya ukumbi wa Bunge, yaani wewe utafanya watu wajute kukuchagua maana hujielewi aysee..

Kwa kuongezea umeomba (Lema) na umechaguliwa kuwa Mbunge ili uwakilishe watu wa Arusha na Watanzania ndani ya Bunge. Hii ni pamoja na kutoa maoni, kuchangia, kukosoa serikali inapobidi, na shughuli nyinginezo za bunge. Mapambano yako ndani ya Bunge, unapokimbia maana yake nini? Ni kweli hujielewi? na hata mimi sikuelewi.
 
Back
Top Bottom