Denti wa Kapuya atinga Marekani!!

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
WAKATI polisi wakiendelea kukalia jalada la Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kubaka na kutishia kuua binti wa miaka 16, sasa suala hilo limefikishwa katika ubalozi wa Marekani. Mbali na hatua hiyo, binti huyo pia amelifikisha jambo hilo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amiri Manento akitaka msaada zaidi.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumatano, binti huyo na dada yake, walisema wameamua kuomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani kwa madai ya kuhofia usalama wao kutokana na vitisho wanavyozidi kuvipata kila kukicha.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, binti huyo alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DDP), hawataki kulifikisha suala lao mahakamani wanakoamini haki yao itapatikana.
Alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakisikia kuwa Marekani ni vinara wa utawala bora na demokrasia, hivyo aliamua kwenda ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini wasaidiwe.
"Kapuya inaonekana anatisha au analindwa sana, lakini sisi tutahakikisha haki yetu tunaipata kwa njia zozote," alisema.
Aliongeza kusema kuwa serikali imeshindwa kuwapa hifadhi kutokana na vitisho wanavyovipata, na wanahofia kuuawa hali inayowafanya wawe waangalifu zaidi.
Tanzania Daima Jumatano limedokezwa kuwa mabinti hao walikwenda ubalozi wa Uingereza kuomba hifadhi hiyo ambako walielekezwa kuwa wakienda katika ubalozi wa Marekani shida yao itatatuliwa.

Source: Tanzania Daima
 
Haji Salum

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
1,022
0
Hii ngoma bado mbichi! Hii serikali ya CCM ndio kwanza inaendelea kujichafua! Hii kitu ikinaswa na CNN ni doa kubwa sana kwa Tanzania!

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
Wanajitambua ukapu sio wakuletewa mzaha we usikie waukomeshe kwa kizazi hiki na kijacho USA Haihongeki na Manento ni muda kuonyesha una meno kwenye sakata hili tusije kuwa na CHAMA CHA MAKAPUYaa kuwadhofisha na kuwazalilisha wanafunzi wa kike.
 
mahuyange

Member
Nov 25, 2013
26
0
Hoja yao haina mashiko nchi yetu inaviongozi makini sana wanaojari usawa na maana ya she ria msumeno bhaumwogopi kapuya.
 
kibugumo

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
1,420
1,500
Asichunguzwe kapuya peke yake,hii nchi imeoza sana kwa kashfa za ngono na udhalilishaji,mara wabunge mara mawaziri,wakurugenzi nk,hakika taifa hili hakuna tunachojua zaidi ya zinaa.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,547
2,000
Kama ni kweli, nampa HONGERA zake huyo binti. Mungu amsaidie aweze kukiweka kilio chake angani watu woote wamsemee. CCM inayosema ni sikivu, naona masikio yao yameingia kiwi, wanahitaji mtaalam wa haki za wanadam kutoka USA awafikiche masikio huenda wakasikia.
Hon. Kapuya, are yu OK? Nakusalimia tu mzee wa Mitoto ya sembe
 
bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
WAKATI polisi wakiendelea kukalia jalada la Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kubaka na kutishia kuua binti wa miaka 16, sasa suala hilo limefikishwa katika ubalozi wa Marekani. Mbali na hatua hiyo, binti huyo pia amelifikisha jambo hilo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amiri Manento akitaka msaada zaidi.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumatano, binti huyo na dada yake, walisema wameamua kuomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani kwa madai ya kuhofia usalama wao kutokana na vitisho wanavyozidi kuvipata kila kukicha.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, binti huyo alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DDP), hawataki kulifikisha suala lao mahakamani wanakoamini haki yao itapatikana.
Alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakisikia kuwa Marekani ni vinara wa utawala bora na demokrasia, hivyo aliamua kwenda ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini wasaidiwe.
“Kapuya inaonekana anatisha au analindwa sana, lakini sisi tutahakikisha haki yetu tunaipata kwa njia zozote,” alisema.
Aliongeza kusema kuwa serikali imeshindwa kuwapa hifadhi kutokana na vitisho wanavyovipata, na wanahofia kuuawa hali inayowafanya wawe waangalifu zaidi.
Tanzania Daima Jumatano limedokezwa kuwa mabinti hao walikwenda ubalozi wa Uingereza kuomba hifadhi hiyo ambako walielekezwa kuwa wakienda katika ubalozi wa Marekani shida yao itatatuliwa.

Source: Tanzania Daima

Ahsante Tanzania Daima na chadema kwa ukuwadi...
 
manyimbo

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
629
500
mliokaribu na US embassy msisite kutu-update kwa kadri mambo yatakavyoendelea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom