Dennis Mpaganze katika hili I beg to differ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dennis Mpaganze katika hili I beg to differ!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nsami, Apr 8, 2012.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu salute!

  Jana katika kipindi cha tuongee asubuhi kilichorushwa na Star TV (Jicho letu ndani ya habari) ndugu Dennis Mpaganze (Sijui kama nimelispell vizuri jina lako) ulionekana kukereka sana na baadhi ya vichwa vya habari katika baadhi ya magazeti yaliyoripoti matokeo ya uchaguzi mdogo wa Arumeru Masharki.

  Vichwa vya habari ulivyofanyia reference ni vile vilivyosema "CC CHALI" na "CHADEMA HAIKAMATIKI" madai yako yakiwa magazeti hayo yameandikwa kishabiki kuwa yameshabikia CHADEMA na ukaenda mbali zaidi kusema yanatuchonganisha ati mwana CCM hawezi kununua gazeti kama hili!

  Pamoja na kujitahidi kuwa mojawapo ya wasikilizaji wako makini sikukuelewa katiaka hili kwa misingi ifuatayo

  1.Kwanza ulishindwa kutoa kichwa cha habari mbadala, kwamba kama mwanataaluma ya habari jiweke mwenyewe kwenye chumba cha habari na unataka kuripoti jambo kama hili utaandika nini?

  2.Uchunguzi wako haukuwa wa kitaalamu, kwa kuwa kuna chaguzi nyingi tu zimeshafanyika hivi karibuni kama kule igunga na uzini. Nilitegemea kama msomi utuletee data kwa ke-refer chaguzi hizo jinsi zilivyoripotiwa . Kwa mfano kwa gazeti ambalo lingekuwa limeandika katika uchaguzi wa Igunga labda "CHADEMA imetereza" CHADEMA iliposhindwa siku chache baadae likaandika "CCM CHALI" ungenishawishi kuona umechukua hatua zaidi ya mtu aliyejikuta tu studio na kuulizwa swali la papo kwa papo! Lakini kama gazeti hilo hilo jana liliandika "CCM kidedea igunga" sipati shida yoyote gazeti hilo hilo kuandika "CCM CHALI" au "CHADEMA haikamatiki" Arumeru.

  3.Sikuona ukiwa much concerned kuona vichwa vya habari kama "SIMBA kidedea" ama "YANGA mwendo mdundo" pindi matokeo kati ya mechi za simba na yanga yanaporipotiwa, hivyo unanipa nafasi ya kuhisi kuwa nikikuona studio nisitarajie chochote kipya cha kutofautiana na wenzako wengi tu kama Dr Benson Bana, TBC1, radio UHURU nk.

  Ushauri
  Ni jambo la busara sana na litaheshimu taaluma kama usiporuhusu hisia zako wakati wa ukitoa mchango wako wa kitaaluma kwa vyombo vya habari ili kuinua taaluma ya habari!

  Lakini pia nitakuchukulia mzalendo sana ukijitokeza na kulalamikia vyombo vya habari kwa kutoipamba CCM hata kama imeshindwa kwenye uchaguzi, ila usijifiche kwenye mwamvuli wa taaluma. Hapo tunakuhitaji kama Kada wa chama au hata Green Guard!

  Kama nimekuudhi naomba ujue ya kwamba Sio lengo langu kukuudhi na wala sio tabia yangu! Ni uhuru wa mawazo kama uliyoyatoa Star TV!
   
Loading...