Deni la Tanesco - Zanzibar na Serikali ya Muungano

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Ndugu wabunge msiorasmi wa JF (hamjatangazwa na NEC ya mafisadi). Katika mkutano wa wajumbe wa mikoa wa chama cha wafanyakazi-Tanesco; moja ya hoja nzito walizozitoa ukiacha ile ya DOWANS ni juu ya deni la umeme ambalo Tanesco wanaidai SMZ kupitia shirika lake la umeme ambalo ni takribani bilioni 46.

Pia serikali ya Muungano inadaiwa mabilioni. Madeni haya makubwa yamekuwa sababu nyingine kubwa kwa Tanesco kupandisha gharama za kufungia wateja wapya umeme na kuuza umeme wao kwa gharama kubwa mno.

Watanganyika tunabebeshwa mizigo isiyo yetu. Serikali ya Muungano imechukua gharama zote za IPTL, SONGAS, DOWANS na SMZ na kuzitua juu ya vichwa vyetu, watoto wetu, wajukuu wetu na hata wazee wetu waliofariki kwa ufisadi huu,walipokosa dawa,vipimo,huduma na umeme huko mahospitalini.

TUAMKEEE!:angry:
 
Wakate umeme tu tujue moja, kuna umuhimu wa kuwauzia haya mashirika wazungu ili serikali itie adabu.
 
Wakate umeme tu tujue moja, kuna umuhimu wa kuwauzia haya mashirika wazungu ili serikali itie adabu.
Mkuu.
Huamini kuwa kuna waafrika au watanzania wanaoweza kuliendesha hili shirika?

Kama ni hivyo huoni pia ni vyema hata uendeshaji wa serikali tukawakabidhi hao wazungu pia?
 
Back
Top Bottom