Denti wa chuo kikuu atekwa, na kuwawa

Denti wa chuo kikuu atekwa, na kuwawa

Gumzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Posts
211
Reaction score
9
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King’unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
“Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
“Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
GUMZO LA JIJI

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King'unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
"Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu," kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
"Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao," kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
GUMZO LA JIJI

Hivi IFM ni Chuo Kikuu?
 
uzembe wa kwanza
mtu hajitambui wanampeleka polisi?
halafu aga khan alikuwa na pesa au insuarance card?
pengine walikataa kwa kuwa hawakuona uwezekano wa kulipwa
tatu muhimbili inajulikana kwa uzembe
 
Sasa hivi kila chuo kimekuwa chuo kikuu!
Binti kama alitekwa kwa hila za watu roho yake ipumzike kwa amani
Lakini kama ilikuwa ni tabia za wadada kuwachuna wakaka iwefundisho kwa wale wadada wanaopenda vya bure.
 
Wanafunzi wote wanakuwa wanalipa insurance money (nadhani laki moja hivi), so matibabu isingekuwa tatizo. Na aghakhan hawakatai emergencies, watafanya huduma ya kwanza na kupeleka mgonjwa safely to another hospital
uzembe wa kwanza
mtu hajitambui wanampeleka polisi?
halafu aga khan alikuwa na pesa au insuarance card?
pengine walikataa kwa kuwa hawakuona uwezekano wa kulipwa
tatu muhimbili inajulikana kwa uzembe
 
baadhi ya vyuo vimepandishwa hadhi na kuwa vyuo vikuu vishiriki
e.g I.F.M
C.B.E
D.I.T
ustawi wa jamii e.t.c

Ni vyuo vikuu vishiriki vya chuo gani hapa Tanzania? unaelewa nini maana ya chuo kikuu kishiriki?
 
habari hii niliiona michuzi wiki jana..inasikitisha kweli, binadamu tumezidi ukatili..Inahitaji uangalifu kweli!!
 
baadhi ya vyuo vimepandishwa hadhi na kuwa vyuo vikuu vishiriki
e.g I.F.M
C.B.E
D.I.T
ustawi wa jamii e.t.c

Mkuu, hii taarifa uliyoleta inabidi uifafanue tuelewe.
Awali ya yote nina mashaka kama unaelewa maana ya Chuo Kikuu Kishiriki!
Ungetusaidia sana kama ungedokeza Vyuo tajwa hapo juu vimekuwa chini ya Vyuo Vikuu gani.
Kwa kifupi,kwa kawaida,ili Chuo kiweze kuwa chuo Kkuu Kishiriki ni sharti chuo husika kiwe chini ya Chuo Kikuu fulani ambacho ni kamili.
Kadiri ninavyojua,IFM ni moja ya Taasisi za Elimu ya Juu hapa nchini.
 
wanafunzi jaman hasa wa kike muwe na woga mnapotolewa out na mtu usiyemfahamu vizuri
 
Haya matokeo ya utekeaji mbona ynapamba moto kwa kasi sana sasa hivi.

Kuna umuhimu mkubwa wa wa mambo ya ndani kujipanga kwani awmeshindwa kazi.
Haya mambo yamekuwa yakijirudia sana.
 
Back
Top Bottom