acer
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 1,595
- 142
*MKURUGENZI MALINYI AKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 6 ZA WALIMU KWA SIKU 23.*
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi ndugu _Marcelin Ndimbwa_ amefanikiwa kukamilisha ujenzi wa nyumba 6 za walimu ambapo kila nyumba itakuwa na uwezo wa kubeba kaya/familia sita pamoja na matundu 24 ya vyoo ambao ni mradi wa SEDEP.
Ujenzi huo ulianza mara moja baada ya tangazo la mh Rais alilotoa mwishoni mwa mwezi novemba kwa kuwataka wakurugenzi wote kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu, ndugu Ndimbwa (Mkurugenzi Mtendaji) aliamua kufunga mkanda na kulivalia njuga ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka iwezekanavyo na kuwa tayari kwa matumizi ya makazi hadi kufikia kipindi mkurugenzi aliendelea na shughuli za halmashauri kutokea hapo hapo site (Kwenye ujenzi wa mradi) na hatimaye ndani ya siku 23 kazi hiyo imekamilika kama inavyoonekana pichani.
Endapo miradi ya namna hiii isopokamilika kwa wakati imeelezwa moja madhara ya ni fedha kurudi World bank, hivyo ingepelekea serikali kupata hasara pamoja na kufutwa kwa msaada huu.
Tunapongeza juhudi hizi za wasaidizi na watendaji wa mh rais katika kuhakikisha serikali inatumia vema fedha za misaada pamoja na kusimamia vema mapato na matumizi ya fedha za umma na serikali yetu.
Hakika tunahitaji utendaji wa wakurugenzi wengi wa mfano wa ndugu Marcelin Ndimbwa ili kutimiza adhma ya serikali katika kuwatumikia wananchi wake kwelikweli.