Josaje Mtui
JF-Expert Member
- Oct 1, 2016
- 2,459
- 2,141
Nilikua na demu mmoja hivi tuliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi tukiwa secondary miaka ile ya 98 na kwa kweli tulikoleana ila baada ya kumaliza shule yeye alienda kusoma kenya na kwa muda mrefu hatukuwahi kuwasiliana.pindi aliporudi masomoni alirudi na mtoto na nilipojua alijaribu kunikwepa sana.nilijaribu kunyapia nyendo zake nikagundua kuwa jamaa aliemtundika mimba ndie alikua anamsomesha kuanzia kidato cha kwanza mpaka chuo.baada ya kujua hivyo nilichukulia poa tu kwa maana sikua na namna yeyote ya kufanya ila kubwa ya yote nilitamani japo papa yake tu nikate japo kiu.katika pita pita ya kimaisha tukakutana kwenye kamati ya harusi ya rafiki yetu ambae tulisoma wote pia.hakika nilifurahi sana kumuona na hapo hapo ikawa shughuli ni moja ya kula utamu kiroho safi.tulikumbushiana mengi sana na alifunguka changamoto anazokabiliana nazo kwenye mahusiano yake na yule jamaa a-z.hakika ilikua long story lakini sikumshauri kitu kibaya zaidi ya kumwambia yatafika mwisho tu.na kweli yalitimia wakaachana na gafla nikajikuta naendeleza libeneke.kwa bahati mbaya nilipata kazi Geita hivyo ikanilazimu kupiga kambi ya kimaisha huko..duh bidada akavuta msela mwingine ambaye nae walikuja kuzinguana wakaachana akarudi tena kwangu.sasa amenigeuza kama dekio kwa maana amekua akijihusisha na mapenzi ambayo akishakorofishwa huko yeye anapiga break kwangu na hunielezea yote anayotofautiana huko..kwa sasa umri umeshasogea na mimi ninafamilia yangu sasa ila juzi kati kanipigia cm ananitafuta na anataka kuonana na mimi.nimejaribu kumkwepa lakini bidada huyu amekua mgumu kuelewa na ananiambia haogopi hata familia yangu.wakuu hebu nipeni ushauri na upembuzi yakinifu..