Dereva na Rubani

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,817
DEREVA NA RUBANI

Zamani—baada ya kusafiri mwendo mrefu kwa basi, dereva wetu alisimamisha gari kwenye mji mdogo halafu akapotea!

Nusu saa, baada ya kuona kimya, abiria tukaanza kumzonga konda kutaka atueleze kisa cha kutuweka kituoni usiku wa manane bila maelezo. Baada ya kumsonga sana, konda akakubali kutupeleka aliko dereva. Dereva alikuwa amechukua chumba kwenye Gest jirani na kuuchpa usingizi. Nusura tuvunje mlango wa gesti, lakini baada ya kusikia utetezi wa dereva toka ndani, abiria wote tulinywea tukarudi kwenye basi na kulala pia. Dereva alikuwa amezidiwa na usingizi hivyo aliogopa angetumwaga njiani!

Kwa sababu usalama na mwenendo wa basi unamtegemea umakini wa dereva kwa kiwango kikubwa sana, usafiri wa basi Afrika una vituko vingi sana ambavyo ni nadra kuvisikia kwenye usafiri wa ndege, meli au hata treni. Tofauti na rubani, dereva wa basi, hasa hapa Tanzania, kuvunja sheria za barabarani ni jambo la kawaida. Dereva aliyeamka na hasira baada ya kugombana na mkewe/mumewe ataendesha gari kwa kisirani na kuwarusha abiria kwenye mashimo utadhani ndio waliomkosea. Ndio maana kwenye basi huwekwa namba ya simu—ikitokea dereva akaanza kupandisha maruhani, abiria mtoe taarifa.

Rubani huanza safari kwa saa, dakika na sekunde maalumu; dereva wa basi haondoi gari mpaka ijae. Safari ya ndege toka Marekani mpaka Dar es Salaam, inajulikana itachukua saa na dakika ngapi; safari ya basi kutoka Dar kwenda Moro haijulikani itachukua muda gani—inategemea na foleni na manjonjo ya dereva wa siku hiyo. Kabla ya kuruka, kila rubani lazima akague na kujaza kwenye daftari orodha ndefu ya tahadhali za kiusalama; dereva wa basi akisharukia na kubamiza mlango safari huwa imeanza! Wakati ndege yenye hitilafu ndogo tu hairuhusiwi kabisa kuruka, yapo mabasi mabovu mengine yasiyo na breki yanayoendelea kusanya abiria kama kawaida!

Rubani hata awe mzoefu namna gani, kuna mahala atalazimika kuongozwa na wengine; haruhusiwi kuendesha zaidi saa 9 mfululizo na ndege ya abiria hairuki bila rubani wawili au watatu! Sheria zote hizi zimetungwa ili kupunguza kabisa uwezekano wa makosa. Ndiyo maana hata ikitoea akili zikamfyatuka rubani njiani, bado ndege inaweza akatua salama. Dereva wa basi zikimfyatuka njiani, ndio mmekwisha!

Zingekuwa ni taasisi, tungeweza kusema usafiri wa ndege ni taasisi imara kutokana na vipengele yake vingi vinavyoshirikiana kuhakikisha kuwa hapatokei kosa. Usafiri wa basi ni taasisi dhaifu sana maana dhamana yote ya usalama na mwenendo wake vimewekwa mikononi mwa mtu mmoja tu.

Kuna mtu mmoja alipata kupendekeza kuwa, ili nchi za Afrika ziendelee, basi itabidi ziwe na taasisi imara kuliko kutegemea madereva mahiri wanaoweza kusimamisha basi hata kama halina breki. Haishangazi, katika nchi za Afrika, kila anapokuja dereva tofauti mwendo wa basi hubadilika pia. Busara ya kutegemea taasisi imara kuliko kutegemea watu inatokana na ukweli kuwa, ni vigumu kuwategemea watu kwa asilimia mia moja! Watu huchoka, hubadilika; lakini kubwa zaidi, watu hufa!

Kwa mfano, baada ya kifo cha Rais Magufuli, njozi ya Tanzania ya viwanda inaweza kuwa ndiyo imefikia mwisho endapo Mrithi wake, Rais Samia, atachagua kuwa na vipaumbele vingine. Ni jambo la kutia moyo kwamba, Rais Samia ameshaahidi kuwa ataeendeleza njozi ya Magufuli tena kwa kasi ileile, lakini litakuwa jambo jema zaidi kama atajenga mfumo imara, wenye vikorombwezo kama vya ndege kiasi kwamba, rushwa kama ilivyoadimika wakati wa Magugufuli, iwe nadra atakapoondoka yeye na hata itakapotokea tukapata dereva anayesinzia njiani!

Mwanafasihi

Hakuna kitu ambacho wana ccm wengi wanakiogopa kama Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi!! Wanafahamu fika wakiruhusu mambo hayo mawili kufanyika, basi ndiyo kiama chao kitakuwa kimewadia.
... wataendelea kuogopa hadi lini? Wataendelea kutawala kijanjajanja hadi lini?
 
Back
Top Bottom