Mjukuu mai dia, mimi siko lawamani,
Mila naizingatia, tangu enzi utotoni,
siwezi kuichenjia, nitakuwa matatani,
mwanaume kaumbiwa, kuishi na wake wengi.
Mwanaume kwa yakini, infi kwake asilia,
Acha mwanamke ndani, wa nje kuhudumia,
Kuweka sawa mizani, wanawake mezidia,
Mwanaume ameumbwa, kuishi na wake wengi.
Mwanamke kibishia, kisasi talipizia,
Hiyo ndio chakachua, mjukuu anasemea,
Infii haina nia, kuanzisha chakachua,
Mwanaeme kaumbiwa, kuishi na wake wengi!:welcome::welcome::welcome:
Hahahahaa naona nimekushika pabaya Kamanda...... nipe tofauti ya chakachua na infii tafadhali loh
OOppps you missed me again... and probably infii regulations hujazielewa... Infii by no means replaces the prime love and therefore you can never compare the two. in actual facts infii ni kama chachandu kwenye pilau au maziwa kwenye kahawa... lengo lake kuu ni kuboresha na sio kushibishaInfi huleta amani, kwao wasojua penzi
Sijaribu kwa fulani, anojua mapenzi
Hisia ikiwa moyoni, nataka penzi ulienzi
Infii ni chakachua, ni penzi liso hisia kamanda !!
Kiziangalia sheria, za infii zinavyosema
si kama penzi huria, infii hatakiwi sema
Hutakiwi fikiria, fidileta kwa mtima
Infii ni chakachua, ni penzi liso hisia kamanda!!
Kamanda hapa napinga, kwa infii kutoa yote
kutoa yote ni kazi, yahusisha moyo wote
Kama hunayo hisia, huwezi toa yote kamanda.
Deodat karibu, ukaribie na kiti
unijuze kwa karibu, ngoja nibebe na kiti
Mzoefu na tabibu, utujuze kitikiti
Chakachua ya binamu, vipi ikawe ni tamu?
kwanini si chakachue, naye fikiri aweza?
ubunifu kwake yeye, upo umejituliza
mwanamme si pekee, faida anae waza
kama ni kuchakachua, wote wana nguvu sawa.
mwanamke siku hizi, ni mjasiriamali
hesabu haimkwazi, sio kama wa awali
chakachua ya mapenzi, mtaji wafika mbali
kama ni kuchakachua, wote wana nguvu sawa.
Seriously .... I rest my case. Totally defeated I admit.aah kamanda, mbona somo liko wazi?? kuchakachua ni kuongeza kitu chenye ubora wa chini kwenye prime... mfano mzuri kama vile kutumia zana zisizo (madude feki, pingu, nk. kwenye love marking. infii ni ile dhana na tendo la kushare nje ya mstari ukiwa na lengo zuri sana la kuboresha nyumbani, either kupunguza visirani, au kuongeza ujuzi
OOppps you missed me again... and probably infii regulations hujazielewa... Infii by no means replaces the prime love and therefore you can never compare the two. in actual facts infii ni kama chachandu kwenye pilau au maziwa kwenye kahawa... lengo lake kuu ni kuboresha na sio kushibisha
unaona sasa kamanda?? kila sehemu lazma utoe yote, tofauti na chakachua kwani haina ubora.. infii na prime kote lazma utoe vyema
Kumbuka huwezi kutema bigG yako kwa karanga za kuonja
kwanini si chakachue, naye fikiri aweza?
ubunifu kwake yeye, upo umejituliza
mwanamme si pekee, faida anae waza
kama ni kuchakachua, wote wana nguvu sawa.
mwanamke siku hizi, ni mjasiriamali
hesabu haimkwazi, sio kama wa awali
chakachua ya mapenzi, mtaji wafika mbali
kama ni kuchakachua, wote wana nguvu sawa.
Mwanamke asilia, kaumbiwa wa nyumbani,
kuitunza familia, na kutoa burudani,
mume kumtimizia, yajiriyo nje ndani,
Mwanamke chakachua, si mwanamke bora.
Wanyama wa makondeni, mfano wanatolea,
majikeye asilani, hayafanyi chakachua,
na madume makundini, majike yanachangia,
Mwanamke chakachua, si mwanamke bora
mie nimebaki nimeduwaa, ni huyu huyu kichpin?....MJ1 na Gaijin mnanikosha sana, Acid nae wamo khaa balaa kubwa hili, akija Fidel hapa atamwaga utumbo wake mpaka bac.
leo nakula nao sahani moja hawa wachakachuaji mashuhuri ................lol
Nakuwakilisha Nyamayao manake naona mduao wako mkubwa!
asili ya binaadamu, chimpanzi wajua.
yeye bila kulaumu, mabwana achakachua
kuikidhi yake hamu, apendacho ajilia
penzi la kuchakachua, na litumike kwa wote
sauti ya mngurumo, au mnene mkia
mwingi wake mtazamo, akionapo kifua
mawazo yashinda humo, vipi atakilalia
penzi la kuchakachua, na litumike kwa wote
dhana hii ya usawa, sasa sio ngeni tena
mwanamke ana power, kuishi anavyopenda
baolojia kapewa, ya dume yote kutenda
penzi la kuchakachua, na litumike kwa wote
:tonguez:
aaahh swahiba... wanasema riski fil' manyaat aiseeKaditama wahisani, naomba kuwakimbia,
vilivyomo mafrizani, tayari vimeshapoa,
vinapendeza kooni, kwa kasi vikiingia,
Infii asilani, si sawa na chakachua.
Vikishapanda kichwani, lojistiki zaanzia,
kina eliza yakini, mipango najifanyia,
napeleka mjengoni, nao najichakachua,
nikirudi nyumbani, mwepesi najifikia!
Mama matesha tulia, mumeo niko milani,
infii najifanyia, ila sitakurubuni,
nikisha kujisevia, naingia utunduni,
kitanda tukiingia, nakupa maburudani.
Hahahaha!Asprin is HOT! You are :welcome:Asprin is on FIYAH! ......
aaahh swahiba... wanasema riski fil' manyaat aisee
ndo naingia home baada ya kazi ngumu sana ya kuangalia europa league
Teamo is seriusly considering the offer to become a visiting professor wa infii at the university of Washington, GA
swadaktaaaaHahahaha!Asprin is HOT! You are :welcome:
Kamanda naona somo lilieleweka..... Chakachua si sawa na Infii......Thats 2010 Acid's motto!:hand:
Kaizer arent you back yet??
by the way Avatar yako inanikwaza yaani kila nikiiona nasikia kiu!!
Sifaye binaaadamu, yeye si kama mnyama
amepewa ufahamu, ili siweze kukwama
akilize zi timamu, maisha kuyaandama
penzi kulichakachua, ni ujuzi wa kuwaza
mafuta wechakachua, ili kupata faida
mhudumu alijua, pesa singekuwa shida
mbaya kwake ilikuwa, sheria zikampiga
penzi kulichakachua, ni ujuzi wa kuwaza
inapokuja kwa penzi, mfumo ni ule ule
mkakati nguvu kazi, faida waweka mbele
kuchakachua si kazi, mafao yajaa tele
penzi kulichakachua, ni ujuzi wa kuwaza
(naomba ni eleweke kuwa sifagilii hii dhana ya uchakachuaji wa penzi, lakini i have to give to them, ni ubunifu wa hali ya juu) lol