Degree ya udereva miaka mitatu

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,678
Mtaalam wa kughushi vyeti ambaye pia ni mwana JF alikuwa kakaa bila kazi kwa miaka miwili. Baada ya kupigika sana kwa kukosa kazi na hela huku akijua fika kuwa hana elimu ya uhakika, akaamua kwenda kughushi vyeti. Na ili vyeti vyake viwe marketable kwenye interview pannel, akaamua kutengeneza vyeti vya kuanzia certificate, diploma na degree vya fani ya udereva.
Baada ya siku kadhaa wizara ya Nishati na madini ikatangaza nafasi za kazi nyingi sana zikiwemo za madereva.
Aka tuma haraka vyeti vyake na akaitwa kwa ajili ya usaili.
Kwenye meza ya usaili walikuwepo wadau mbalimbali wakajitambulisha, mmoja akasema, Mimi ni afisa mpelelezi wa polisi, mwingine akajitambulisha kuwa katoka NIT mtaalamu wa vyeti na mafunzo, mwingine akasema katoka Veta na mwingine TRA.
Jamaa akaanza kuona ndoto yake ikififa. Vyeti vyake vilikuwa kama ifuatavyo:~
Certificate ya udereva, muda mwaka mmoja. Daraja la ufauli Divisheni wani.
Diploma ya udereva, muda miaka miwili, daraja la ufaulu Divisheni wani.
Degree ya udereva, muda miaka mitatu daraja la ufaulu Divisheni wani.
Jamaa akaona atakamatwa akanikabidhi makablasha yake na kuaga kwenda chooni.
Hakurudi tena....
Nikaamua kufungua bahasha yake, nilichokutana nacho kilinitoa machozi kwa kicheko
 
hahahahahah duuuuuuuh noma sana hebu malizia na kilichokuwepo ndani ya bahasha
 
Hahahahaaaa bijibuji bwana umenifanya nitabasamu wakati nilikuwa na hasira za kufa mtu...
 
Ha h aha aaah!! Huyo ni noma.......hivi sio wewe Bujibuji.
 
Last edited by a moderator:
heeee maukubwa hayo jamani
kweli mjini ni shule na ukiwa na mbinu za maisha utaishi bila shaka

halafu wewe my dia ulipotelea wapi maana nilikutafuta kila chumba huonekani
na ikizingatiwa jf kuna vyumba vingi hadi vile vya uchochoroni sikukupata nkamu?
 

Chezea silent mode wewe. Niliwekwa kinyumba
 
nimesomea havard degree ya roho mbaya na ukorofi kwa miaka 4, nilifaulu kwa grade ya div 6.
 
Ha!ha!ha!haaaa.. Atakua Excel huyo.
 
Last edited by a moderator:
Ha!ha!ha!haaaa.. Atakua Excel huyo.

hahahaaa!! bila shaka ni wewe! Bujibuji nae muongo tu!

ww nafasi yako ilikuwa ni ipi bana kwenye interview pannel?

NIT sasa hivi kuna diploma ya driving.....! hio degree sasa kudadeki!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…