DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Makambako, Mkoa wa Njombe, Deo Sanga maarufu kama Jah People, amemtupia lawama aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, akisema kauli zake za kuipinga serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinachochewa na mabadiliko ya mazingira ya kisiasa.
Akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam Jumamosi, Sanga amesema Polepole aliwahi kudai kuwa miradi iliyoanzishwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli isingeendelezwa na Rais wa sasa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye wakati huo alikuwa Makamu wa Rais.
"Polepole alikuwa akituambia kuwa miradi hasa ile iliyoachwa na Hayati Magufuli haitokamilika wala kuendelezwa na Rais Samia. Sasa baada ya miradi hii kwenda vizuri ni dhahiri jambo hili limemchanganya," amesema Sanga.
Aidha, ameeleza kuwa ukaribu wa Polepole na Rais Magufuli wakati wa uhai wake ulimfanya ajione sehemu ya Ikulu, hali ambayo imekuwa ikimpa mtazamo tofauti katika awamu ya sasa.
"Kikubwa nilichokiona ni pale ambapo Marehemu Magufuli alikuwa karibu naye sana kiasi kwamba Polepole aliweza kwenda Ikulu kama mtu anayekwenda kunywa chai au kula chakula cha mchana. Yaani pale Ikulu palikuwa kama kwake," ameongeza.
Sanga amesisitiza kuwa pamoja na kauli za Polepole, miradi ya maendeleo imeendelea kutekelezwa kwa kasi chini ya uongozi wa Rais Samia, jambo linaloonesha kuwa serikali iko makini katika kuwaletea wananchi maendeleo.