Definition mpya kwa mwaka mpya 2012

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Katika shughuli zangu napanda daladala mara nyingi sana. Kama ilivyo kawaida abiria wengi wanapenda kuzungumza sana. Wazungumzaji wakubwa niwapendao ingawa saa ingine wanakua kero ni wamama wafanya biashara sokoni wanaojikusanya kwenye kundi moja na wote kupanda basi moja kwenda na kurudi sokoni. Kutoka kwenye mazungumzo yao nimeunda definition mpya zifuatazo:

Matusi ya Nguoni: Maneno machafu yaliyoandikwa kwenye T-shirt au khanga
Maziwa Makuu: Mwanamke mwenye matiti makubwa
Kuvunja mwiko: Kusonga ugali mgumu wa kisukuma
Kufumania: Kushona sketi fupi sana
Kula rushwa:Kula chakula chenye pilipili nyingi
Vyombo vya Habari: Masufuria, sahani, na vijiko vinavyoyumika kwenye sherehe kubwa kama harusi sendoff nk.
Kupiga ramli:Kununua mzigo kwa bei iliyo juu kuliko bei ya soko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom