Democrasia ni nini?

Democrasia ni nini?

Vianelly Vian

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
337
Reaction score
100
Nimekuwa nikifuatilia bunge la katiba na nimeona mapungufu mengi sana kubwa zaidi ni la wajumbe wengi kuto kujua maana ya democrasia.Tunapozungumzia democrasia huru ni kila kitu kuamuliwa kwa kupiga kura na mwenye kura nyingi ndiye anakuwa mshindi ukiangalia bunge unaona vyama vya upinzani havitaki kukubaliana na ukweli kuwa chama tawala kina wabunge wengi zaidi hivyo kila watakachokitaka lazima watakifanikisha kwasababu kura ndiye mwamuzi wa mwisho na mwenye kura nyingi ndiye mshindi.Kitendo cha wabunge wa upinzani Leo kutoka nje wakishinikiza matakwa yao yafanikiwe hiyo siyo democrasia na wala si uungwana,Kumekuwa na maoni kuwa kuutishwe mkutano wahadhara kukishitaki chama tawala kwa wananchi nimekuwa nikijiuliza wananchi hao ni wepi?maana kila mbunge anawananchi wake ambao wanamwamini na ndio waliompa kura,
Mwisho ushauri wangu ni kwamba mara nyingi nimeona vyama vya upinzani vinataka kuiona pepo bila kufa cha msingi kwanza wahakikishe wananchi tumewaamini kwenye majimbo na kuwapa kura nyingi ambazo zitawafanya wawe na wabunge wengi bungeni hivyo kufanikisha malengo yao pia Maana kwenye democrasia ya kweli maamuzi yote yanafanywa kwa kura na siyo kutoka nje ya bunge wala kuandamana
 
Nashindwa kuamini kuna mtu anaweza kuandika hivi! Unataka tuongelee demokrasia hiyo ya kupata katiba?

Demokrasia ilkosekana tangu serikali ilipowapora wananchi uwezo wa kujichagulia wenyewe wawakilishi wao kwenye mabaraza ya katiba, Tume ya Warioba na hata bunge la katiba. Na bila aibu bunge la JMT likalazimisha, kwa kuwa ni wengi, mwenyekiti wao ndiyo ateue nani awe wapi!

Demokrasia ilikosekana pale Rais, ambaye ni mwenyekiti wa CCM alipoona inafaa yeye na chama chake kujitwisha katiba kama ilani ya CCM wakati yeye na serikali yake walikuwa na msimamo wa wazi kuwa haina haja, huku wakijua wazi kuwa hawaihitaji, ila kwa makusudi tu wakaamu kuharibu mchakato huo.

Demokrasia ilikosekana pale CCM kupitia kwa wabunge wake, ambao kama ulivyosema ni wengi, waliposhindwa kuona siyo sawa kulazimisha Mwenyekiti wao awe na uwezo wa kuteua Wabunge wa bunge maalum, ambapo amefanya upuuzi wa kuhakikisha robo tatu ni WanaCCM.

Demokrasia ilikosekana pale CCM ilipoona ni vema na haki maoni ya wananchi yapuuzwe, Ila matakwa ya CCM yalazimishwe kwa kutumia wingi wao. Kwamba wanachi waliotaka serikali tatu ni wapuuzi na hawajua wanataka nini, ila kwa kuwa nchi hii ni ya CCm, na kwa kuwa wao ni wengi basi wana haki ya kuwaamulia wananchi wainshi vipi!

Hicho kilichofanyika kilikuwa uhuni toka mwanzo. Na ilikuwa wazi kuwa ile safari haikuwa ya kuleta katiba mpya. Na kama tukiendelea kuangalia upuuzi huo kinachofuata ni kupata katiba ya CCM na si vinginevyo. Pamoja na kuwa hata hii inayolalamikiwa ni ya CCM kwa asili yake, angalau CCm iliyoitengeneza ilikuwa ya Mwalimu, ambayo tofauti na hii yenu ile haikuwa na majambazi wengi. Kwa hiyo nadhani ni hatari kuwa na Katiba ya CCM hii ya leo iliyokosa utu.

Unataka kuongelea demokrasia? Nenda kajifunze kwanza demokrasia ni nini halafu tuongee. maana kwa ulichoandika ni wazi hukujua demokrasia ni nini wala misingi yake ni ipi!
 
Back
Top Bottom