GE2025 Deodatus Balile: Dira ya 2050 Siyo ya CCM

GE2025 Deodatus Balile: Dira ya 2050 Siyo ya CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile, amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa nchini vyenye kushiriki uchaguzi mkuu kuwa na ilani za uchaguzi zenye kuakisi malengo na mipango iliyopo kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025/50, ili kuwa na mtazamo wa pamoja wa ‘Tanzania tuitakayo kufikia 2050’.

Balile amebainisha hayo Jumanne Julai 08, 2025 Jijini Dar Es Salaam, wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo dhidi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, mkutano wenye lengo la kufahamisha wananchi kuhusu mchakato wa Maandalizi ya Dira hiyo.

"Niseme sisi tumejipanga kutangaza habari zinazohusiana na Dira ya Taifa ya mwaka 2025/50 na dira hii si kwaajili ya Chama Cha Mapinduzi pekee maana baadhi ya watu wanaweza wakachanganya kuwa hii Dira ni ya CCM. Vyama vyote vya siasa vinavyopenda kuandika ilani zao inapaswa kuakisi Dira hii na wakifanya hivyo sisi hatutasita kuandika habari zao." Amesema Balile, ambaye pia ni Rais wa Jukwaa la wahariri Afrika Mashariki.

Akisisitiza utayari wa wanahabari katika kuufahamisha umma kuhusu Dira 2050, Balile pia amesisitiza umuhimu wa Idara ya Habari ya Ofisi ya Tume ya Taifa ya Mipango kuwa na bajeti ya kutosha, itakayowezesha utoaji wa elimu na kukuza ufahamu wa wananchi kuhusu Dira 2050, ili kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa kutosha wa ‘Tanzania tuitakayo kufikia mwaka 2050’.
 
Leo JKamenda mbali na kumpigia Maza kampeni. Kwa kweli CCM wanaiona hii nchi ni mali yao binafsi.

Polepole usituangushe kesho. Ni thahili kuwa yanayofanyika kwa sasa ni kwa faida ya KIKUNDI.
 
Back
Top Bottom