Dhambi saba mbaya zaidi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,640
729,614
Tunaendelea na ufunuo wa siri ya namba saba...kwenye mwendelezo huo wa siri ya namba saba leo hebu tujadili hizi dhambi saba ambazo ndio kama mizizi saba ya dhambi zote za ulimwengu huu...kwamba kupitia hizi ndio zao la madhambi yote unayojua na kuyafahamu hapa duniani

Kwa mshangao wa wengi dhambi nyingi unazowaza si kati ya hizo saba.. Hebu tuzipitie moja baada ya nyingine

1. Tamaa(lust) tamaa hii ni ile ya utamanifu wa kimwili, na kutaka kuitosheleza nafsi iwe kingono, na tamaa nyingine zote za nafsini na hisia za kimwili

2. Uroho(gluttony) uroho ni sehemu ya tamaa, lakini hapa ni kwenye kumiliki na kutawala zaidi..dhambi nyingi za uchawi na mauaji zimetokana na uroho

3. Choyo(greed)ukiangalia mfuatano huu utagundua kitu cha kushangaza mno, uchoyo ni tunda la uroho.,MTU mroho daima ni mchoyo .. Uroho na uchoyo haviachani

4.Wivu(envy)mtiririko ni uleule ,MTU mwenye wivu ni mchoyo ni mroho pia ana tamaa

5. Ghadhabu(wrath) hapa tumepoteza watu wengi na hata kugombana kutokana na ghadhabu za mmoja ama wengi..sababu kubwa zikiwa ni wivu choyo tamaa nk..

6. Uvivu(sloth)..kama ulikuwa hujui uvivu pia ni dhambi... Na matokeo ya dhambi hii ni kutaka kupata na kustarehe bila kutoka jasho hapa wizi utapeli udanganyifu vimefanyika sana

7. Kiburi(pride) unaweza pia kuita majivuno..kwamba Mimi ni mimi na hakuna zaidi yangu mimi...matatizo mengi yametokea kwenye jamii kutokana na kiburi na kujiona bora kuliko wengine (hata JF tunao)hii ni dhambi ya kunajisi uumbaji na kumkataa Mungu ama la kumkosoa.nknk

Hizi ndio dhambi saba kuu ...najua hakuna mkamilifu kati yetu na wote tunashiriki dhambi hizi kwa njia moja ama nyingine...na wote tunajijua udhaifu wetu ulipo ila kwa kiburi na unafiki wetu huwa tunajivika koti jeupe kuficha uchafu uliomo ndani yetu

Mungu ibariki Tanzania na wanyonge wake...!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom