Design simple za Nyumba vyumba 2

Asante sana........ila kwa wakati tuliopo........finishing ni ghali kuliko hata nyumba yenyewe.........acha kabisa..........

Ndio hapo sasa. Bila finishing ni pagala si nyumba!
 
Michoro inachapishwa kwa karatasi isiyofutika ikilowa maji miaka 50 je umewahi ona technolojia hii,
 
Inawezekana huwa wanakopi na kuoesti. Maana kama wao mdio wabunifu wenyewe hawawezi kukimbia jukwaa kwakuwa wateja wanakuwa na hamu ya kupata bidhaa waliyotangaza. Mimi nashauri watu wasitangaze bidhaa ambayo hawazalishi wao, hawana ujuzi nayo hawafanyi biashara hiyo kwani inakuwa ni kuwapotezea muda watu. Watu serious ungekuta wametoa contacts zao kama simu, email na anwani.
 
Siyo katagharimu ...itagharimu...vyumba vitatu unaita 'ka'
Yuko sahihi mkuu. Wewe unafikiri sisi tunaohangaika kupata kajumba kama hako ka vymba viwili au vitatu tutakuwa sawa na wenzetu wanaotumia milioni 10 kwa mboga au wale ambo wakiuguliwa wanapewa milioni 80 za pole? Hatuwezi kuwa na majumba kama yale majamaa yanayojiita majoka yenye makengeza. Hivi unafikiri yale yanaweza kuhangaika kuulizia ramani ya kajumba ka vyumba vitatu? Kwao hiyo ni Servanti Kwota yaani nyumba ya mtumishi, mlinzi au hausi boi. We jitu lina lala likiamka mara limepiga bil 1.6 za rada halijakaa sawa zinaingia zingine bil. 16 za Escrow, huku tena linapiga za katiba mpya halafu lenyewe kwa umafia wake ndio linakuwa ndio liandishi likuu. We unafikiri linapiga nyomi ngapi?
 
Mtoa mada hutaki kujibu maswali, akitokea mwingine akaweka diagram, na akaweza kujibu maswali yetu, bac huyo ndo the best
Of course huyo ndio atakuwa best akiongezea na kukupa quantity ya materials (rough figure)
 
Hizi picha wanachukua kwenye internet. Sio wao wanachora. Tafuta mchoraji mwonyeshe kiwanja atakuchorea raman nzuri tu.
Mkuu jenga tabia ya kuamini kile wanachofanya watz wenzako, mpaka ramani huamini kama mtanzania anaweza kuchora? wewe mpe specifications unazotaka uone kama hatokupa kitu roho inataka (kwenye sector hii tuna vijana wanaweza)
 
]Gharama zote ni Milioni 10[/B] kwa ujenzi wa kawaida kisha unahamia nyumba yako. Kwa anayetaka complicated finishing na installations ya vitu vya pesa ndefu basi ni 25-30 milioni.
Mkuu hiyo 10 Million umepiga rangi kila kitu, ceiling board, sakafu, milango (fremu plus top) na madirisha yote yaani umeweka vioo? au ni ule ujenzi wetu ukiezeka na kupiga lipu ukaweka milango na dirishani ukapiga wavu tu?. Otherwise kazi nzuri mkuu
 
Preta nyumba inaongezeka gharama kutokana na finishing inategemea unataka quality gani kwenye finisjing lakini roughly inaweza kusimama 25ml kama finishing zako zitakuwa sio za quality ya hali ya juu sana.
Yes ni kweli kutokana na udogo wake lakini kama ukikafanyia manjonjo kanaweza kakafika mpaka 40 - 45 million kama utazunguushia na fence ya kizushi
 

Umeniumiza mbavu zangu,Mkuu umetisha!
 
Tuonyeshe na Floor Plan tuone ulivyo sema kuwa ni Mtindo wa Kisasa kuryo kuwa na Corridor.
 
Tuonyeshe na Floor Plan tuone ulivyo sema kuwa ni Mtindo wa Kisasa kuryo kuwa na Corridor.

Sasa mkuu hapo si ndio unaenda kujenga, hivi ukishaona image, na floor nini matokeo yake, ..........
 
Preta nyumba inaongezeka gharama kutokana na finishing inategemea unataka quality gani kwenye finisjing lakini roughly inaweza kusimama 25ml kama finishing zako zitakuwa sio za quality ya hali ya juu sana.

Only? Duh! Kama hivyo jamani kila mtu angejenga.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu........mpaka hiyo nyumba ifike kama inavyoonekana hapo kwenye picha.......natakiwa niwe na sh ngapi..........?........

Akishakwambia gharama niambie nitakupa hiyo pesa (mwambie asiweke garama ya vitasa vya milango...hivyo utanunua mwenyewe)
 
Preta nyumba inaongezeka gharama kutokana na finishing inategemea unataka quality gani kwenye finisjing lakini roughly inaweza kusimama 25ml kama finishing zako zitakuwa sio za quality ya hali ya juu sana.

Hiyo nyumba kwa 25m? Nina mashaka kama una idea yeyote na ujenzi
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…