Devid Mranda atimuliwa rasmi TPA

Devid Mranda atimuliwa rasmi TPA

Sabato masalia

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2011
Posts
228
Reaction score
134
HATIMAYE yule mkuu wa usalama wa mamlaka ya bandari[TPA] aliyesimamishwa kwa ubadhirifu bwana Devid Mranda leo amekabidhiwa barua rasmi ya kutimuliwa, akikabidhiwa barua hiyo hii katika ukumbi wa mamlaka ya mawasiliano pale ubungo ambapo bodi ya TPA ilikutana kwa kazi hiyo chini ya mwenyekiti wake Prof. Msambichaka, bodi hiyo imemkabidhi barua ambayo inamtaka afungashe virago vyake mara moja na kurudi ofisi yake ya zamani [TISS], Mranda mara nyingi alikuwa akijigamba yeye ni mtu toka ofisi ya rais na hakuna wa kumgusa.
 
Sasa nani kamgusa?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
TPA nako...wameanguka wenye "vyeo" na "enzi"...kaazi kweli kweli
 
Duh! huu mwezi unatatizo na wakuu wa vitengo ya usalama.
 
Alipong'oka Mkurugenzi wa Rasilimali watu Dkt Maimuna nilijua hakuna ataebaki maana nadhani huyu mama ilifikia hadi akajiona akingo'ka yeye basi mungu angekausha Bahari bandarini, Mwakyembe endelea kusafisha bila ya hofu!
 
Tuangalie misingi sio watu.Kufukuza watu bila kuangalia mfumo mzima wa utendaji kazi ni aina nyingine ya ujinga.Tujiulize tangu watu wafukuzwe ufanisi umeongezeka kwa kiwango gani?
 
HATIMAYE yule mkuu wa usalama wa mamlaka ya bandari[TPA] aliyesimamishwa kwa ubadhirifu bwana Devid Mranda leo amekabidhiwa barua rasmi ya kutimuliwa, akikabidhiwa barua hiyo hii katika ukumbi wa mamlaka ya mawasiliano pale ubungo ambapo bodi ya TPA ilikutana kwa kazi hiyo chini ya mwenyekiti wake Prof. Msambichaka, bodi hiyo imemkabidhi barua ambayo inamtaka afungashe virago vyake mara moja na kurudi ofisi yake ya zamani [TISS], Mranda mara nyingi alikuwa akijigamba yeye ni mtu toka ofisi ya rais na hakuna wa kumgusa.

Sabato masalia , Mbona unamshambulia sana huyu mzee . Do you have anything personal against him ? kwasababu siyo mara yakwanza wewe kituma habari kuhusu mtu huyu huyu
 
Mwekyembe safi sana timua wezi hao ninavyoijua TISS misingi yake ni uadilifu vipi jambazi kama huyo afugwe na TISS naamini nako huko watamtimulia mbali
 
Tuangalie misingi sio watu.Kufukuza watu bila kuangalia mfumo mzima wa utendaji kazi ni aina nyingine ya ujinga.Tujiulize tangu watu wafukuzwe ufanisi umeongezeka kwa kiwango gani?

anyway ndo uwezo wako wa kufikiria ulipoishia. hatuna jinsi ya kukusaidia. pole.
 
Sabato masalia , Mbona unamshambulia sana huyu mzee . Do you have anything personal against him ? kwasababu siyo mara yakwanza wewe kituma habari kuhusu mtu huyu huyu

wewe tatizo lako nini? kama hutaki habari usifungue JF. au nenda jukwaa la mahusiano.
 
kutimuliwa kazi sio mchezo wandugu.
yape mengi yamejificha nyuma ya pazia.
 
Tuangalie misingi sio watu.Kufukuza watu bila kuangalia mfumo mzima wa utendaji kazi ni aina nyingine ya ujinga.Tujiulize tangu watu wafukuzwe ufanisi umeongezeka kwa kiwango gani?

Mapato kuongezeka kutoka Bil 17 hadi Bil 43 kwa mwezi ni ndogo hizo?
 
HATIMAYE yule mkuu wa usalama wa mamlaka ya bandari[TPA] aliyesimamishwa kwa ubadhirifu bwana Devid Mranda leo amekabidhiwa barua rasmi ya kutimuliwa, akikabidhiwa barua hiyo hii katika ukumbi wa mamlaka ya mawasiliano pale ubungo ambapo bodi ya TPA ilikutana kwa kazi hiyo chini ya mwenyekiti wake Prof. Msambichaka, bodi hiyo imemkabidhi barua ambayo inamtaka afungashe virago vyake mara moja na kurudi ofisi yake ya zamani [TISS], Mranda mara nyingi alikuwa akijigamba yeye ni mtu toka ofisi ya rais na hakuna wa kumgusa.

atapelekwa tra ili akaendeleze kazi wafanyayi tiss
 
Back
Top Bottom