Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Kwa wenye akili tumeshaelewa yanayo endelea kutokea ndani ya CCM na CHADEMA, na nilishawahi kusema kuwa DEMOKRASIA kamwe haitamkomboa mtanzania bali "kweli" ndio itakayo mkomboa mtanzania. Rejea sakata la Kitila Mkumbo kwa CHADEMA na sakata la Nape Moses Nnauye na Horyce Kolimba kwa CCM.
Demokrasia inategemea msingi wa wengi wape hata kama hao wengi wamepotoka au wameikanyaga "kweli". Ikumbukwe maamuzi ya kidemokrasia huitimishwa kwa kura, na wengi ndio hupata "haki". Naweza kusema "haki" huthibitishwa na kura.

"Kweli" husimama yenyewe na haiitaji nguvu ya kura ndio ipate kusimama. "Kweli" yaweza kufichwa na "haki" mara nyingi lakini si mara zote. Hata mahakamani jopo la majaji au mahakimu hupiga kura ili wapate kuipa nguvu "haki", kama ndivyo, hata mahakamani hakuna "kweli" bali kuna haki inayopatikana chini ya misingi ya wengi wape.

Pamoja na hayo, "kweli" ni kama kaa la moto kiganjani, wacha mwenye kuusimamia aungue, "kweli" ni kama pakanga ulimini wacha mwenye kuukumbatia aonje uchungu wake, naam, wacha yote ya mkute kwani ndio gharama ya kusimamia "kweli".
MFANO HAI.
<font size="4"><span style="color:#008000;">
Kama sitakosea Mh John Mnyika mbunge wa wananchi mwaka wa jana aliwasilisha hoja ya binafsi kuhusu uboreshaji wa mfumo wa maji safi na maji taka katika jiji la Dar es salaam. Hoja ilikuwa ni sahihi na ilikuja wakati sahihi pamoja na kuchelewa kwake, na niseme bila kigegezi chochote kuwa mh.Mnyika aliongozwa na "kweli" wakati alipokuwa anawasilisha hoja yake ile. Nasema aliongozwa "kweli" kwasababu ni kweli iso shaka yoyote Jijini Dar es salaam kuna tatizo kubwa la maji na bado serikali haijakuwa na nia ya dhati katika kulitatua.
Mnyika alilitaka bunge liamue kulipunguza si kama kulimaliza tatizo hilo kwa kuitaka serikali ifanye mambo kadhaaa ambayo Mnyika aliyapendekeza kwenye hoja yake binafsi.
Kilichotokea, Waziri akiwa mchangiaji wa kwanza alipendekeza hoja iondolewe wakati kimsingi serikali haitakiwi kuja na pendekezo hilo zaidi ya kutaka maboresho, bunge ndio laweza kuiondoa hoja.
Kilichofuata na tena mara baada ya vurugu za hapa na pale, Ndugai akasema "sasa nawahoji" wanaosema hoja iondolewe waseme "ndio" na wanaokataa waseme "sio" waliosema ndio walishinda na hoja ikaondolewa. Wachache pamoja na "kweli" yao lakini walishindwa, naam, "haki" iliishinda "kweli".
Sasa hii ndio haki iliyoiminya "kweli", na hii ndio demkrasia. Mambo kama haya ya bungeni, hata kwenye vikao vya vyama vyetu hujitokeza na tena mara nyingi sana. Nchi, vyama vya siasa na vile ambavyo si vya siasa hubeba gharama za maamuzi mabovu kisa wengi walishinda pamoja na hao wengi wamepotoka. Demokrasia ije na mlango wa kuwashughulikia wengi na maamuzi yao mabovu na si kusema hao wachache wajipange tena ikiwa wao ni sehemu ya watu watakao onja chungu ya maamuzi mabovu pindi yakianza kutekelezwa.
Kwa kuzingatia nukta za hapo juu, tusiishie kutaka demokrasia ndani ya vyama vyetu bali tuende mbali zaidi kwa kuhitaji zademokrasia ya kizalendo; demokrasia itakayoweza kuwashughulikia na kuwashinda wengi wanao kiuka malengo makuu ya kuundwa vyama vyetu. Kama wengi watategemea wingi wa kura zao katika kuharibu malengo makuu ya aidha ya nchi yetu au ya vyama vyetu ni lazima demokrasia iwe na mlango wa kuwashugulikia na kwashinda hao wengi.
Nahisi mlango huo kwenye demkrasia yetu ya hapa duniani haupo, na kama upo basi si wa kutosha kwa kupita mtakaji na kisha asipate madhara kwa kubanwa au kuchubuka. Hivi tukijaribu kuuweka tutashindwa? Hakuna daraja, lakini tukiamua tutaweza kutengeneza japo moja. Hapa nilipo natafakari namna ya kuutengeneza huo mlango. Je mwenzangu uko na namna?
Njano5.
0684588504

Last edited by a moderator: