Demokrasia ilobagazwa

Swali moja - Unaweza nambia kwa nini Kiutawala tunahitaji Vyama vingi vya Siasa?
Sio kwamba tunaitaji bali Demokrasia ndiyo inayoitaji hivyo. Pia ili kunielewa vizuri nakuomba soma ibara ya 11(9) kupata maana ya neno "Demokrasia", pia ibara hiyo hiyo ibara ndogo ya (8) imezungumza maana ya neno "Siasa".

Kumradhi: hapa nazungumzia rasimu ya katiba iliyopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com
 
Mkuu rasimu ya Katiba (Warioba) inatokana na maoni ya Wananchi, hii sio Katiba wala maoni au mapendekezo ya Warioba na tume yake. Hata Katiba pendekezwa ya Bunge nayo ni mapendekezo ya Bunge lile ambalo Ukawa walijitoa. Ni Chupa ilojaa nusu au nusu chupa pungufu.

Kutokana na mada hii tukizungumzia Demokrasia ilobakwa ni muhimu kutambua umuhinu wake katika jamii badala ya kuiga kwa sababu ati Demokrasia ndiyo inataka wakati sisi hatiitaki. Hili ni kosa kubwa sana sawa na kuozeshwa mke wakati wewe humtaki wala humuhitaji.

Ni hivi ndugu yangu, duniani kote chimbuko la vyama vingi ama Upinzani ilitokana na Upinzani wa Mfumo wa Kiutawala kwa wakati huo.
Mfano Uingezeza ilokuwa ikitawaliwa Kiumla mamlaka yote chini ya mfalme, likatokea kundi la watu wakaona hatakiwi utawala wa Kifalme kuwa na Mamlaka yote pasipo kuwa questioned katika uwajibilaji wanapokosea (to be accountable) na ikibidi kuwakosoa viongozi wa Serikali yake haitakuwa ni Uhaini. Hoja zote za Kiutawala zitajadiliwa Bungeni na ndio Uliberali ulivyotokea Uingereza na kuwa chama cha Siasa mpaka leo.

Marekani vile vile, Walianza kama nchi moja Federalism kwa states zile 13 (nchi moja, chama kimoja) wakatokea wataalam wakataka kila States iwe na mamlaka yake katika mambo yasiyokuwa na Muungano (Federalisim) ikafanyika kwa.matkwa ya wengi kutenganisha mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano.

Kabla ya hapo nadhani ujio wa chama cha Republican ulitokana na kupinga biashara ya Watumwa. Hivyo utaona kwamba Vyama vya Upinzani vilitokana na pingamizi ya mfumo wa Kiutawala ulokuwepo, sii kwa sababu Demokrasia inataka hivyo.

Sisi kwa bahati mbaya sana tuliiga Demokrasia ya vyama vya Upinzani pasipo sababu ya msingi na ndio maana asilimia 80 walikataa Vyama vingi. Mwalimu akatoa ushawishi mkubwa kinyume cha maoni ya Wananchi na hata rais Mwinyi kama sikosei. Nyuma nimeeleza wazi jinsi Chadema na CUF zilivyopatikana.

Hii ndio sababu mimi nimezungumzia Swala la Mwalimu Nyerere nikitumia Ujamaa na Azimio la Arusha kama mfumo tangulizi ulokuwepo na sasa tuunde Vyama vya Upinzani kutokana na Upinzani wa Azimio hilo. Yaani tuwe na sababu ya kuunda vyama vya Upinzani, laa sivyo tunaonekana wapumbavu kuiga vitu ambavyo sisi hatuvihitaji kabisa.

Na napotumia jina la Mwalimu Nyerere haina maana.yeye ndiye muasisi alotuletea Ujamaa nchini bali Utawala wake wakiwemo toka kina Abrahaman Babu, Salim A.Salim, Hanga pamoja na hawa wazee wetu kina Warioba, Wasira na wataalam kina Prof. Shivji n.k. walikuwepo na wakapitisha Katiba ya mwaka 1977.

Natumia jina la Mwalimu kwa sababu yeye ndiye alokuwa kiongozi. Hao wanaotaka zidumu fikra za Mwalimu iwe ndio Chama lao maana wana haki Kikatiba ya kuendeleza Ujamaa ule halafu ilitokee Wapinzani wa fikra zile. Hii ndio maana halisi ya kuwa na Demokrasia nchini.

Laa sivyo basi tuchukue sababu ya Mfumo wa Utawala huu wa Samia (CCM) kufanya Upinzani wa Itikadi na sera za CCM badala ya Upinzani wa rais Samia kama tunavyoufanya kuwa wa Uzanzibar vs Utangantika. Demokrasia yetu inakuwa ya kutopendana wenyewe badala ya kupingana na mfumo kandamizi wa Kiutawala.

Tusipokuwa na sababu inayozaa Vyama vya Upinzani kwa maana ya kupingana na mfumo uliopo, basi tutakuwa Wapumbavu wakubwa wa kuiga vitu tusovihitaji katika jamii na ndio maana tunasambaratika badala ya kuuungana.
Chadema, ACT, CUF, NCCR na vyama vingine vyote 19 kama havina pingamizi la mfumo au muundo wa nchi ili wapewe ridhaa yetu kuleta mabadiriko ya mfumo (Kutunga Sheria) basi tutakuwa majuha kalala wa kutupwa.
 
Asante na nimekuelewa vizuri kabisa.
Kwanza kabisa naomba nikwambie hili kwa usahihi kabisa kwamba Rasimu ya katiba iliyopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com ni pendekezo langu la katiba sio la serikali au la wananchi wote, pia pendekezo hilo haliondoi mchakato rasmi wa katiba. Hivyo basi yale yaliyokuwa humo yachukulie kama ni mchango wangu wa kisomi, kitaaluma na kiraia kwa taifa langu hasa pale nilipozungumzia kuhusu muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, Yaani.
1. Baraza la Usimamizi wa Taifa (huu ni muhimili wa usimamizi wa misingi yote ya taifa, ndio mamlaka ya kimuungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, mamlaka ya kutoa Tathmini zote za taifa na muongozo.)

2. Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (muhimili wa utendaji, utekelezaji wa sera za taifa, Dira ya taifa, ulinzi na usalama na mengineyo mengi.)

3. Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania (muhimili wa uwakilishi wa dhamiri mbali mbali za wananchi katika ngazi za majimbo, kutunga sheria, kupitisha bajeti na mengineyo )

4. Mahakama ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (muhimili wa utoaji haki, hukumu za kisheria, mtatuzi wa migogoro ya mihimili yote na mengineyo)

Ubora wa muundo huo ni kwamba hile hoja ya serikali tatu, au mbili unatatuliwa kwa kuongeza muhimili wa nne ambao kazi yake si kuunda serikali bali kusimamia misingi yote ya taifa, yaani.
1. usawa katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania,
2. kila upande wa muungano upate kilicho sawa,
3. ndio waangalizi wa wapi tumekwama kama taifa,
4. ndio mfano wa refa kwenye mechi za mpira wa miguu au vyovyote.

Pia Rasimu hiyo haijaishia hapo imezungumzia maswala mengine mbali mbali yenye tija kwa taifa letu.

Hivyo basi naomba nikubaliane na wewe kwamba rasimu hiyo ni maoni tu ya mtu mmoja na yanaweza kukubaliwa na wengi au kukataliwa kwa hoja iliyowazi kabisa.

Nikirudi kwenye maswali yako mengine nakumbaliana na wewe kwamba Miaka ya 80 tulikubaliana wote au kundi kubwa la watu kuitaji mfumo wa chama kimoja cha siasa lakini Nyerere hakaona sio sahihi kubaki kwenye chama kimoja. Lakini hoja hii naomba tufanye hivi.

Embu tujaribu kuuliza swali lile lile la zamani kwamba wananchi wanataka mfumo wa chama kimoja au vingi hivi leo kisha tuone majibu yao watasemaje...?

Mimi nadhani 80% watataka vyama vingi na hapa sasa ndipo unapoona kwamba zamani hawakuwa na utandawazi na uelewa wa kina lakini sana shilingi inapinduka. Kwaiyo hoja hile hile na swali lile lile la zamani likiulizwa leo litatoa jibu tofauti na la kushangaza kabisa.

Pia vitu vingine vyote ulivyosema hapo chini naunga mkono kwa ukamilifu isipokuwa tu mimi naona kwamba Tunapaswa kuwa na muhimili wa usimamizi wa misingi ya taifa hili isije kupotea au kuiga mataifa mengine ndio maana Pendekezo langu la muhimili wa nne inapata nguvu. Pia Let's say tuko na ujamaa kama unavyotaka, swali ni je bila kuwepo na mamlaka ya kusimamia misingi huo huoni kwamba wanaweza kuzaliwa wananchama kwenye chama hicho hicho na kuanza kudhoofisha chama chenyewe na msingi wenyewe.?
Mfano huu ndio tunaosikia now days kuhusu "CCM MTANDAO, WAUNI, WABAGAZAJI, N.K",

Kitu tunachobishana mimi na wewe ni chepesi sana, kwamba wewe unataka turudi kwenye misingi bila nyoongeza nyingine yoyote, lakini mimi nataka turudi kwenye misingi isipokuwa tuwe na muhimili wa usimamizi wa misingi hiyo.

Hivyo basi kurudi kwenye misingi bila kuunda chombo madhubuti cha kuilinda hiyo misingi ni bahati nasibu, kamali, na kukosa mzizi ya kweli na mwisho Tust me miaka kumi baadae tutarudi kulalamika tena kwamba turudi kwenye misingi.....!, Misingi yetu imedhoofishwa tena..!, na malalamiko mengine kama hayo lakini tukiwa na mamlaka yenye kazi hiyo tu.! malalamiko yanakuwa ni kuikumbusha mamlaka hiyo itende wajibu wake sio kuanza kubishana tena wapi tumekwama.


Mimi nadhani Pendekezo la katiba nililolitoa linaitaji kupewa macho ya kisomi, kitaluma na kiraia na nina imani kuna kitu cha msingi sana kinaweza kulisaidia taifa letu.

Nawasilisha Hoja.
mrxtz2026
Chanzo: www.katibampya.com
 
Nami nimekuelewa vizuri nadhani hata mimi niliwahi kupendekeza Mhimili wa nne nikiutaja kama Baraza la Wazee (Senate) ambao watakuwa na mamlaka ya juu kupitisha maazimio yote ikiwa ni pamoja ya Sheria, Mikataba, teuzi za rais na mamlaka ya kumhoji Kiongozi yeyote wa Serikali au Taasisi za Umma anapokiuka Sheria za nchi pamoja kujihusisha na Ufisadi wa aina yeyote utakao ligharimu taifa, especially kutokana na report ya CAG itashughulikiwa na Baraza hili. Hii itawapunguzia kazi wabunge wa Bunge la Jamhuri wao waendelee kutumikia majimbo yao, kutunga Sheria na kuisimamia Serikali. Baraza la Wazee litajikita zaidi kwenye Check and Balance.

Kwa hiyo, napotengana na wewe ni jina la Mhimili huo na majukumu yake. Kikubwa nilichokiona upande.wangu mimi ni kutokana na Bunge letu mara nyingi Upinzani hawapati 1/3 ya Wabunge, hivyo Chama tawala kinaweza pitisha Sheria au mikataba mibaya kwa sababu wana zaidi ya 2/3 ya Wabunge Baraza hili litakuwa kinga kati ya Serikali na Wananchi.

Uwepo wa Baraza la Wazee utalazimu wao wapitishe muswada kwanza kabla ya rais. Wakikataa basi muswada au Mkataba hautapita japokuwa Bunge na rais walitaka kupitisha chini ya pazia.

Shukran sana kwa Uandaaji wa rasimu yako, kusema kweli sikuelewa toka mwanzo nikidhani unatumia rasimu yq Warioba na ile Pendekezwa.
 
Exactly, nakuunga mkono kwa 100%, nakubaliana na wewe na nimefurahi sana kuona tuko watu wawili wenye wazo moja na tumepishana majina tu, mimi sitaki kuongeza hoja ya kwanini kuliita baraza la wazee sio sahihi au linaweza kutishia uwakilishi wa vijana au kuonekana kwamba mtu akizeeka basi hata akiwa kiongozi wa siasa anaweza kuwa kwenye hilo baraza na hatari yake mwisho ndipo wataibuka wazee wa hovyo kusema baraza hilo ni lao na mwisho sifa ya baraza kupotea.

Mimi nikitetea upande wangu naona kuliita "Baraza la usimamizi wa taifa", ndio bora zaidi lakini naomba nieleweke hapa kwamba hatushindani kwamba jina bora ni lipi.? tunajaribu kuangalia hatari inayoweza kujitokeza kwenye jina hilo maana kiukweli kuna wazee wa vyama vya siasa ni wa hovyo sana na kwenye rasimu yangu nimeondoa kabisa wanasiasa kwenye baraza na kulifanya liwe huru kabisa.

Pia vyote ulivyosema ndio exactly of how Baraza lina oparate isipokuwa tu nimeweka check and balance la hali ya juu kabisa na mipaka ya baraza kwamba watatoa tathmini na muongozo sio kuchukuwa utendaji wa mamlaka hiyo.
 
Sawa kabisa naheshimu mawazo yako, niseme tu kwamba binafsi nimetumia Baraza la Wazee kwa sababu naelewa kitu kimoja aidha tukubali tusikubali ya kwamba Wazee huwa na makarama yao. Wana Busara na Hekima ambazo vijana wanapenda sana kuchukua na kuiga ya nje tukapoteza UTU wetu (Mila na Desturi) haswa kwenye maswala ya mali na hadhi.

Wazee kama kina Warioba na Prof. Shivji ndio walokuwa walimu wetu na bado ni walimu wetu wa maadili, wanaijua Historia yetu na hawana woga.Wakizungumza kitu wanazungumza kwa staha na mara nyingi baraka zao ndio hutuletea mafanikio. Nani asomsikilia ushauri na usia mzazi wake?

Hata Uhuru wetu ulipiganiwa na vijana lakini mawazo ya wazee ndio yalowapa Vijana wale kina AbdulWahid, Nyerere, Hamza Mwapachu na wengineo wakapata nguvu ya kuendeleza mapambano pamoja na kuswekwa ndani na wakoloni. Wazee walisimama na kwa usiri mkubwa kukieneza chama hadi mikoani kwa nguvu yao. Ndio maana Maalimu hakukosa hata mara moja kuwashuru wazee.

Isitoshe Wazee hawa sii rahisi kupokea rushwa kupitisha Sheria ama Mikataba mibovu tofauti na vijana ambao wanatafuta bado Utajiri wa kumikiki Mali.

Mwisho niseme hata nchi za Mataifa makubwa, Baraza la Senate limeshehena Wazee kwa sababu hawaogopi mtu, wana misimamo na wazuri sana kwenye kujenga hoja na kuhoji pale wanapoona tunaenda kombo.

Na trust me, mimi naweza kusoma mada humu ndani nikakwambia Umri wa mwandishi na uwezo wake katika kujenga hoja. Kwa hiyo, kuita Baraza la Wazee ina maana sawa na kusema Bunge la Senate ambalo linakuwa na watu waliitumikia Serikali na taasisi kwa miaka mingi wanajua haki na haramu.

Ni hivyo tu mkuu wangu, vinaja wana nafasi kubwa huwezi kuwatenga Wazee kwa mtazamo hasi wakati tunajaribu kuweka uuwiano baina yetu Wanawake.

Maasalaam
 
Pia wanaweza wakaingia wazee chawa, wakachafua mambo humo!(mf. akina Wasira), Jina ''baraza la usimamizi wa taifa'' kwangu naona sahihi zaidi kwa kufuatia mijadala ya hoja hapo juu. Japo kunaweza kuwa na kanuni za kuhakikisha uchawa haujipenyezi endapo jina likibaki ''baraza la wazee''
 
Exactly 💯 % kwanza kabisa kuliita Baraza la Usimamizi wa Taifa linatoa maana ya moja kwa moja kwamba kazi yake ni kusimamia misingi ya taifa, lakini kuliita Baraza la wazee kuna zalisha hoja kwamba wazee ndio baraza Lao, sasa hapo ndipo kijana watakosa uwakilishi wao, maoni yao na kuchangia hoja kwa uwezo wao.

Mimi kama muandishi wa rasimu hiyo ya katiba nasema hivi vijana wetu wana nafasi katika mchango wa taifa hivyo ni busara kuliita Baraza la usimamizi wa Taifa kisha ndani yake wazee wawepo na kwa sehemu kubwa ya baraza hilo wawe wazee, lakini si kuliita moja kwa moja ni baraza la wazee.
 
Hapana mkuu kwa kawaida Mabaraza kama haya yanatakiwa kuwa na wajumbe wa pande zote mbili kama vile - the jury mahakamani. Huwezi pata HAKI ikiwa wajumbe wote wanatoka upande mmoja kama ilivyo leo Bunge letu.

Hakuna jambo duniani tunaweza sote kuwa upande mmoja isitoshe Chawa anaweza kuwa sii wa CCM bali Chawa wa Chadema. Kinachotakiwa ni Uteuzi wa hawa Wazee kutokana na Sifa zao katika Utumishi.

Hata chukulia hii kesi ya Tundu Lissu wapo wanaoona ni mkosa na wengine wanaona hana hatia. Mahakama haiwezi chagua Majaji watatu ambao wote wako upande wa Tundu Lissu ama against. Itakuwansii Mahakama tena, Ushahidi ndio unawaongoza Majaji hao kutoa hukumu sio kwa sababu huyu ni nani..

Kwa hiyo, Baraza la Wazee au Senate linakuwa baraza tofauti na Wabunge wa jimbo ambao ni makada wa vyama vya Siasa. Hawa kazi yao kubwa ni check and Balance shughulu zote za Serikali kuhakikisha Demokrasia inasimama katika mising ile tuloizungumza - Utawala Bora.

Na hata tukirudi kutazama hulka nantwbia baina ya Wazee na vijana nadhani utakubaliana na mimi Machawa wengu tulionao ni vijana. Tena hawana aibu kujitambulusha kama wao ni Machawa! Miiko na Maadili yetu yanavunjwa na vijana sio Wazee.

Leo tuna mbegu za GMO katika mazao yote na afya zetu zipo hatarini kwa sababu ya maamuzi mabaya ya viongozi vijana. HIV, Saratani, sukari, magonjwa ya figo, yanaondia vijana miaka 40-50 wakato hawa wqzee wetu wanacheza na 90! Hujajiuliza kwa nini?

Mzee Wasira inabidi wewe ndio umuelewe nafasi aliyonayo ndani ya Chama kama ilivyo mimi leo nitegemee Heche kuikosoa Chadema au Tundu Lissu. Nitakuwa najidanganya mwenyewe! Isitoshe Barwza la Wazee halita deal na Siasa za vyama bali Utawala Bora. Ujana hautupi sifa ya kutatua migogoro hata siku moja infact wanaweza rushiana ngumi na matusi wai wenyewe.

Nazungumza haya kwa Uelewa mkubwa na sii dhana kwa sababu nimeziona kazi za mabaraza ya Senate nje jinsi yakifanya kazi. Chukulia la Marekani, wanapomwita Kiongozi yeyote kumhoji wazee wale hawana simile japo wamechanganyika pande zote Republican na Democratic lakini kwenye Maslahi ya Marekani hawana msamaha.

Anyway, najaribu tu kutetea hoja zangu kwa kile nachokiona BORA zaidi lakini sii lazima tuwe na Baraza hili maana wapo pia wasokubaliana kuwa na mihimili minne. Muhimu zaidi tunachojadili hapa ni DEMOKRASIA ILOBAGAZWA.
 
Uchaguzi wa ,2025ndio ulikuwa na mapungufu Sana!
 
Uchaguzi wa ,2025ndio ulikuwa na mapungufu Sana!
Kweli hapo ndio tulopofika kileleni lakini Mapungufu yalianzia ndani ya vyama vyote vya Siasa. Kuna watu walikatwa bila sababu, kuna watu walishinda kura za wanachama wakapigwa chini kwenye kutangazwa. Na baadhi vyama wagombea walikuwa viongozi walopita bila kupingwa.

Kwa hiyo, tusitazame tulipoangukia bali tukubali ukweli tulijikwaa wapi? Tuutazame mfumo nzima wa Uchaguzi toka kwenye Vyama vya Siasa maama mwaka 2025 binafsi nilifuatilia sana lawama za wagombea nchini zilikuwa juu sana.

Chadema hawakushiriki, lakini kitendo cha Mbowe na Lissu kugombana kilianzia wao kutaka kugawana madaraka! "Nani awe Mwenyekiti nannaninagombee Urais" hii kwangu haikuwa picha nzuri kabisa. Mwisho wake Lissu yuko ndani, Chama kinapigwa makombora kushoto na kulia. CCM ndio Usoseme, huko Zanzibar Muafaka na maridhiano yanafanywa na vyama viwili kupeana vyeo! Yaani ni shaghala baghala...

DEMOKRASIA IMEBAGAZWA...
 
Na mambo yanaishia kwenye makaratasi, utekelezaji ni Ziro!
 

1.wasiojulikana wanaoteka wanaharakati, na wapinzani, toka mwaka 2016 mpaka leo 2026, ni kundi la ulinzi la chama gani kati ya vyama 19 vilivyosajiliwa Tanzania?

2.Mgombea Huru akiruhusiwa kura zake zitalindwa na nani ktk mfumo huu wa kihuni unaosimamiwa na wateuliwa wa Raisi / Mwenyekiti wa CCM?

3.Raisi apunguziwe Madaraka ktk namna ya kuteuwa watu kama Majaji, Tume ya Uchaguzi, Spika wa Bunge na watendaji wake, nk.

Yeyote anayeshika nafasi ya Uraisi asiruhusiwe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha siasa. Mbona kwenye mambo ya mpira wa miguu, Raisi wa TFF, sio Raisi wa Yanga, Simba, au kilabu chochote?

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Raisi kwa sasa hivi ndiye anayeidhinisha jina la mgombe wa Uspika kupitia chama hicho. Kwa hiyo, Spika akishachaguliwa anakuwa loyal kwa Raisi [ mhimili wa serikali], badala ya mhimili wa Bunge.

4.Nafasi za Wakuu wa mikoa na Wakuu wa wilaya ziondolewe kwasababu tayari kuwa watendaji watumishi wa umma wanaoitwa RAS, na DAS. Wakuu wa mikoa na wilaya wako pale kuingilia na kuwakwamisha Wabunge waliochaguliwa na wananchi.
 

..vyama vya siasa kufanya madudu ktk chaguzi zao za ndani haihalalishi Tume ya Uchaguzi nayo kufanya madudu na uhayawani wakati wa uchaguzi mkuu.

..wagombea wa vyama wanaweza kutafuta chama chenye nafuu, lakini hawawezi kutafuta Tume nyingine itakayowatendea HAKI ktk uchaguzi mkuu nchi nzima.

..kwenye nchi za wenzetu kuwa na wakala wa uchaguzi wala sio hitaji la lazima. Chaguzi zao zinaaminiwa na washiriki wote. Kura zikishapigwa watu wote wanasubiria majibu ya Tume zao za uchaguzi na wanayaamini.

..Kwanini Watanzania hatuamini matokeo ktk chaguzi zetu, mpaka vyama, na wagombea, walazimike kuwa na mawakala, kuwe na waangalizi wa uchaguzi, mapolisi na wana usalama kila mahali?

..Tume ya uchaguzi na wasimamizi wanapaswa kuwa watu wanaoaminiwa kama vile wanavyoaminiwa Madaktari. Ukipeleka mgonjwa wako kupasuliwa unawaamini Madaktari, na huanzi kulazimisha uwe na wakala ndani ya chumba cha upasuaji.

..Kwenye nchi za wenzetu wananchi hupiga kura na kwenda kupumzika majumbani kwao kusubiria matokeo ktk vyombo vya habari.
 
Wajumbe wa hilo Baraza la Wazee watapatikanaje?...je sifa za kuwa mjumbe ni zipi ?...

Kwa kuwa umetamani uwe muhimili,je huo muhimili mkuu wake atapatikana vipi?...
 
Mkuu, sote ni watu wale wale hatutofautiani sana. Ikiwa unaweza kuiba kura ndani ya Chama ama kumtengua mtu aloshinda Uchaguzi ndani ya Chama, unawezaje kuwa na Ujasiri wa kunyooshea kidole Tume huru?

Kwa nini Viongozi wa vyama waruhusu kukata wagombea walichaguliwa na Wananchi halafu, waje wadai Demokrasia haipo upande wa Tume kwa makosa yale yale waloyafanya wao ndani ya Vyama vyao?

Mimi nikidhani demokrasia ni kuwapa Wananchi mamlaka ya kuchagua Viongozi wao, halafu inatokea Mgombea alokubalika na Wananchi akatwe ngazi.ya Chama tuone hakuna tatizo, ila yule aloshindwa kenda Uchaguzi Mkuu akashindwa ndio kadhulumiwa?
Infact HAKI sio ya mgombea ni ya Wananchi ndio maana ya Power to the people wanavyosema Chadema!

Katiba imewaka mamlaka kwa Wananchi kuchagua Viongozi na Wawakilishi wao very clear kabisa.. Halafu nyuma tunashuhudia Chama kinakata majina ya wagombea na kuweka majina wanayoyataka wao, hii tuite bado Demokrasia? Yaani Katiba inahusika wakati wa Tume tu tusiangalie mgombea anayepelekwa kugombea kapitaje?

Kisha mkuu wangu mambo ya Utekaji na Demokrasioa sioni yanasianaje! Kama unatala tuzingunzie hilo anzisha mada nyingine maana binafsi naamini Utekaji unafanywa na kundi dogo maalum la Wahuni wanaolipwa kufanya kazi hizi.

Kuna pahala nimesema ifike wakati Sheria ya Ukamataji ihitaji Polisi kujitambilisha kwa jina na namba yake na lazima awepo afisa wa Polisi wa kituo cha Polisi kilicho karibu na hapo.Mtuhumiwa asomewe mashtaka yake palepale.

Kama itahusu Usalama wa Taifa basi waje na arrest Warant ama barua ilotolewa na mahakama baada ya kuridhia kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka. Usalama wa Taifa utumike kwenye high profile cases sio upuuzi tunaosikia.

So, Hizi ni baadhi ya solution zinazotakiwa, na siwezi kabisa kusema Watekaji ni CCM ikiwa Sheikh Mwaipopo ameweza kuunda jeshi lake na kulitangaza wazi kabisa!

Jana nimeona wengine walotoka Chadema wakijiunga CCM kama kwamba kuna majeshi mengine tusoyajua kinyume cha Sheria ya majeshi nchini. This country is F...d up!
 
Wajumbe wa hilo Baraza la Wazee watapatikanaje?...je sifa za kuwa mjumbe ni zipi ?...

Kwa kuwa umetamani uwe muhimili,je huo muhimili mkuu wake atapatikana vipi?...
Ukiniuliza mimi nitasema hivi, Baraza la Wazee litachaguliwa pia na Wananchi. Utaratibu wake - Wataomba fomu kwa kujaza wasifu wao (Elimu, Utumishi n.k), Uanachama wa Chama cha Siasa, hili muhimu liwekwe wazi.

Upatikanaji wao - Kwanza hawatakuwa wengi labda nusu au robo ya idadi ya Wabunge.

Mathalan, Kila Wilaya itachagua Mjumbe mmoja halafu wengine watatoka taasisi muhimu za Kijamii kama tulivyofanya kwenye Bunge la Katiba bila kuwasahau TLS na Haki za Biadamu. Kikubwa ni uwezo wao wa kuhoji (Check and Balance).

Haya ni maoni yangu japo zIpo njia nyingi za kuwapata. Tunaweza pia kuiga nchi nyingine kama Kenya au Marekani wao wamefanyaje..
 
Mambo ni mengi Yako nyuma sana,Hata hao wazee walipwe pension,Bila kujali akifanya kazi wapi, angalia Singapore watoto tuu wanalipwa hawajazalisha chochote!
 
Mambo ni mengi Yako nyuma sana,Hata hao wazee walipwe pension,Bila kujali akifanya kazi wapi, angalia Singapore watoto tuu wanalipwa hawajazalisha chochote!
Kweli kabisa mambo ni mengi lakini kwanza tukubali Uhalisia tumejikwaa wapi?

Jiulize hivi, ikiwa Katiba ya mwaka 1977 ilifanyiwa marekebisha makubwa mwaka 1984 ikaongezwa Vyama vingi (Demokrasia) na Haki za Binadamu imetokeaje marekebisho hayo, leo hii hayaheshimiwi kabisa?

Iweje kila Sheria ilofanyiwa marekebisho toka 1977 ndio zinakiukwa sana kiasi kwamba unaweza kujiuliza hivi ni Sheria gani ndani ya Katiba hii inayoheshiwa? Wakiapishwa kuilinda wao ndio wanaoivunja. Katiba inasema Binadamu wote ni Sawa! Usawa huo upi?

Kwa hiyo tuna tatizo kubwa zaidi ya tunavyo fikiria, hata tukiandika Katiba Mpya kwa mwendo huu ni kujidaganya na kujitekenya wenyewe.

Tunahitaji muundo wa Serikali ambao Katiba itajieleza wazi wazi Kutenganisha Mihimili yote minne na sii kuonyesha tu shughuli zake bali iseme wazi Mihimili itakuwa HURU na haitaingiliwa na Mihimili mingine kufikia maamuzi yake.

Jambo jingine, kuna pahala huwa nawasikia watu wakisema Rais apunguziwe Madaraka. Sawa! Hayo madaraka ni yapi? utasikia asichague Majaji, Wakurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na wakuu wengine kwa sababu za Kisiasa zaidi - Sawa kabisa.

Lakini Wananchi wanateseka na nini zaidi tunaposema Rais ana mamlaka makubwa zaidi? Utakuta ni vyombo vya Usalama ndio vinalaumiwa zaidi pamoja na viongozi walipewa dhamana ya kutumikia Wananchi.

Kwenye Usalama wananchi wanateseka na Utekaji, Ukamataji wa watu bila kufuata sheria. Wafungwa kukaa muda mrefu jela bila kufikishwa mahakanani, Migogoro ya ardhi, Mashamba, Utaifishaji wa mifugo, Uhamishaji wa Wananchi bila kulipwa fidia, na hata wakilipwa hailingani na thamani ya ardhi n.k

Yaani adha za wananchi sio kero tena zinajenga chuki baina ya Wananchi na Serikali kwa sababu Utendaji haulinganu kabisa na matakwa ya KATIBA. Tunatokaje hapa ikiwa hali yenyewe ndio hii? Katiba haiheshimiwi wqla haithaminiwi kama kwamba Katiba ni kitabu cha Hadithi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…