nenda start tafuta program inaitwa "RUN" alafu andika "regedit" weka OK itakupeleka kwenye Registry.
Ila kwa kua hujui hilo sitokushauri uende kwenye System registry kufuta kitu chochote unless unauhakika ni keys zinazohusika na hiyo app unayotaka kufuta, unaweza futa kitu cha maana system yako nzima ikacrash.
Kuna option ya kusave registry kabla ya kufuta kitu, ili just in case umeharibu mambo uweze kurestore. Ila kua makini maana effects nyingine unaweza usizione kabla ya kurestart machine, ukarestart ikagoma kuwaka ukapata tabu kidogo ya kufix kama hujazoea.