Dereva mzuri husikiliza abiria wake

Abiria gani anapanda malori?au wale wanaoenda minadani?
 
Bas sasa iv askari haina haja kuuliza abira mwendo wa dereva barabarani.
 
Silence can be a golden answer
 
Kwanini unadhani alitolea mfano was lorry si bus,?kawaida tumezoea tunasafiri na bus,kuhusu lorry ni mizigo,na uhalisia wa lorry hata kimuundo linanafasi ya dereva,konda(sio makonda) na walau nafasi ya MTU mmoja.Huyu dereva alipotoa mfano wa lorry alikuwa na mana pana sana,angeongelea bus tungekuwa na maswali mengi.Tumedandia wenyewe lorry wakati buss lipo,wacha tupelekwe kama mizigo
 
Kwahiyo alimaanisha sisi ni mizigo.
 

Udereva ni taaluma, kitendo cha kuendesha chombo cha usafiri peke yake hakitoshi kuitwa udereva kwa ulimwengu wa sasa.

Dereva kama kiongozi wa chombo anapaswa kuhakikisha chombo anachokiongoza kiko timilifu kwa safari na kinasafiri salama. Kila kilichomo ndani ya gari (wakiwamo abiria) wapo chini ya uangalizi wa dereva. Kwa mantiki hiyo dereva anapaswa kuhakikisha utulivu wa abiria, mizigo imefungwa vizuri, na kila inapojitokeza kasoro yoyote ni lazima dereva achukue hatua kuhakikisha safari inaendelea katika namna salama na inayokubalika.
Kuendelea kuwaendesha abiria wanaofanya fujo na vurugu eti tu kwa sababu wewe kazi yako ni kuendesha chombo tu si sawa na ni mapungufu makubwa kwa dereva mhusika.
Vinginevyo tutashuhudia dereva akiendesha gari wakati huku nyuma abiria mmoja ameshika bunduki anaua wenzake, mwingine anawasha moto kwenye gari achome siti, mwingine anafungua TV akaiuze akishuka au abiria wengine wakiwa wanabembea madirishani nk. akiamini hayo hayamhusu.

Katika mfano wako wa fujo za abiria ni dhahiri unaakisi mapungufu katika udereva wa dereva wetu. Kama anaona abiria "wamemshinda" ni bora akaomba usaidizi kwa dereva mwingine maana ameshindwa kuongoza safari vile inavyotakikana. Hatujafikia hatua ya kuendeshwa "bora liende"

Dereva mweledi ni lazima apate mrejesho toka kwa abiria wake namna anavyowaendesha ama kwa kuwaangalia comfortability yao kwenye chombo, mood, maongezi au malalamiko kama yapo. Dereva anayapima hayo na yanamsaidia kuamua ni namna gani aiongoze safari.

Nikutakie Safari njema.
 
Na usipo wasikiliza abiria wako basi umekunywa viroba
 
Mwenye jukumu la kuongea na abiria ni kondakta sio dereva la si hivyo gari litapata ajari mana kila mtu amwongeleshe dereva amsikilize huku aendeshe gari wapi na wapi.

We ongea na konda ujumbe utafika.
 
Upo sawa ila sio abiria akufundishe jinsi ya kukata kona. Hiyo haikubaliki!
 
YUKO KWENYE MWENDO KASI
 
 
Mwenye jukumu la kuongea na abiria ni kondakta sio dereva la si hivyo gari litapata ajari mana kila mtu amwongeleshe dereva amsikilize huku aendeshe gari wapi na wapi.

We ongea na konda ujumbe utafika.

Nadhani ni "kuwasikiliza" sio "kuongea nao".
Dereva anapaswa kusikiliza na kupima maoni ya abiria, kama yana msingi sio vibaya kuyafanyia kazi. Sio sawa sana kuazimia kutosikiliza abiria kwa lolote, si sawa.
 
Kila abilia akitaka ufuate anacho sema what do yu expect....sisi kama abilia tumechagua wawakilishi wetu...badala ya kutusemea matatizo yetu wao wanasemea vyama vyao we unadhan dereva afanyeje..pachika magia twende atae ona mwendo ni kasi apitie dirishan ila tukifika kwenye kituo kingine atapanda mwingine over.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…