Deni la Ugiriki na Funzo kwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Deni la Ugiriki na Funzo kwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Jun 17, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ugiriki ni moja ya nchi zilizoendelea duniani ikikisiwa kuwa ni 27th in the world kwa ukubwa wa kiuchumi duniani (World Bank, 2009). Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Ugiriki ilikuwa ni moja ya nchi zilizoendelea ikiwa na kiwango cha juu kulinganisha na baadhi ya nchi nyengine za Ulaya ikikisiwa ni ya 22 duniani kwa kuwa na ubora wa maisha. Uchumi wa Ugiriki umetawaliwa zaidi na sekta ya serikali inayokisiwa kuwa na asilimia 40 ya total GDP, 78% inashikiliwa na sekta ya huduma, 17 sekta ya viwanda na 4% sekta ya kilimo (Wikipedia).

  Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kabla ya kuanza kwa mtikisiko wa sekta ya benki duniani mwaka 2008 Ugiriki ilikuwa ikikopa kwa kiwango kikubwa sana kuendesha serikali hasa kwenye budget na shughuli zenginezo za kiserikali. Hilo lilitokana na kushuka kwa mapato ya ugiriki na kuporomoka kwa mauzo ya nje ya nchi (IMF World Economic Outlook Report, 2009). Kutokana na hayo serikali ilijikuta ikipungukiwa na mapato na kulazimika kukopa kwa kiwango kikubwa kufidia mapungufu ya mapato. Inakisiwa baina ya mwaka 2001 hadi 2008 Ugiriki walikuwa na budget deficit of 5% (punguzo la mapato) kila mwaka (IMF World Economic Outlook Report, 2009).

  Punguzo la mauzo ya nje lilikuwa 9% kila mwaka ukilinganisha na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi (current account deficit) (IMF World Economic Outlook, 2009). Ilipofika mwaka 2009 ufinyu wa bajeti ulifikia kiwango cha zaidi ya asilimia 14 ya GDP (Nielsen et.al., 2010). Sababu kubwa za kukua kwa ufinyu wa bajeti kulitokana na kuongezeka kwa matumizi makubwa ya serikali (Economist, Feb 4 2010).

  Ili kufidia ufinyu wa bajeti na kuwezesha uendeshaji wa serikali, Ugiriki walianza kuazima pesa katika masoko huria ya pesa na mitaji kimataifa (International capital Market). Hadi kufikia mwaka 2009 Ugiriki ilikupa kufikia 115% ya uchumi wa nchi (GDP) (Economics Intelligent Unit, 2010). Mwaka 2008 Ugiriki ilikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi ambapo ilichangia kushuka kwa pato la nchi kwa kiwango kikubwa. Makusanyo ya kodi, kushuka kwa biashara ya utalii na huduma zenginezo vilichangia kwa kiwango kikubwa kuiweka ugiriki katika hali mbaya ya kiuchumi (Jackson J., Congress Report).Vile vile Uchumi wa Ugiriki uligemea zaidi mikopo katika masoko ya nje. Serikali ya kisoschalisti ya ugiriki ilikosa mawazo ya jinsi ya kujikwamua kutokana na uchumi tegemezi wa kukopa.

  Kwa kukumalizia yepi yalikuwa matatizo makuu ya ugiriki kufikia hapa walipo nitayaelezea kwa ufupi:-

  a. Matumizi makubwa ya Serikali:

  Inasemekana kati ya mwaka 2001 hadi 2007 uchumi wa Ugiriki ulikuwa kati ya asilimia 4 mpaka 4.5 (World Economic Outlook, 2009). Hata hivyo matumizi ya serikali yaliongezeka kwa asilimia 87 kulinganisha na mapato yaliyokuwa kwa 31% tu (Greece Minister of Finance, January 2010). Hili lilisababishwa na sababu mbali mbali kama usimamizi mbovu wa mapato na matumizi ya pesa za umma, gharama kubwa za huduma ya afya, na ukwepaji kodi (Greece Ministry of Finance, 2010).

  b. Ukuaji wa ushindani wa kimataifa.

  Sekta ya uzalishaji imeporomoka kwa kiwango kikubwa kutokana na kuongezeka kwa ushindani wa kimataifa. Hilo lilichangia kukua kwa mishahara ya wafanyakazi na kuporomoka kwa uzalishaji wa ndani ya nchi (OECD Survey, 2009). Ugiriki ilifanya hilo ili ikubalike katika jumuiya ya kimataifa na hivyo kuathiri viwanda vya ndani ya nchi. Utafiti unaonyesha biashara ya nje ya nchi ilikuwa nusu ya biashara zinazotoka nje ya nchi kwenda Ugiriki (OECD Survey, 2009).

  c. Urahisi wa upatikanaji wa mikopo na Sarafu yenye nguvu:

  Utafiti unaonyesha kuwa kujiunga kwa Nchi za umoja wa ulaya kulichangiwa kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa ufinyu wa bajeti (OECD Survey, 2009). Kujiunga kwa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) kulidumaza mauzo ya nje (export) na kuongeza mauzo ya ndani kwakuwa sarafu ya ugiriki ilipanda thamani na kufanya mauzo ya nje kuwa bei ya juu. Hilo lilichangiwa kwakuwa Umoja wa nchi za Ulaya ulijumuisha nchi zenye uchumi mkubwa kama Ujerumani, na Ufaransa (Nielsen et.al.,Congress Report 2010). Urahisi wa kupata mikopo nao ulichangiwa na kukuwa kwa kasi na utegemezi wa mikopo kuendesha serikali ya ugiriki.

  d. Sheria za Umoja wa Ulaya:

  Hili nalo linasemekana kuwa na mchango mkubwa kukua kwa ufinyu wa bajeti ya nchi.


  Mtazamo wa Tanzania:

  Kuna masuala ya kujifunza kwa nchi yetu inayoanza kuendelea na ni vema yatiliwe maanani. Hii ni kwasababu serikali yetu imeanza mchakato wa kukopa katika masoko ya pesa na inasemekana mwaka huu inataka kutangaza Eurobond of 500 Bn katika soko la fedha la kimataifa (East Africa, June 2011). Fedha hizo zinasemekana ni kusaidia kunyanyua uchumi na shughuli za maendeleo. Hata hivyo according to Zitto Kabwe speech, 15th June, 2011 hesabu zinaonyesha deni la taifa kukuwa kwa 38%, deni la taifa limefikia $11.5 Billion hadi kufikia December , 2010. Pia matumizi mabaya ya fedha za serikali yanaonyesha yanakisiwa kuwa ni 25% ya bajeti yote ya serikali (CAG Report, 2010). Hili linakisiwa kuwa ni sawa na Shs Trilioni 9.5. Hivyo wakati tunazidi kukopa pia tunaongeza ukubwa wa matumizi ya serikali na vile vile tunashindwa kusimamia vizuri pesa za umma. Hizo ni sababu sawia na sababu walizokumbana nazo Ugiriki.

  EAC Community, Hali ya uchumi wetu zinaonyesha Tanzania uchumi wake unakuwa kwa kiwango cha asilimia 6.5 , Kenya ni 4.98 % na Uganda ni 5.18%, Rwanda 6.5% (IMF, 2010). Pia sarafu na cost of living inaonyesha kuwa Kenya sarafu yao ni yenye nguvu kuliko sarafu nyengine ya Africa Mashariki. Muungano wa Africa Mashariki unaweza kuleta matatizo yafuatayo kwa Tanzania kwanza ni kukua kwa gharama za maisha nchini na pili kushuka kwa mauzo ya nje ya nchi. Hivyo hilo nalo linaweza kuwa na uwiano na tatizo la ugiriki kwani litachangia kupungua kwa mapato ya nchi na kuongeza tatizo la deni la nchi.

  Kwa kumalizia kufilisika kwa nchi huanzia na matatizo madogo madogo ambayo baadae yanasababisha nchi kuwa kwenye matatizo makubwa.

   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Shida ya watu wa ccm na serikali yao na wapanga plani zao za uchumi hawawezi kuona kama wanajikaribishia kiama kwa kuacha deni la nchi kuendelea kukua.
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ni hatari sana nchi kukopa kwa ajili ya kuendesha serikali ndio sababu Ugiriki walifilisika haraka. Kama tunakopa tukope kwa ajili ya uzalishaji na miradi ya maendeleo na sio kuendesha serikali deni lolote la ndani na nje ni hatari kwa uhai wa nchi na vizazi vijavyo.
   
 4. H

  Haki JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Marekani bado inakopa kwa ajili ya matumizi ya serikali yake, lakini mbona haianguki kiuchumi? IMF, EU ni magangs ambao nia yao kubwa ni kuziangamiza developing countries.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Good point mkuu ila nikuulize Debt ratio to GDP ya Greece ilikuwa ni 115% to GDP , USA pamoja na kukopa wako bado 50% to GDP unafahamu kitu gani??? Greece walikopa zaidi ya hata wanachokizalisha (National Economy). Greece watu hawalipi kodi, (marekani jamaa wa uncle sam hukufuata hadi chumbani for tax evasion ), Uchumi wa marekani ni mkubwa sana na hauko concentrated ukilinganisha na Greece. Lakini Uchumi wa Greece uko concentrated kama wa kwetu wa Tanzania.
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Shule tosha kwa kilaza Mustafa Mkullo, aone anavyotumaliza kwa vile yeye na JK wanaondoka 2015
   
 7. H

  Haki JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ujanja wa Marekani ni kwamba wanatumia Dollar. Pamoja na kwamba ratio yao ipo high, dollar haina thamani kiukweli. Wanaprint hela, lakini nchi zengine haziwezi kuprint hela zao, bila ya kuwa na devaluation ya thamani ktk hela yao. Dollar zipo nyingi sana nje ya US, kuliko thamani ya gold ambayo US anayo. Sasa hivi dunia nzima wanatumia US dollar, lakni hawajui kwamba kiukweli, haki, thamani ya dollar ni sawa au chini ya TZ shillings.
  Greece walikuwa na uchumi mzuri kabla hawajajiunga kutumia EU. Global Free Market ipo especially kwa nchi chache duniani, ambazo hazitocollapse hata ikitokea dharuba gani, wakiongozwa na US.
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Rais wa zamani Ujerumani atoa tahadhari sarafu moja EAC[/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 17 June 2011 21:17[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg


  Peter Saramba, Arusha

  RAIS wa zamani wa Ujerumani, Profesa Horst Kohler ameonyesha wasiwasi na mpango wa haraka wa umoja sarafu unakusudiwa kutekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), ifikapo 2012.

  Akizungumza katika hafla maalumu ya kuangalia matarajio na uhalisia wa EAC katika ulimwengu wa utandawazi mjini Arusha juzi, Profesa Kohler alisema kuharakisha mpango huo kunaweza kuleta mkanganyiko wa mambo siku zijazo kwani baadhi ya masuala ya
  msingi yanaweza kurukwa bila kujadiliwa na kupata makubaliano ya pamoja kwa maslahi ya wote.

  "Kwanini haraka katika jambo la msingi na muhimu kama hili. Siamini na haiwezekani kutekeleza mpango wa kuwa na sarafu moja 2012 kama ilivyokubaliwa katika makubaliano ya EAC. Jambo hili lazima lijadiliwe
  kwa makini na tahadhari kubwa," alisema Profesa Kohler.

  Aliwaambia wajumbe waliohudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Sekretarieti ya Afrika Mashariki na taasisi ya Kijerumani ya Konrad
  Adenauer Stiftung kuwa baadhi mambo yanayohusu sarafu moja hugusa utaifa wa watu ambao uzoefu unaonyesha ni kitu muhimu kuliko vyote kwa
  jamii yoyote.

  Alitolea mfano wa mpango wa sarafu moja kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya aliochukua muda wa zaidi ya miaka 10 tangu mwanzo wa mjadala ulioanza mwaka 1991 hadi mkataba uliposainiwa mwaka 1999 kabla ya utekelezaji
  rasmi kuanza mwaka 2002 ulipozinduliwa sarafu na noti ya kwanza ya jumuiya hiyo (EURO)

  "Kwa sababu hiyo, lazima yote yanayokusudiwa katika ushirikiano wa EAC upate kibali na uungwaji mkono kutoka kwa wananchi…ushirikiano usiwe mawazo na msukumo kutoka kwa viongozi wa kisiasa, lazima
  uzingatie mahitaji na maslahi ya wananchi," alisema Rais huyo wa zamani.

  Kuhusu mfumo wa soko huria, Rais huyo wa zamani ambaye jana alitembelea nchi ya Rwanda
  alisema lazima ziwepo sera na mfumo unaojali na kuzingatia faida na manufaa kwa wote msukumo mkubwa ukiwekwa katika maslahi ya jamii.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera alimhakikishia mgeni huyo nia thabiti ya kukamilisha na kutekeleza mipango yote inayokusudiwa katika ushirikiano wa nchi za ukanda huu wa Afrika Mashariki na kuongeza kuwa viongozi wote waliopo wameweka mbele nia na umuhimu wa mipango hiyo.

  Dk Sezibera alisema pamoja na mambo mengine ushirikiano huo unapanua soko kubwa na la uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa katika ukanda huo wenye jumla ya wakazi zaidi ya milioni 130 na tayari mipango ya
  kuboresha miundombinu ya barabara, reli, anga na maji kurahisisha mawasiliano na kusarishaji wa watu na bidhaa za biashara umeanza kutekelezwa.

  Source: Mwananchi.

  Pengine wakisema wafadhili watasikiliza na hoja sio thamani ya sarafu bali hatari ya kufilisika kwa nchi kutokana na madeni na mipango isiyo na tija ya maendeleo mkuu[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mdondoaji,

  ..hili bandiko lako lina umuhimu mkubwa sana.

  ..I wish wangepatikana wachangiaji wengi zaidi wanaoweza kuchangia ktk level yako.

  ..kuna mahali nilitoa dokezo kwamba tujifunze yanayotokea Greece wakati tunaendelea na mchakato wa EAC na haswa suala la Monetary Union. kauli yangu hiyo ilipelekea jamaa mmoja ambaye hutokea kwa msimu hapa JF anishambulie na kudai kwamba "sikulelewa ktk mazingira ya Kitanzania."

  ..wakati Uingereza wanakataa kujiunga na Euro watu wengi walikuwa hawawaelewi. Sasa hivi kuna wanaoona busara ya Uingereza kwa maamuzi waliyochukua.

  ..Tanzania na sisi tunapaswa kuangalia maslahi yetu kabla ya kuangalia maslahi ya wengine ktk hatua zote za muungano wa Afrika Mashariki.

  NB:

  ..umeeleza kweli kabisa kwamba Greece walianza kukopa bila simile. lakini ukumbuke kwamba hali hiyo ilisababisha na wao kuanza kutumia Euro na kulazimika kuishi ktk standards za nchi vigogo ktk EU. kwa lugha ya mtaani Greece alianza kumuiga "tembo" matokeo yake akapasuka "msamba."
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Unajua kubali kuonekana mbaya katika jamii lakini usimamie katika misingi unayoiona sahihi. Suala la EAC ni la kuangalia kwa macho mawili kwani kuna masuala mawili mazito hayajibiwi na majirani zetu. Mosi kuhusu ardhi ya Tanzania ni vizuri ardhi ya Tanzania imilikiwe na watanzania, wageni wa kutoka nje ya Tanzania wapewe temporary ownership au lease. Kuruhusiwa kwa ardhi kumilikiwa kwa watu wa nchi za nje kutachangia kupanda kwa bei ya ardhi, kodi ya nyumba, bei za nyumba mwisho wa siku watanzania wataishia wengi wataishia kuishi kwenye Squaters kama Kibera slums au Bombay slums. Ni swala sio la kubeza wala kudharau kwa lina athari kubwa kwa jamii ya Tanzania. Tunaweza kuungana na wenzetu katika viwanda, uhuru wa wafanyakazi, biashara, na haki za binaadamu. Masuala ya uchumi, sarafu na umilikaji ardhi yabakie ya kwetu sisi kama Tanzania.

  Swali la pili la hatari katika EAC ni tatizo la muungano wa sarafu. Sarafu ya Tanzania kwanza ina udhaifu mkubwa kutokana na kuzidi kwa matumizi ya dollar (dollarisation) nchini, pili sarafu ya nchi ni kipimo cha nguvu ya uchumi na kupanda au kushuka kwa sarafu kunaweza kuathiri kwa kiwango kikubwa uchumi wa nchi. Tatizo linaanzia katika thamani halisi ya sarafu yetu ukilinganisha na sarafu nyenginezo africa mashariki (basket of currencies). Tukijiunga na wenzetu ambao sarafu zao ni za juu kuna uwezekano wa sarafu ya nchi ikapanda na hivyo basi kupelekea thamani ya shillingi kupanda. Hilo sio tatizo kwa nchi yetu hasa ukitilia maanani tunategemea zaidi kuagiza bidhaa nje ila utaharibu sana maendeleo ya nchi. Kwani gharama za uzalishaji ghafi zitaongezeka kutokana na kupanda gharama za maisha, vipuri nchini, na pia malighafi. Hilo linaweza kuwa sio tatizo ikiwa tuna mipango thabiti ya kudhibiti mfumuko wa bei lakini kama hatuna mpango huo tusimlaumu mtu. Vile vile muungano wa sarafu utasababisha uuzaji bidhaa zetu nje ya nchi kuwa za ghali hasa bidhaa za kilimo. Kutilia maanani hatuna sauti katika soko la biashara linaweza kuwa tatizo kwani tunaweza kupunguza mauzo ya nje nchi (kilimo na viwanda) na kupelekea ufinyu wa pato la uzalishaji (current account deficit).

  Greece walipokosea ni hapo kwani wao walikuwa ni nchi ya kisoschalisti inayoingia kwenye ulimwengu wa kibepari. Walipojiunga na EU wakajikuta uzalishaji unapungua kila sikukutokana na kuongezeka ushindani, kukua kwa gharama za uzalishaji, mfumo mbovu wa ukusanyaji kodi. Hivyo basi mapato ya nchi yakawa yanapungua siku zinavyoenda. Tanzania ni vema tukajipanga kwanza tukaungana kwenye diplomasia, biashara, uhuru wa watu kufanya kazi, na usalama. Uchumi na mfumo wa fedha na umiliki ardhi tubakia nayo hadi tutakapoona tumesimama vizuri kwani sasa hivi ndio kwanza tunatambaa!!! Kama ulivyosema ndio maana Waingereza waliliona hilo wakalitolea nje sasa hivi anawacheka Ujerumani na Ufaransa kwani wanakiona cha mtema kuni.
   
 11. N

  Ngo JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haki; Marekani bado inakopa kwa ajili ya matumizi ya serikali yake, lakini mbona haianguki kiuchumi? IMF, EU ni magangs ambao nia yao kubwa ni kuziangamiza developing countries.

  Hapo kwenye Red, Upo dunia gani wewe? Unajuwa situation ya marekani ya leo? Kwa taarifa yako hali ni mbaya kuliko maelezo. Hakuna raia hata mmoja wa US utakayemuuliza tatizo kubwa la nchi yake na asikwambie ni Uchumi mbovu. Na uchumi ndo itakuwa issue kubwa kwenye uchaguzi mwakani. Kupiga kote kelele juu ya social security ni kwa sababu ya uchumi mbovu. Leo hii Obama anashitakiwa kwa kupeleka jeshi kupigana Libya bila ruhusa ya Bunge yote hiyo ni kwa sababu ya uchumi mbovu. Wasingepiga kelele kama uwajuwavyo wamarekani ( Vilanja wa dunia) juu ya kupeleka jeshi Libya kama uchumi wao ungekuwa Imara. Kama wasipopata ufumbuzi mapema, US wana hali mbaya zaidi miaka michache ijayo maana deni lao linaongezeka kwa haraka zaidi kila kukicha.
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,677
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ni moja ya thread za maana sana humu jf,provocative na imeshushwa vizuri.
  Mabenki makubwa duniani ndiyo chanzo cha worldwide financial crisis.Mtindo ambao wameutumia kuwarubuni viongozi wa dunia hii ndio umetufikisha hapa na utaharibu dunia hii kama mataifa maskini kama yetu hayatafumbua macho.
  Mabenki hayawezi kuendesha shughuli zake bila kukopesha,na faida kupitia riba ndiyo biashara yenyewe,nchi nyingi zina madeni,states,cities na hata watu wa kawaida wanaishi kwa madeni na asilimia inaogezeka kila siku.
  Madeni haya yametegwa kwa makusudi kuuleta utumwa,ni sawa na feudalism/serfdom ambapo peasants hata siku moja hawawezi kufaidika.
  Moja ya njia kuu ya kuhakikisha financial institutions zina make mega profits,ni free trade zones kama hizi za EAC,intergrated customs,common markets and finally currencies zina aim kutumia nchi kama Tanzania kuwa easily exploited by monopolies through regional trade blocks ambazo zinazidi kupanuka kwa sasa.
  Denmark,karibu 60% is the government revenue as a percentage of GDP,compared to 40% ya greece.Denmark siyo member wa EU lakini ina per capita income kubwa kuliko nchi yoyote ulaya na uchumi wake uko very stable.Kwa hiyo big government is not an issue.
  Solution ni ku balance trade hapa nchini,ku discourage importation through high taxes,ku overhaul our energy policy na ku redistribute earnings za government workers from bureaucrats kwenda kwenye education,health na agricultureal field employees.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kobello,

  Ni yakini kamilifu kwamba benki nyingi duniani zimekuwa zikifaidika na kunufaika na mikopo inayotolewa katika maendeleo ya nchi mbali mbali. Na kuna utafiti mmoja ulifanyika Oxford University ilionyesha kuwa nchi zilizokuwa katika mikopo ya IMF zilikuwa kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi kulinganisha na nchi zilizokuwa haziko kwenye mikopo ya IMF au World Bank (Elliot, The Guardian, 2011). Lakini tukirejea kwenye suala la mikopo ushauri uliotoa ni mzuri na una mantiki ila kuna mawili au matatu ya kutilia mkazo.
  Balance of trade ni kitu kinachoendana na mfumo wa nchi, usitarajie balance of trade kama hakuna njia au misingi ya kuweza kufufua viwanda vyetu. Kunahitaji kuwapo na mfumo wa kuwezesha sekta za uzalishaji zikafufuka, kurahisisha uanzisha wa biashara za kati (middle size enterprises), kutoa punguzo la riba katika mikopo kuifanya mikopo iwe rahisi nchi, na kama ulivyosema kudiscourage importation (uagizaji vitu nje). Vile kuwapo na mazingira ya kuwavutia wawekezaji wa nje walete viwanda vyao nchini (hasa Marekani ambao wanaonekana wamechoshwa na China) waje kuwekeza viwanda vyao kwetu ili watu wetu wapate kazi.

  Energy policy ni muhimu kama ulivyosema but Tanzania ni nchi inayohitaji fikra pana zaidi. Energy problem sasa hivi kuwepo na mipango ya hapa na baadae. Mipango ya sasa ni kuhakikisha umeme unapatikana wa uhakika, kutumia vyanzo vya maji (Rufiji) na mto Ruvuma, makaa ya mawe, na gesi vinatosha kutusaidia kupata umeme wa uhakika nchi. Pia mipango ya baadae tunaweza kukubaliana na hao Symbion, GE au mwekezaji mwengine waanzishe viwanda vya umeme kwa kutumia nyuklia , wind farm na makaa ya mawe kwa kiwango kikubwa na kuuza nchi kama Mozambique, Rwanda, Angola, Congo, Uganda, Somalia etc. Tukifanikiwa hili litaongeza ajira kwa watanzania, kukuza pato la nchi kwenye kodi, na kuhakikisha umeme wa uhakika nchini unapatikana.

  Denmark ni nchi moja ambayo umeitolea mfano wa uchumi imara. Ijapokuwa mwaka 2008 OECD Survey Report walionyesha kwamba Denmark waliathirika sana na mtikisiko wa sekta ya kibenki na uchumi, wadenish wameendelea kuwa na kiwango cha wastani wa mikopo. Inakisiwa kuwa kabla ya 2008 Denmark walikuwa na deni la nchi hadi 80% of GDP, deni la taifa likafikia kiwango cha asilimia 26 ya GDP ya nchi mwaka 2008(OECD Survey Report, 2009). Denmark wanakusudia kulimaliza hilo deni kufikia mwaka 2015 kwa kuhakikisha kila moja analipa kodi (in fact ni nchi ambayo wananchi wake wanalipa kodi kwa kiwango kikubwa kuliko wengine), kubana matumizi na kutumia rasilimali zao vizuri. Uchumi wa Denmark kwa asilimia kubwa unategemea sekta nne tu Madini, Viwanda vikubwa (petrochemical), Sekta ya kibenki na Kilimo hasa dairy farming. Wadenish walikataa nao walikataa kujiunga sarafu yao na Euro kwasababu kama za waingireza. Kroner badala yake waliiunganisha na Euro kwa makubaliano yakinifu (fixed exchange rate). Serikali ya Denmark walitaka kupitisha muswada mwaka 2004 kuhalalisha matumizi ya Euro ukakataliwa na wananchi kwasababu kama za waingereza juu ya athari ya sarafu ya pamoja kwa uchumi wa nchi.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [h=1]Greece loses €15bn a year to tax evasion[/h][h=2]Greek taxmen are under pressure to make a bigger contribution to easing the country's financial pain by collecting more money. The government is providing encouragement by cutting their numbers, salaries and closing 130 tax offices.[/h]
  [​IMG]Greek finance ministry employees protest in Athens last week


  By Roland Gribben
  6:00AM BST 20 Jun 2011
  [​IMG]9 Comments


  Tax evasion is a way of life in an economy riddled with abuses, discrimination and corruption but changing habits and culture represents one of the biggest headaches for a beleaguered government trying to climb a financial Olympus in flip-flops.

  Reducing the estimated €15bn (£13.2bn) that slips through the tax collection net each year is one of the conditions tied to a bail-out.

  There have been some imaginative attempts to widen the collection pool. Helicopters have been hovering over plush suburbs in northern Athens in the search for swimming pools in the homes of professional people who claim they are living on only €35,000-€43,000 a year.

  Thousands have been identified but tax records show only 300 have been declared. The swimming pool fraternity are also responding by using nets to cover the pools to avoid detection.

  Cash provides a convenient escape route for lawyers, accountants and builders. The government has published the names of almost 70 doctors it says have cheated the taxman and some surgeons are said to be earning €900,000 a year and not declaring tax.

  [h=2]RELATED ARTICLES[/h]
  "Only the stupid pay tax," one eye surgeon told a Greek state radio.
  Three months ago the country's top tax official was fired after failing to boost tax income, up from €50bn to only €52.5bn over the last two years. There was another €40bn of outstanding tax payments awaiting collection.
  Collectors complain that the taxpayers they chase have pay only about 20pc of what they owe and then disappear
  Economists estimate that 2m private sector workers are carrying the brunt of the tax load while a million public sector employees and 1.3m self-employed escape almost financially unscathed.
  The government is hoping that the rationalisation of tax offices and the belated introduction of a centralised database will help speed the collections.

  source: Telegraph UK.

  Greece loses €15bn a year to tax evasion - Telegraph

   
 15. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mdororo wa uchumi nchini Greece unapoendelea kugonga vichwa vya habari, serikali mjini Athens kupitia bunge, inafanya juhudi zote za kuikomboa. Njia zinazotumika zikiwa kupandisha ushuru na kuomba mikopo kutoka banki ya takriban euro billioni thelathini (30bn) kutumika rasmi na serikali. Hapo awali, juhudi za Greece kuungana na EU, zilizaa matunda mengi na zenye manufaa kwa uchumi zikiwemo kuongezeka kwa mapato ya serikali, sarafu katika sekta ya banki kuboreshwa, na kuimarika kwa miundo msingi za mawasiliano.

  Greece iliungana na EU mnamo mwaka 1981, na ikawa sehemu muhimu katika soko kubwa Uropa. Sekta ambayo ilinawiri kwa kiwango kubwa kutokana na muungano huo wa sarafu ni ya utalii ukizingatia kuwa uchumi bado ilikuwa changa. Na baadaye sarafu yao ikabadilishwa ikawa euro. Vyombo vingi vya habari zimesalia kusema banki nyingi ndani na nje ya mipaka (World bank ikihusishwa) ndio za kulaumiwa kwa mdororo unayoikumba. Hata kabla yao kujiunga na EU, kulikuwa na rekodi serikali hiyo ilikuwa na deni ya asilimia (37%) takriban dollar billioni $174bn, ikichangiwa kwa kasi na wafanyi biashara na wale "middleclass consumers" ambao walikuwa wana uwezo wa kupokea mikopo. (Economics of Imperialism: Origins of the Greek Crisis)

  Licha kuwa na deni, hii haikuzuia Ugiriki kujiunga na EMU mwaka wa 2001, ikizingatiwa Ubelgigi na Italia, walikuwa na deni sawia na Ugiriki ambayo ilikuwa asilimia sitini juu ya kiwango kilichohitajika kujiunga na EMU. Ingawa inaweza onekana sawa "kisiasa" kulaumu banki ya dunia, na kile kitendo cha muungano na EMU kama sababu kubwa za mdororo wa uchumi, udadisi unaonyesha Greece hawana uwezo wa kurejesha deni kwa ukamilifu. Kwa sasa serikali imesalia kupeleka mali ya umma kwenye minada ili serikali za nje na banki wapate njia ya kurejesha mikopo walizotoa. Lawama hii ya mdororo wa uchumi haitatwaliwa na banki ya dunia pekee au wadau wengine wa uchumi, bali itachukuliwa hata na wagiriki na hasa serikali kwa kushindwa kuimudu uchumi.

  Kwa kifupi, tunazingatia hii deni kuchangia kwa ziada matatizo ya kiuchumi, baada ya mwaka 2006 na 2007, wakati akiba za watu binafsi au "middle class" katika banki zilishuka kutoka asilimia 3.2% hadi negative -3.2%. Tatizo la "job-cuts" au kupungua kwa makazi miaka za tisini kuendelea hadi 2001 ilisababiswa na banki nyingi humo kudai mikopo zao kutoka kwa makampuni hata kabla yao kujiunga na EMU, na siyo kufurika kwa wageni kutoka sehemu zingine za EU (kama Waingereza). Mataifa kama Ureno na Italy, kwa mfano wana "credit rating" inayolinganishwa kama "junk status". Kwa nini nchi hizi mbili haziangaziwi sana katika vyombo vya habari licha yao kuwa na deni sawia? Je! Kuna kitu maalum kinaangaziwa Ugiriki? Jibu ni la!.......

  Serikali ya ugiriki ilikuwa inatumia asilimia 45% ya mapato ya nchi, GDP yao ikiwa asilimia 39-40% (ikilinganisha na asilimia 44-45% ya viwango vya mataifa mengine katika EU) huku baadhi ya makampuni, wafanyi biashara, watu binafsi, na viongozi wa kisiasa wakikwepa kulipa ushuru. Hii ndiyo tatizo kubwa ambao imechangia kwa mdororo wa uchumi! Takwimu za banki ya dunia zinaonyesha wazi viwango vya mkopo za mataifa kama ireland na portugal zikilinganiswha na Ujerumani. Mkopo wa Greece ni aslilimia 18% ukilinganisha na 3% ya Ujerumani.

  [​IMG]

  (Source: IMF World Economic Outlook Update, June 2011 )


  Ujerumuni kama tujuavyo wana export market kubwa katika EU na uchumi yao inapokea "inflows" kutoka "direct investment" ya kuwawezesha kulipa mikopo. Katika kuanza kwa muungano wa sarafu ya EU, GDP ya Ugerumani ilichangia asilimia 24%, na ya ufaransa ilichangia 20% huku ya Ugiriki ikichangia asilimia 2% (economicsofimperialism.blogspo t.com/2011/06/origins-of-greek-crisis.html).

  Tahariri:

  Utakuta kuna wadadisi wa kiuchumi hususan wale kutoka Uingereza kupitia vyombo vya habari na tovuti zao binafsi wakimulika mdororo huo kama tatizo la muungano wa sarafu. Lakini hiyo ni propaganda mtupu. Uchumi ya Uingereza wakati huu inapitwa na mataifa kama India, South Africa, na Brazil.

  NB: Nimetumia EMU kumaanisha European Monetary Union! Kuhusu Unitary visa, hebu digest makala yangu kwanza, halafu nitakusimulia mtazamo wangu
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Bado Saana, Tanzania haiwezi kufika huko Tuna Madini Mengi, Watanzania hawaishi kwa Plastiki (Credit Card)

  Hawanunui Nyumba wa Mkopo wa Mabenki Feki

  USIWE NA WASIWASI na KUTISHA WABONGO
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba Mkullo is the worst Minister for Finance this country has ever had; the guy does not know what is happening around him and to make matters worse his boss is not knowledgeable and hence cannot take any remedial measures.
   
 18. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kufananisha Tanzania na Ugiriki ni kituko
   
 19. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  open lesson to our enclosed ostriches....! they hide their heads undernearth thinking they are not seen while the whole body is out....!
   
 20. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Na jaribu kusema, ukipewa dhahabu halafu mwishowe ipotee, utalaumu nani?
   
Loading...