Silas Haki
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 368
- 39
Wakuu, nawaombeni msaada wenu kwa mara nyingine tena. Laptop yangu imekuwa ikileta shida tangu nilipoi-formart miezi miwili iliyopita. Tatizo lillilopo kwa sasa ni la desktop icons hasa shortcuts kubadilika, kila unapofungua program fulani icons zote hubadilika na kufanana na icon ya program hiyo. Kwa mfano, ukifungua muziki kwa kutumia window media player, basi shortcut icons zote hubadilika na kuonekana zote ni za media player. Na pale zinapobadilika inakuwa ngumu kuzirudisha katika original appearance yake. Nawaombeni msaada wa namna ya kurekebisha tatizo hili, vinginevyo nafikiria kui-format tena. Laptop bado ni mpya, nimeinunua mwezi November, 2010 ikiwa mpya kabisa.