GE2025 Devotha Minja ajitosa ubunge Morogoro mjini kupitia CHAUMMA

GE2025 Devotha Minja ajitosa ubunge Morogoro mjini kupitia CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,442
Reaction score
5,240
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Tanzania Bara, Devotha Minja, Agosti 1, 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Mjini kupitia chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za CHAUMMA mkoani Morogoro, Minja amesema chama hicho kiko tayari kupambana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao na hakitasusia uchaguzi kama ambavyo baadhi wamekuwa wakidhani.

“CHAUMMA tupo imara, tumejipanga, na tutaingia kwenye uchaguzi kwa nguvu zote. Lengo letu ni kuhakikisha tunaleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi”, ameeleza Minja.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hadi sasa, jumla ya wanachama nane wa CHAUMMA wamechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni ishara ya mwitikio chanya ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Screenshot 2025-08-01 175240.png
 
Duh,
Mbogamboga na vibaraka wao wana mambo ya ajabu sana
 
Anadhani atapewa kura na nani?
CCM kuna majimbo watawaachia ACT lakini sio CHAUMMA
 
Hatapata aibu ambayo hajawahi kufanya nayo. Maana ni punda anayerudi bila bwana akijua zile shangwe zilikua zinamuhusu yeye
Mikutano yao yenyewe hainaga watu, watakaompigia kura watatoka wapi?!
 
Back
Top Bottom