Nimekuwa naifuatilia sana tamthilia hii ya designated survivor na mengi yanayoonyeshwa yanaakisi changamoto katika kutawala nchi. Rais Kirkman ambaye hakutarajia kuwa Rais anaukwaa urais baada ya uongozi wote wa juu wa taifa la Marekani unapoteketea siku ya hotuba ya State of Union.
Kilichonivuta hadi niandike bandiko hili ni pale Chief of Staff wa Rais alipoamua kujiuluzu baada ya kutuhumiwa kwenye conspiracy ya kuuangusha utawala wa Rais Kirkman. Ingawa FBI waliendesha uchunguzi na kubaini kuwa hakuhusika lakini alisisitiza kuwa anajiona tayari ni liability kwa Rais Kirkman kwani akiendelea kuwa COS maswali yataendelea kuulizwa ilikuwaje mtu wa karibu na Rais kiasi hicho ametuhumiwa kwenye kashfa nzito kama hiyo.
Najua hawa jamaa wanaigiza, lakini wanatufundisha ni jinsi gani sisi tulivyo tofauti na wao. Madaraka ni dhamana tu, siyo kitu binafsi. Heshima ya kazi ni pale ambapo unaifanya kazi bila chembe ya doubt kwa uongozi wa juu au wale unaowaongoza. Ni pale unapoweza kujitathmini mwenyewe kama wewe kwenye utawala ni asset au liability, na kuchukua hatua muafaka.
Nimetupa jiwe gizani, tujifunze kuwajibika kabla ya kuwajibishwa.