Deni la taifa ni sh 35.01 trilioni, ukiambiwa uchangie kumaliza deni uko tayari?

Freelancer Wakala

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
1,193
828
DENI LA TAIFA AMBALO LINATAJWA KUFIKIA SH.35.01 TRILIONI UKUAMBIWA UCHANGIE UPO TAYALI KUMALIZA DENI HILO?
 

Attachments

  • 1458968843557.jpg
    1458968843557.jpg
    35.5 KB · Views: 35
Tunaweza kusema kila Sh 10000 ya fine za barabarani zipelekwe kulipia deni la Taifa bila shaka litaisha
 
kila kitu tuchangie mtasema tuchangie kulipa mishahara watumishi wa umma sasa..kazi ya serikali ni nini mkuu..Sichangii
 
Mimi sichangii....kila mwisho wa mwezi wananikata kodi 145,000.. hiyo itatosha walipe...

pumbavu...walikopa zkaishia matumboni mwao..then kulipa tulipe sote....##nyambafu
 
Hela wanazichezea kwenye kurudia mauchaguzi ambayo washindi walishajulikana baada ya kwenda kupunguza deni LA taifa,siko tayari kama hawataniambia wale twiga waliwauza bei gani na kama hawakuwauza kwanin hawajarudishwa hadi leo
 
Sidaiwi chochote maana sijakopa popote, kama kuna waliokopa kwa niaba yangu basi watalipa pia kwa niaba yangu
 
DENI LA TAIFA AMBALO LINATAJWA KUFIKIA SH.35.01 TRILIONI UKUAMBIWA UCHANGIE UPO TAYALI KUMALIZA DENI HILO?
Deni lote akamatwe Kikwete na mtandao wake wa mafisi mafisadi na majangili walipe; wao ndio chanzo na sababu ya deni hilo, kukopa na kuiba!
 
Kabla ya kuchangia itabidi waniambie hizo hela walifanyia nn? Na zile Lumbesa za manoti pale Stanbic nani alichukua.
 
Kila mtu ambaye yupo tz whether ni Raia ama ni mkazi tu! anachangia kwa kukatwa kodi ya kipato (paye), faida katika biashara, na chochote anachonunua (VAT), Na hakuna mtu wa kawaida asiyechangia kwa njia hizi za kodi ya moja kwa moja za kipato (direct tax) na kupitia manunuzi/ kodi ya ongezeko la thamani na forodha (VAT & import duties). Sasa sijui mtoa mada ulikuwa unataka tuchangie kama michango na sadaka zinazotolewa kwenye nyumba za ibada?

Kama ni kuchangia kwa kutoa michango na sadaka kama katika nyumba za ibada natumaini watz wengi tena wazalendo hawapo tayari. Ila kama ni kuchangia kwa kulipa kodi halali kwa ajili ya maendeleo ya taifa lao wapotayari wazalendo wote kufanya hivyo, ingawa uzalendo wa kufanya hivyo nauona kama unapungua kwa kuwa kuna ubadhilifu mkubwa wa mali ya umma unaofanywa hivyo uzalendo unashuka kwa kuwa kuna rushwa, ufisadi na urasimu na mbaya zaidi hali ngumu ya maisha kwa walio wengi tena wakiona wachache wanaishi maisha mazuri.

Tena walio wengi wenye maisha duni wa(tu)nahoji hizo fedha zimefanyia nini wakati miundombinu mibovu, hakuna dawa, zahanati, hospitali,elimu duni. Gharama ya maisha imepanda sana, mifumuko ya bei tena bei ya bidhaa muhimu kila kukicha zinapanda bei na kufanya maisha kuwa magumu sana, sasa tuliowengi tunafikiri ndio tumefunda mikanda ili kufidia deni hilo maana ni lataifa linamhusu kila mtu aliye wa taifa ili, na hivyo linaathiri maisha ya kila mtu wa kawaida.

Ingawa sio mchumi wala mtaalamu wa masuala ya bajeti, ila ukiangalia bajeti yetu ya kila mwaka utaona kuwa matumizi ya kawaida ya serikali (Recurrent expenditure) ni makubwa sana hata hayana uwiano na matumizi ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo (Development expenditure). bajeti2015/2016 ni trilioni 22.5, Za maendeleo trilioni 5. I bet tunakopa ili kufinance reccurent exp instead of dvp thus why national debts speeds ups like Bolt in the Olympic race
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom