DED Mbinga kusalimia CCM oyee ni sahihi?

Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,606
2,000
ilikuwa tarehe 14 dec.2012 kwenye kijiji cha Utiri wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga (anaitwa Shaib Nnunduma) aliitwa kusalimia kabla ya mkuu wa mkoa kuanza kuhutubia,mkurugenzi alipoitwa alianza na salam ya CCM oyee .

Mkurugenzi wa halmashauri ndiye msimamizi wa uchaguzi wa madiwani,wabunge na rais kwenye halmashauri husika sasa mkurugenzi anavyosalimia hadharani CCM oyee ,je kwenye kusimamia uchaguzi atafanya haki kwa vyama vyote vinavyoshiriki ichaguzi ?

maoni yangu sasa ni wakati muafaka wa kuwa na tume huru ya uchaguzi na tume iwe na watendaji wake watakaosimamia uchaguzi kwenye majimbo ya uchaguzi.
 
ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,211
0
Kwa mtazamo wangu sio sahihi kwa sababu DED ni mtumishi wa umma,na sheria za utumishi haziruhusu mtumishi kushabikia chama chochote cha siasa awapo kazini. Huo ni ulevi tu wa serikali ya ccm,kwa kuvunja kanuni na taratibu za nchi.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,742
2,000
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!

Usipende kutoa majibu raisi bila kuushirikisha vizuri Ubongo, tungekuwa katika mfumo wa Chama kimoja sawa lakini kwa sasa si sahihi kwa sababu tupo katika mfumo wa vyama vingi, na hili linatokea kwa sababu uteuzi wa hawa MaDED hauna tofauti na uteuzi wa wakuu wa Mikoa au Wilaya kwani hakuna sifa zilizowekwa kama vigezo ili mtu kupewa hiyo nafasi.
 
mbayaaa

Senior Member
Oct 17, 2012
132
195
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!

C tatizo lako N TATIZO LA UFAHAM MDOGO wa sheria ulionao ndo unakusumbua, DED cyo political leader yeye n mtendaji na anawatumikia wananchi wote ivyo apashwi kuonesha bias yoyote ya kisiasa au kiitikadi.
 
Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,047
0
Hakuna chuo cha u-DED, Hivyo lazima DED, apiganie maslahi ya mwajiri wake, kwani ikitokea mabadiliko yoyote ya kisiasa, teuzi zote zaweza kuwa mashakani. hivyo anapalilia unga wake!!!!
 
Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,158
2,000
Sio sahihi hata kidogo, kutekeleza sera za chama kinachoongoza hakumfanyi muajiriwa wa serikali kuwa mashabiki au wanachama wa chama hicho. Kumbuka DED ni muajiriwa kama muajiriwa mwingine yeyote ndani ya serikali na ile sio post ya kisiasa kama DC.....
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,476
2,000
kwahiyo Polisi,jeshi nao waseme CCM oyee kwa sababu na wao wanatekeleza sera za CCM,Hata hivyo kumbuka DED ni msimamizi wa uchaguzi.

Ni kweli mkuu na lengo la kufanya hivi ili watendaji wa serikali waweze kufanya kazi kwa uhuru, utekelezaji wa ilani unafanywa kwa kutekeleza yale yaliyoamuliwa na bunge na baraza la madiwani hivyo from there hawa watendaji including DED wote ndio wanapata base ya kufanya mambo yao. Sasa huyo Tume ya Katiba anavyosema yupo sahihi anapotosha
 
Zimamoto

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
464
195
Kama kungekuwa na tume sahihi ya maadili ya viongozi, hiyo kauli inatosha kumwajibisha huyo DED. Kwa maoni yangu hana hadhi ya kuwa DED.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,476
2,000
Hakuna chuo cha u-DED, Hivyo lazima DED, apiganie maslahi ya mwajiri wake, kwani ikitokea mabadiliko yoyote ya kisiasa, teuzi zote zaweza kuwa mashakani. hivyo anapalilia unga wake!!!!

Ni kweli hakuna chuo cha U-DED lakini kila halmashauri lazima iwe na msimamizi ambae anawasimamia watumishi hivyo ni lazima awe mtumishi wa serikali na tena mkuu wa idara, tunaposema anateuliwa maana yake kuna mchakato unafanyika kumpata mtu ambae anafaa na waziri mwenye dhamana anatangaza kumteua rasmi lakini lazima awe na qualification na ndio maana ili uwe DED lazima uwe mkuu wa idara katika moja ya halmashauri.

DED ni mtumishi wa serikali hata kije chama kingine mkuu ataendelea na utumishi wake serikalini kitakachotokea tu ni kubadilisha majukumu yake ya kikazi kama utaingia utawala mwingine na ikaonekana kuna haja ya kufanya hivyo. Kwahiyo hata kama ni nafasi ya kuteuliwa bado ni mtu ambae sifa mojawapo lazima awe mtumishi wa halmashauri mojawapo na ma-DED wengi walikuwa ni wakuu wa idara mojawapo katika halmashauri tofauti na nafasi kama ya ukuu wa wilaya akiingia kiongozi mwingine na wewe unakwenda na maji
 
pamoja sana mkuu.
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,948
2,000
Ni sahihi, kwani DED anatekeleza sera za chama gani? acha umbumbumbu wewe!
We ndo mbumbumbu kiongozi.Ni kosa DED kusalimia salamu za chama maana hawakilishi maslahi ya chama kwenye halmashauri.Akionyesha mapenzi yake kwa chama fulani anaonyesha kutojiamini na pengine amepata nafasi hiyo kama hisani kutokana na maslahi ya chama chake.
Hafai hata ukiangilia utendaji wake utabaini mapungufu makubwa na upendeleo maana anatekeleza maslahi ya chama.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom