DEREVA KIPOFU.

DEREVA KIPOFU.

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
mjaza.jpg


DEREVA KIPOFU.

Nina maneno machache, wingi wa vitendawili,
Twende sote sikuache, tuliza yako akili,
Kama usiku na uche, ulione jambo hili,
Kibogoyo ala fupa, mwenye meno lamshinda.

Katika kupitapita, nikakutana na basi,
Hovyo kona linakata, na mwendo wake wa kasi,
Watu wote wanajuta, wamejawa wasiwasi,
La ajabu wana mato, dereva wao kipofu.

Nilimuokota paka, kichanga hana wazazi,
Namlisha atosheka, nyama maziwa mchuzi,
Ikakatika miaka, ndipo nikaja maizi,
Kumbe si paka ni chui, roho yangu i' shakani.

Maajabu ya dunia, mahala nimeyakuta,
Mtu tawi kakalia, ndilo hilo alikata,
Na alivyo dhamiria, kuna pato anapata,
Hajui tamaa mbele, mauti hufata nyuma.

Yataka uwe makini, kuelewa nilosema,
Bure tabaki njiani, na mawazo chungu nzima,
Sijue ufanye nini, na jua lenda kuzama,
Mja fahamu majazi, mwenzi wake taawili.

03/11/2016

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/Whats app 0622845394 Morogoro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom