Dhamira ya Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhamira ya Rais Kikwete

Discussion in 'Sports' started by Mpita Njia, Aug 16, 2012.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado ni dhamira ya Serikali yake kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania – La Liga – kutembelea Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania katika Tanzania kusaidia kufanikisha dhamira hiyo.Aidha, Rais Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita katika Poland na Ukraine.Akizungumza na Balozi mpya wa Hispania, Mheshimiwa Luis Manuel Cuesta Civis mara baada ya kupokea hati yake ya utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika leo, Alhamisi, Agosti 16, 2012, Ikulu, Dar es Salaam, Rais amesema:“Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbunga zetu maarufu za wanyama,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:“Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.”Rais Kikwete pia ameipongeza Hispania kwa kutetea ubingwa wake wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano ya Euro 2012 yaliyomalizika karibuni katika Poland na Ukraine.“Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.”EndsNOTE: Taarifa hii imetumwa na salva kwa vyombo vya habari jioni hii
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Bread and circuses.
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Upuuuzi upuuuzi upuuzi mtupu. Usanii usanii usanii mtupu. Watanzania wanahitaji maisha bora siyo timu bora ya mpira. Huu upuuzi awaachie mawaziri wa michezo na makocha wa timu husika. Kwani rais hana mambo mengine muhimu ya kutolea ufafanuzi? Mbona ameshidwa kutaja mali zake na kutoa maelezo kuhusu shutuma zinazomkabili kuwa aliingia madarakani kwa pesa ya wizi wa EPA? Huu muda wa kukamia upuuzi anaupata wapi?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Dhamira yangu kama mwananchi ni kuona watanzania wengi wanaamka na kuanza kuchapa kazi na kushiriki katika shughuli mbalimbali za uchumi na uwekezaji. Kuangalia timu za hispania naangalia kwa luninga yangu if I have time
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi timu ya Hispania itakuja kucheza na timu gani bongo?
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Janga Kuu!
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wapi Ritz?
   
 8. b

  bainamugisha Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah kikwete my president???? Ndo maisha bora hayo kwa kila mtanzania???? Unatusikitisha watanzania kweli mchagua nazi upata korona''''
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Nalo neno mkuu.
   
 10. afrique

  afrique JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 495
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hilo la kutembelea mbuga linanifanya nihisi kuna jambo hapa!waletwe kwa cost zetu na mbugani wapelekwe bure!ngachoka kuchu
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,739
  Trophy Points: 280
  it doesn't get more insane than this, does it?
   
Loading...