Jamani njoni muone, naleta kwenu habari
kwa wembamba na wanene, nawajia kwa shairi
Huyu Mwanajamiione, kaleta mada hatari
Mapenzi ya siku hizi, ni kweli yamenanihi
Shida wayakimbilia, wakiwa bado watoto
kisha wanatulilia, wamejawa na utoto
kwa kweli hawajatulia, ni kama waota ndoto
Mapenzi ni wa wakubwa, waliokamaa akili
Mapenzi si lelemama, ni vizuri tufahamu
mwulize baba na mama, kama kozi wametimu
badala ya kulalama, heri muwe moja timu
Kama wewe ni mtoto, mapenzi si saizi yako
subiri kwanza ukue, hili shauri nakupa
na kanuni uzijue, tulia na uache pupa
na utoto uutue, na ujinga kuutupa
vinginevyo ni hatari, kukimbilia mapenzi
mwamkumbuka kitila, yule aishi tabata
alijifanya msela, leo sasa anajuta
karudia ukapela, amekumbwa na utata
Mapenzi yana kanuni, ukizikwepa hatari
kaburunye memba mwenza, karibu tena karibu
nionavyo umeanza, tena kwa kujaribu
naona umejiponza, kuweka jina mujibu
kanuni na chakachua, kamwe haviendani
kamwe haviendani, kanuni na chakachua
japo siendi undani, lakini nimegundua
wewe umekwenda ndani, na mengine kuibua
kanuni na chakachua, kamwe haviendani
sasa tuje kwenye mada, infi nayo jumuisha
kwani hilo sijaona, wewe ukijumuisha
vyawezaje kuendana? tena bila kushtusha...
kanuni na chakachua, kamwe haviendani
Jamani njoni muone, naleta kwenu habari
kwa wembamba na wanene, nawajia kwa shairi
Huyu Mwanajamiione, kaleta mada hatari
Mapenzi ya siku hizi, ni kweli yamenanihi
Shida wayakimbilia, wakiwa bado watoto
kisha wanatulilia, wamejawa na utoto
kwa kweli hawajatulia, ni kama waota ndoto
Mapenzi ni wa wakubwa, waliokamaa akili
Mapenzi si lelemama, ni vizuri tufahamu
mwulize baba na mama, kama kozi wametimu
badala ya kulalama, heri muwe moja timu
Kama wewe ni mtoto, mapenzi si saizi yako
subiri kwanza ukue, hili shauri nakupa
na kanuni uzijue, tulia na uache pupa
na utoto uutue, na ujinga kuutupa
vinginevyo ni hatari, kukimbilia mapenzi
mwamkumbuka kitila, yule aishi tabata
alijifanya msela, leo sasa anajuta
karudia ukapela, amekumbwa na utata
Mapenzi yana kanuni, ukizikwepa hatari
Acid nimekupata, hoja nataka nijibu
ingawa ina utata, mi sitaki niwe bubu
hili ni kubwa sakata, naja na hoja za babu
Infi mchezo mbaya, sithubutu kuucheza.
hebu mtunze shemeji, ndani ya ndoa ubaki
usije lijua jiji, upatwapo na mikiki
nikupa yangu meseji, pokea uepuke dhiki
Infi mchezo mbaya, ni hatari kuucheza
maandiko yakataza, kutoka nje ya ndoa
yanatupa na mwangaza, ndoa isiwe na doa
hakuna ililosaza, na mwongozo yametoa
Infi mchezo mbaya, ni hatari kuucheza
ridhika naye mmoja, acid nakushauri
tena mkae pamoja, muiepuke hatari
usijeleta vioja, nakuonya kwa shairi
Infi mchezo mbaya, ni hatari kuucheza
hapa tamati nafika, umeelewa nadhani
sidhani umeudhika, wewe ni mtu makini
usije kughafilika, ukanaswa hatiani
Infi mchezo mbaya, ni hatari kuucheza
leo umenishangaza, tena meshangaa sana
na wengi umewakwaza, kwa hii ya kwako dhana
ati utoto waweza, ikawa sababu sana
mapenzi kuyaingia, uwe na umri gani?
utoto unaosema, maanaye methibiti
bado hajui kusema, kutembea kwa magoti
kutamka kwa kuhema, mchezo ni wa manati
mapenzi kuyaingia, uwe na umri gani?
enzi za wazee wetu, waweza zikumbukia
ukimaliza la tatu, nyumbayo wajipatia
dunia ujaze watu, vizazi kuendelea
ukitaka kuingia, uwe na umri gani?
kaka kei ana hoja, sema hajaipanga
kachanganya yake hoja, ni wazi hakuipanga
infi chezo lini hoja? kweli hakujipanga
ni wazi ataelewa, kaka kei kachanganya
tena basi kwenye rika, hapo ndo balaa
ni lini ilisikika?, kwamba umri una baa
eti penzi lina rika? kweli hii balaa
ni wazi ataelewa, kaka kei kachanganya...
its exciting
Acid
kaburunye kachemka, hoja ameidandia
mapenzi yalotukuka, na yale ya kuchakachua
kapu moja ameweka, nadharia kuvumbua
vitu hivi sio sawa, hata kama vya fanana
hata kama ya fanana, tuwi haliwi maziwa
Kurwa na Doto ni wana, tofauti kwa muruwa
wajuzi wenye maana, kundi moja huwatoa
penzi la kuchakachua, ni mtindo wa kisasa
ni mtindo wa kisasa, penzi la kuchakachua
ni jambo la kianasa, kama raizoni ze kuwa
wakichoka watatosa, fesheni new kutoa
rika halina makosa, Kei kijana hukuwa?!
lolol
Gaijin ndugu yangu, naona hujanelewa
Lisome neno la Mungu, infi imekataliwa
Zipitie hoja zangu, polepole utaelewa
kuchakachua mapenzi, ni chukizo kwa muumba
Mapenzi ni ya wawili, kuchanganya si vizuri
Siyo jambo la adili, chakachua ni hatari
Ni kinyume cha maadili, Gaijin tafakari
Kuchakachua mapenzi, siyo jambo la heshima
Fikiria kwa makini, mkeo akitendewa
Wengine wamrubuni, penzi kwa nje kutowa
Na wajue wa mtaani, na masela ametiwa
Siyo jambo la heshima, mapenzi kuchakachua
Hili tusilikubali, ndugu zangu nawaasa
Hatari yatukabili, kuchakachua ni kosa
Mungu aipishie mbali, mioyo ipigwe misasa
Kuchakachua mapenzi, wala tusishabike
Mwenye hoja ya msingi, kusapoti atwambie
Atupe sababu nyingi, kwanini ashabikie
Atupe hoja kwa wingi, ndipo tumkubalie
Kuchakachua mapenzi, si jambo la kujivunia
Mimi naenda kulala, mpenzi anisubiri
Ninayajua madhala, chakachua ni hatari
Ni uchafu ka jalala, kuchanganya si vizuri
Lidhika na huyo mmoja, muhudumie vizuri
kaburunye kaburunye, tafadhali tafadhali
rejea palipo penye, penye mada mada tafadhali
ulikoenda si kwenye, mada hii ya halali
kaka kei umeanza, kupindisha kamba yetu
kupindisha kamba yetu, kaka kei umeanza
bila-jali mada yetu, wewe yako umeanza
tafadhali ndugu yetu, irejee mada kwanza
kaka kei umeanza, kupindisha mada yetu
Wenye akili za kitoto, mawazo yao ni ngono
Tunda kwao ndio ndoto, tamaa mpaka kwenye meno
Watapatwa na msoto, wasipokemewa kwa neno
Jamani nasisitiza, mapenzi si ya watoto
Mapenzi haya ya sasa, si kama yale ya kale
Tumeuvika usasa, tukakosoa wa kale
Kila mtu mambosasa, hakuna katoto kale
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua
Si wakubwa si wadogo, hata ngazi mbalimbali
Si kanisa si vigogo, wote wameenda mbali
Dunia mekuwa ndogo, waletwa hata wa mbali
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua
Ilianzia mafuta, super kutiwa ya taa
wengi tukafurukuta, hali hiyo kukataa
Tukaujenga ukuta, biashara kukataa
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachuwa
Kama vile ikutosha, makombora yakahama
Kuanzia kwa Mugisha, mpaka kwa Bi Halima
Miili wachangamsha, bila kujali kiyama
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua
Mume atoka na yule, penzile alichakachua
mke anagawa kule, peremende chakachua
Huyu mke wa yule, jirani achakachua
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua.
Nilidhania ni mafuta, pekee huchakachuliwa.........
Hapo ndipo ulipokosea mjukuu...Mh Naona JF ina malenga wa kutosha tu......... kuna umuhimu wa kuanzisha chama lol...... mwenyekiti awe Asprin na katibu wake Acid (This is a better chama than that of Infidelity)
Acid kamanda wangu, nimekupata sawia,
Kaburunye ndugu yangu, hoja kaipotezea,
Kavipindisha vifungu, sredi kaichakachua,
Hoja mbona iko wazi , mapenzi ya chakachua?
Hapa hatusemi dhambi, ila penzi chakachua,
Tusitoke kwenye kambi, hoja kuvurugia,
Hoja haina kitambi, tuhofu itavilia,
Hoja iliyo mezani, ni mapenzi chakachua.