Dereva wa bajaji

Dereva wa bajaji

sara-22

Member
Joined
Apr 6, 2013
Posts
99
Reaction score
14
Mie nilikua na bajaji na dereva alikua ananisumbua sana wakati nilimpa bajaji mpaya alikua ananiletea elfu80 au 50 kwa wiki eti kazi mbaya hamna wateja na ilikua kosa yangu nilimpa bila mkataba.

Sasa natarejia bajaji mpaya mwezi ujao natafuta dereva anaye weza kuniletea laki 250 kwa wiki baada mwaka mmoja na nusu bajaji itakua ya dereva.

Mkataba upo matatizo ya kiofundi kwanzia elfu 1 hadi 15 jua ya dereva ikizidi kwangu kubadilisha mafuta jua yangu mimi hivo dereva atajua maana ya amana maanake atakua mwaminifu sana na bajaji yake.

Mashariti

Awe anakaa kwenye nyumba yakumiliki.

Ndugu wazazi wapo naye serekali ya mtaa wake anamjua na amdhamini.

Atakaye kua tayari PM.
 
Punguza masharti, hilo la kumiliki nyumba mbona gumu.
 
Unajua kwanini madereva hawako wamenifu kama hamna nyumba ya kumiliki itakua rahisi sana kukimbia nacho
 
siyo lazma awe yeye ana nyumba yakumiliki angalao anakaa kwenye nyumba ya kumiliki na ndugu zake
 
hata mkiandikishana mkataba bado hela ipo juu
Cha mhimu,Mkuu punguza bei niku PM.
 
Umeandika ki-Congo, ngumu kukuelewa.

Halfu 250,000 ni kwa wiki au mwezi?

Kama ni kwa wiki inamaana baada ya hicho kipindi cha miezi 18 wewe utakuwa na Tshs 250,000 * 4 *18 = 18,000,000!

Hakuna biashara ya hivyo, sema kama utakubali shs 140,000 mi nije tufanye kazi.
 
Mimi kama mimi nikipunguza 230 mwisho yangu huwa najua bajaji anapata zaidi yangu inategemea na wateja na uzoefu wa dereva kwa wateja hasa hupati atakeye kupa ofa hii ya bajaji
 
Najua hua dereva ataumia sana upende wake mpaka atimize ahadi yake lakini mwishoni atafurahi namsaidia na ananisaisidia
 
siyo lazma awe yeye ana nyumba yakumiliki angalao anakaa kwenye nyumba ya kumiliki na ndugu zake

Unataka utajilikie kwa dereva wewe, yaani kwa wiki laki 250 kwa mwezi ni m.1 kwa mwaka m.12 wakati wewe Bajaj umenunua m.6.5
 
Mimi kama mimi nikipunguza 230 mwisho yangu huwa najua bajaji anapata zaidi yangu inategemea na wateja na uzoefu wa dereva kwa wateja hasa hupati atakeye kupa ofa hii ya bajaji

Kwa nini usiendeshe wewe?
 
Laki 2 unusu kwa wiki kwa bajaji hupati. Labda kama una hamu ya kumfunga tu jela kijana wa watu.
 
wewe 250,000 unataka kijana wa watu ale mawe hapa mjini? muwekee mkataba wa 150,000 kwa miezi 24, . utaona raha yake hakuna cha kelele wala nini kutoka kwa dereva.
 
Kama ndo hivo basi mwisho yangu 200 kwa wiki iko fixed na mtu nitampata tu manake akitimiza dereva mwaka moja na nusu nitanunua tena alafu yeye dereva anaweza kuuza au ampe mtu mwengine afanyie kazi na yeye bado atafaidika kwangu kunfanye kazi kwangu tena na ofa hilo hilo akitaka
 
labda kwa huku tunduma,inawezekana,sababu daladala hazitumiki huku na hisabu ya bajaji kwa siku ni tsh,30000
 
Wee mama ni muhindi?shusha mpaka 170000 nitafanya kazi,
Kama ndo hivo basi mwisho yangu 200 kwa wiki iko fixed na mtu nitampata tu manake akitimiza dereva mwaka moja na nusu nitanunua tena alafu yeye dereva anaweza kuuza au ampe mtu mwengine afanyie kazi na yeye bado atafaidika kwangu kunfanye kazi kwangu tena na ofa hilo hilo akitaka
 
labda kwa huku tunduma,inawezekana,sababu daladala hazitumiki huku na hisabu ya bajaji kwa siku ni tsh,30000

Dereva afikirie vizuri kabla kunipa jibu
kufaidika ni mimi na yeye
hii ndo hali ya dunia hamna kitu inakufika kirahisi binadamu lazma avumilie !! maanake hamjui mimi hiyo hela nimeipataje
 
Mimi kama mimi nikipunguza 230 mwisho yangu huwa najua bajaji anapata zaidi yangu inategemea na wateja na uzoefu wa dereva kwa wateja hasa hupati atakeye kupa ofa hii ya bajaji

Hakuna biashara ya hvyo mdada,,mm ktk mihangaiko yngu nshawah kuendesha na kumilik bajaj, hesabu ya dar ni laki na km unataka mkataba wa baada ya miez 18 amilik dereva ni 140 au 150,,
 
Labda upeleke tunduma,kule hesabu ni 25 mpk 30 kwa cku ila madereva ni waznguaji balaa na chombo inachoka mapema sanaa
 
Back
Top Bottom