Deni linaweza kukufunga ukishindwa kulipa

Apr 26, 2022
64
100
Watu wengi wanasema deni halimfungi mtu, lakini sio kweli. Leo nitafafanua Sheria ya Mwenendo wa Madai (the Civil Procedure Code [CAP. 33] kwa kifupi tunaiita “CPC”) kuhusu mazingira ambapo kutolipa deni kunaweza kufanya ukafungwa.

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke, Advocate Candidate.
zakariamaseke@gmail.com
(0754575246 WhatsApp).

Iko hivi, ukishinda kesi Mahakamani na yule unayemdai akaambiwa akulipe, unatakiwa kufanya maombi (application) Mahakamani, kuomba utekelezaji wa hiyo hukumu (execution) wengine wanaita kukazia hukumu.

Sasa mojawapo ya njia ya kutekeleza hukumu ni KUMKAMATA NA KUMFUNGA MDAIWA (ARREST AND DETENTION AS A CIVIL PRISONER).

Njia hii inatumika pale ambapo mdaiwa ana uwezo wa kulipa deni ila anakataa kulipa kwa makusudi. Na mara nyingj inatumika mwishoni kabisa njia zingine zote zikishindikana.

Sasa, kama umeshinda kesi na mtu hataki kukulipa, utapeleka maombi (application) Mahakamani kuomba kutekeleza hukumu kwa kumkamata na kumuweka jela mdaiwa kama mfungwa wa madai. Utaratibu huu upo kwenye Sheria vifungu vya 44, 42(c) na Order XXI rule 35 ya CPC.

VIGEZO NA MASHARTI

(i) Kabla ya kumkamata na kumfunga mdaiwa, sheria inasema inatakiwa Mahakama itoe notice (taarifa) kwa mdaiwa kumuita aje aieleze Mahakama anafikri kwa nini asikamatwe na kufungwa jela? Kama akishindwa kuja utaomba Mahakama itoe hati ya kumkamata (arrest warrant) na sheria imetaja muda gani anatakiwa kukamatwa. Hatakiwi kukamatwa usiku (kabla hakujakucha au baada ya jua kuzama) na hutakiwi kuvunja mlango labda kama mdaiwa yumo ndani na hataki kufungua kwa makusudi. Section 44(1)(a) & (b) ya CPC.

Kama mdaiwa baada ya kupewa notice atakuja lakini akashindwa kutoa sababu za msingi kuiridhisha Mahakama, basi Mahakama itaamuru aende jela.

(ii) Pili, huyo mtu unayemdai lazima awe na uwezo wa kulipa lakini hataki kwa makusudi. Huu utaratibu mara nyingi unatumika dhidi ya watu ambao wako vizuri, wana hela ila wana viburi (ni watata), ambao wana uwezo wa kukulipa ila hawataki kutii sheria mpaka walazimishwe. Ila ukiwa maskini, hauna kitu, sheria inasema utaachiwa huru. Order XXI rule 39(1) ya CPC.

(iii) Sharti lingine, ni lazima wewe mdai uwe na uwezo wa kulipa subsistence allowance (posho) ambayo itatumika kumlisha huyo mtu wakati anatumikia kifungo gerezani. Na hiyo hela unailipa mapema kabla ya tarehe moja ya kila mwezi, ikifika hatua ukashindwa kulipa anaachiwa huru. Section 46(1)(iv) na Order XXI rule 38 ya CPC.

Pia, hiyo hela unayolipa kumlisha akiwa gerezani, itajumlishwa kwenye gharama za kesi na litakuwa deni, lakini haitahesabika wakati wa kutekeleza hukumu, isije mwisho akashindwa tena kulipa ukampeleka jela tena. Hiyo itabaki deni tu ambalo atakuja kukulipa kama gharama ya kesi lakini hairuhusiwi kumkamata tena kwa madai ya hela uliyotumia kumlisha. Order XXI rule 38(5).

Kabla ya kumfunga mdaiwa, taarifa itapelekwa jela ili wajue status (hadhi) ya huyo mtu ili wakwambie vitu gani muhimu kuwa navyo. Kwa sababu mfungwa wa madai hali chakula kama cha wafungwa wengine waliofungwa kwa makosa ya jinai kama vile wizi, ubakaji n.k., wewe uliyeomba mtu afungwe kama mfungwa wa madai unawajibika kumlisha vizuri kama ambavyo huwa anakula akiwa nyumbani kwake.

Akikwambia nyumbani kwake huwa anasoma gazeti kila siku itabidi umnunulie. Kama hali maharage anakula samaki tu, itabidi umnunulie. Hiyo ndio sababu jela wanataka wajue hadhi ya maisha ya huyo mtu ili wakwambie mnyumbuliko / breakdown ya hizo gharama ulipe.

Kwa sababu lengo la aina hii ya utekelezaji wa hukumu (kwa kumfunga mdaiwa) sio adhabu, isipokuwa ni kumlazimisha mdaiwa alipe. Kwa hiyo huwezi kumpeleka jela akaishi maishi ya mateso.

Muda wa kufungwa itategemeana, ila mdaiwa anaweza kufungwa hadi miezi sita. Pia mdai unaweza kuomba mdaiwa aachiwe huru ila kuachiwa huru haimaanishi deni limekufa, na kuna uwezekano wa kukamatwa tena.

Kama kesi ni madai ya hela, mdaiwa akilipa kiasi anachodaiwa na gharama za aliyeenda kumkamata (arresting officer), ataachiwa huru muda huo huo hata kama amekaa siku moja tu gerezani.
Section 46(1)(i) ya CPC.

Kwa uelewa zaidi kuhusu mfungwa wa madai, pitia section 44 - 47 ya CPC na Order XXI rule 35 - 39.

-----MWISHO----

Angalizo: Position au maelezo haya ni kwa mujibu wa sheria zilizokuwa zinatumika mpaka siku ya kupost hili andiko. Hivyo unaposoma leo haya maelezo, soma na sheria zilizopo sasa hivi, ili ujue utaratibu bado ni ule ule au la! Sheria zinarekebishwa na mpya zinatungwa kila siku.

Pia natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili. Unaruhusiwa tu kusambaza lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.

Disclaimer: Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. Ikiwa utaamua kufungua kesi kwa kufata haya maelezo na ukapata hasara, mwandishi wa maelezo haya hatawajibika kwa vyovyote vile. Kama unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mawakili.

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke,
(0754575246 - WhatsApp).

Dah Zakaria Maseke yaani jitu nalidai bado nililishe vizuri huko lupango alafu eti niamini ipo siku litalipa

Acha deni langu abaki nalo tu siyawezi ya sheria hii
 
Mkubwa! Ukikamatwa kwa Criminal case ikaamliwa ulipe na kifungo cha nje, kifungo cha nje ukatekeleza ila kulipa kazi hapo inakuwaje ukidakwa?
 
Back
Top Bottom