Demokrasia ni lazima ipatikane

Demokrasia ni lazima ipatikane

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
8,017
Reaction score
18,437
Rejea hotuba ya Rais wa Marekani kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Taifa, kwa ujumla, Dunia ipo na wapenda na wapigania demokrasia, haki na uhuru.

Tatizo letu Watanzania ni kwamba hatujaonesha kwa vitendo kuwa tunataka demokrasia, haki na uhuru. Tunataka jamii ya kimataifa itutafutie demokrasia, haki na uhuru wetu, badala ya wao kuwa wasaidizi tu katika jitihada zetu.

Sisi yatupasa kuwa mbele, na Dunia itakuwa nyuma yetu, kutupatia nguvu. Hatuwezi kuiweka Dunia mbele, yaani wadaia haki, uhuru na demokrasia yetu kwa niaba yetu, huku sisi tumebweteka.

Sasa tusimame, tuwe mbele, tudai kwa nguvu zote tunachokiona ni muhimu kwa Taifa letu. Japo tunajua, tuna mfumo wa utawala dikteta, tuanze kwanza na mazungumzo. Tukusanye nguvu ya wananchi wazalendo, wanaopenda nchi yao bila unafiki, wanaotaka nchi yao iongozwe kwa misingi ya kidemokrasia, haki na uhuru wa kweli kwa kila raia.

Kikao hicho kishirikishe wawakilishi toka vyama vya siasa, taasisi za kidini, vyama vya kitaaluma, wanaharakati, taasisi za kisheria kama vile chama cha wanasheria wa Tanganyika na Zanzibar. Kikao hicho kitoke na mapendekezo ya maazimio ambayo yatapelekwa kwa Rais.

Rais baada ya kujadiliana na watu wake, atoe ratiba ya utekelezaji wa kupata katiba mpya.

Uovu wowote, kama vile kuzuia kikao hicho au kupuuza mapendekezo yatakayotolewa, kifuatiwe na maandamano. Sijataja kabisa uwakilishi wa Bunge maana sote tunajua kuwa wabunge waliopo ni zao la uovu dhidi ya demokrasia.
 
Alisema zenzake na bado hamna kitu , Biden ndio rais goigoi tangu 1998 ,kazee kamoja kipuuzi sana

USSR
 
Besige hapo Uganda alisubiri kwa hamu ktokana na hotuba kama hizo za akina Baiden lakini mpaka ameamua kuwa Lipumba tu sasa maana haoni chochote mbele ya safari
 
Alisema zenzake na bado hamna kitu , Biden ndio rais goigoi tangu 1998 ,kazee kamoja kipuuzi sana

USSR
Uimara wa kiongozi haupo katika maguvu. Baiden atazidhibu tawala dhalimu bila kutumia nguvu za kijeshi.
 
Besige hapo Uganda alisubiri kwa hamu ktokana na hotuba kama hizo za akina Baiden lakini mpaka ameamua kuwa Lipumba tu sasa maana haoni chochote mbele ya safari
Usaidizi wa Dunia ni baada ya jitihada za wananchi.
 
Usaidizi wa Dunia ni baada ya jitihada za wananchi.
Sasa Besige mpaka alikuwa anapuliziwa maji ya kuwasha akiwa na raia amekinukisha mtaani.

Sembuse nyie mnaokinukisha kupitia Maria space
 
Back
Top Bottom