DED Mbinga kusalimia CCM oyee ni sahihi?

DED Mbinga kusalimia CCM oyee ni sahihi?

Kuna tatizo kubwa sasa hivi kwenye utumishi wa umma. CCM wameamua kuwaingiza kwa nguvu watumishi wa umma kwenye siasa. Haiwezekani eti viongozi wa ccm wakakugue miradi ya maendeleo ya halmashauri kwa kuwaamrisha watendaji kufanya hili na lile.

Je CUF nao wakifanya hivyo si itakuwa chaos tupu nchi hii.

Serikali ifanye kazi yake na chama kifanye kazi yake ya siasa.

Hilo la DED ni sehemu ya sarakasi tu zinazoendelea nchini kwa sasa.
 
ilikuwa tarehe 14 dec.2012 kwenye kijiji cha Utiri wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga (anaitwa Shaib Nnunduma) aliitwa kusalimia kabla ya mkuu wa mkoa kuanza kuhutubia,mkurugenzi alipoitwa alianza na salam ya CCM oyee .

Mkurugenzi wa halmashauri ndiye msimamizi wa uchaguzi wa madiwani,wabunge na rais kwenye halmashauri husika sasa mkurugenzi anavyosalimia hadharani CCM oyee ,je kwenye kusimamia uchaguzi atafanya haki kwa vyama vyote vinavyoshiriki ichaguzi ?

maoni yangu sasa ni wakati muafaka wa kuwa na tume huru ya uchaguzi na tume iwe na watendaji wake watakaosimamia uchaguzi kwenye majimbo ya uchaguzi.
Huyo Shaibu namfahamu toka zamani na Mwaka 2010 nilikuwa Mbinga kabla na Baada ya Uchaguzi.Nilipata taarifa toka kwa Mwalimu Mkuu mmoja wa Shule fulani pale Mbinga Mjini aliekuwa akisimamia Kituo Cha Uchaguzi cha Masumuni akinieleza kwamba DED Shaibu aliwambia kwamba Ole wake Mwalimu Mkuu yeyote asimamie Kituo na CCM ishindwe kwenye kituo atakachokuwa amepewa Mwalimu huyo!Nilizidi kumuhoji yule teacher akanambia kuwa DED alihaidi kutoa adhabu ya kushushwa cheo na kuhamishwa Mjini kupelekwa Nyasa shule za Mipakani au Liparamba kule Machimboni.Huyu DED Janga la Mbinga.
 
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!

Ninauhakika tena bila shaka (Tume ya Katiba) hajatumia ubongo kufikiri ila katumia kamasi kwa kuwa mtu mwenye akitili timamu hawezi kutoa majibu rahisi na yasiyo na mtazamo wa kifikra kama hili jibu hapo juu. Binafsi nasema huyo DED hafai katika kiti chake kwa sababu chukulia kwamba angekosea kwenye salamu yake akasema CDM oyeee nini kingempata, hivyo ambacho kingempata kwa kusema CDM OYEE NDICHO KINACHOSTAHILI AKIPATE HATA KWA KUSEMA CCM OYEE. MAWAZO YANGU
 
Chadema acheni kudandia hoja; mkae chini mmalize mikwaruzano ndani ya chama chenu. DED hapaswi kuhukumiwa alikuwa anatekeleza sera za CCM kwa vitendo
 
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!
Kodi inalipwa tu na wanachama wa hicho chama alichokitaja. Acha kuharibu utendaji wa serekali na nyinyi ndio mnasababisha watu wanang'ang'ania madaraka hata kama hawana uwezo kisa tu wanatoa salamu za kinafiki
 
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!
standing orders 2009 unajua zinasemaje kuhusu vyama?we mbumbumbu squared...huyo DED anajipendekeza tu na ukichunguza utakuta hati chafu nyingi sana kwenye halmashauri yake
 
Chadema acheni kudandia hoja; mkae chini mmalize mikwaruzano ndani ya chama chenu. DED hapaswi kuhukumiwa alikuwa anatekeleza sera za CCM kwa vitendo
nyinyi wa wapi?kanuni za kudumu za utumishi 2009 zinakataza maneno/slogan za kisiasa kwa watendaji..huu ni muendelezo wa uvunjaji sheria wa ccm..mmeshikwa pabaya
 
Maisha mazuri yanapatikana sehemu tatu tu. Kwa YESU, KWA MTUME MUHAMAD SAW NA CCM

Ndo hapo wenye akili timamu tunatambua wazi kuwa ajenda ya udini ni ya CCM tangu 2010 na wanaendelea nayo hadi 2015 maana hawana ajenda muhimu ya kuweza kusikilizwa na wananchi,Je wapagani au wasio na dini hizo mbili au ilo li ccm hawana maisha mazuri?.Try to put your brain on assignments
 
Kuna tatizo kubwa sasa hivi kwenye utumishi wa umma. CCM wameamua kuwaingiza kwa nguvu watumishi wa umma kwenye siasa. Haiwezekani eti viongozi wa ccm wakakugue miradi ya maendeleo ya halmashauri kwa kuwaamrisha watendaji kufanya hili na lile.

Je CUF nao wakifanya hivyo si itakuwa chaos tupu nchi hii.

Serikali ifanye kazi yake na chama kifanye kazi yake ya siasa.

Hilo la DED ni sehemu ya sarakasi tu zinazoendelea nchini kwa sasa.
Tatizo la kubwa sana CCM Hawajagundua kutaka kuteka watumishi wa umma hasa Halmashauri katika mambo ya kisiasa,ilo litakuwa pigwa kubwa sana kwao.Watumishi wengi hivi sasa wa Serikali kuu na Halamshauri hawako katika good terms na wanasiasa hawa na hizi Mikakati ya kuburuza watumishi katika mikutano na kuzomewa na wananchi itakula kwao tu subiri 2015 hali itakuwa mbaya sana kwa ccm.CCM itakuwa inapambana na CHADEMA na Watumishi kwa Sehemu nyingine.
 
Kinadharia ni sahihi lakini ki vitendo ni sahii. Ni ukaidi wetu tu hatutaki kuuona ukweli kama DED ni MuCCM na hata kuwa CUF wala CHadema Nani anbisha hilo?
 
Alie kua DED wa jiji la mbeya 2010 alipewa Ubunge viti maalum kupitia Chadema! think twice!
 
Back
Top Bottom