Demokrasia ya Marekani bado iko juu

Demokrasia ya Marekani bado iko juu

James Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,205
Reaction score
1,509
Inasikitisha kuona baadhi ya watu wakitumia jina la Marekani kueneza propaganda za kisiasa. Nimewasikia baadhi ya wajinga wakijigamba kuwa nchi fulani ina demokrasia ya juu kuliko Marekani!

Sasa ili kuweka mambo sawa inabidi kuwajibu hawa wapuuzi ili wasiendelee kuwajaza watu ujinga.

Kwanza, kuhusu ulalamikaji wa Donald Trump kuhusu upigaji wa kura kwa njia ya posta ni maoni yake binafsi. Utaratibu huo umekuwepo kwa miaka mingi bila ya kulalamikiwa.

Pili, kuhusu Trump kwamba anaweza kukataa kuachia ofisi ni jambo la kupuuza. Ki historia jambo hilo halijawahi kutokea kwenye taifa hilo. Halafu hata ikitokea kwamba atakataa kuachia ofisi bado taifa hilo lina vyombo huru vya kumshughulikia mgombea huyo.

Napenda kumalizia kwa kusema kwamba hata kama kukitokea kasoro za hapa na pale kwenye uchaguzi wa Marekani lakini bado wataweza kuzitatua kwasababu wana vyombo madhubuti na huru. Vyombo madhubuti na huru vya kutatua mambo yao ndio tofauti kubwa kati yao na nchi isiyo ya kidemokrasia.
 
Marekani demokrasi yao kiukweli iko vizuri katika chaguzi na Mambo personal Kama LGBTQ, Lakini kwa upande mwingine wamarekani ni wavunjifu wakubwa wa haki ya kuishi ambayo ni moja ya principle ya demokrasi.

Lakini pia demokrasi yao nje ya Marekani ni kwaajili ya maslahi yao ya kiuchumi na kijeshi tu na sio maslahi ya mataifa wanayoyatupia mabomu.

Fikiria kule Iraq mwaka 2003 wamarekani waliwalazimisha mateka wa Iraq "kufirana" hiyo nayo ni demokrasia?
 
Ninacho amin ni kwamba true demokrasia haiwez kuwepo kweny nchi maskin ....pia x
Sometimes dictatorship ina saidia mfno ....China ..German
 
Back
Top Bottom